buswelu moja
JF-Expert Member
- Aug 24, 2014
- 226
- 180
POLISI ARUSHA WAINGIA LAWAMANI PART (11).
Mwandishi wetu,
Ndugu wana jamvi leo kama nilivyowahaidi kuendelea na ule mvutano uliopo baina ya polisi Arusha na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali(DPP) Arusha baada ya ofisi ya mwanasheria huyo kutoa amri ya kurejeshewa hati miliki yake mara baada ya shauri lililofunguliwa dhidi yake kumalizika lakini polisi wameshindwa kutii amri hiyo kutokana na sababu ambazo hazijawekwa wazi hadi sasa,jana tulihaidi kumzungumzia DAHNI MAKANGA katika sakata hili anahusika vipi…….ENDELEA
DAHNI MAKANGA.
Huyu alikuwa ni mkuu wa wilaya mstaafu wa wilaya ya KIBONDO pamoja na mbunge mstaafu wa jimbo la BARIADI MASHARIKI,kwanini anahusishwa katika sakata hili iko hivi kiongozi huyu ameoa nyumba moja na mfanyabiashara anayepigwa danadana na polisi kuhusu hatimiliki yake aitwaye MATHEW MOLLEL.
MAKANGA NA MOLLEL hawa wameoa nyumba moja huko BARIADI ambapo MAKANGA ameoa dada mkubwa huku MATHEW ameoa mdogo mtu.
Mahusiano ya wawili hawa yalikwua ya karibu sana hadi yalipokuja kutibuka hivi karibuni baada ya kuingia katika ugomvi wa kugombea hatimiliki ya kiwanja hicho kilichopo eneo la MIANZINI jijini Arusha.
Ilikuwa hivi MAKANGA miaka ya nyuma wakati akiishi mkoani Arusha alikuwa akimiliki viwanja viwili moja kilichopo NJIRO na kingine MIANZINI wakati huo miaka ya tisini yalikuwa ni mashamba.
Mara baada ya MAKANGA kuondoka mkoani Arusha na kisha kurejea mkoani MWANZA kabla ya kuanza utumishi serikalini alikuwa akifanya biashara na kampuni ya TBL mkoani Arusha lakini kwa taarifa ambazo hazijadhibitishwa hadi sasa ni kwamba alikimbilia mkoani MWANZA kutokana na kuhusishwa na masuala ya hundi feki katika biashara zake.(sijui siku hizi idara inayochuja wakuu wa wilaya hawakufuatilia background ya huyu kiongozi)
Akiwa mkoani MWANZA walianza kufanya mawasiliano na MOLLEL na kisha kuingia makubaliano ya kuuziana shamba hilo lililoko eneo la MIANZINI baada ya lile la NJIRO kuuzwa kinyemela na wajanja wa mjini na ndipo mazungumzo yalipoanza kufanyika kwa kuwahusisha wake zao na hatimaye biashara ikafanyika.
Mara baada ya muda MOLLEL akaanza kufanya utaratibu wa kupima shamba hilo na kisha kuanza kutafuta hatimiliki ya eneo hilo katika ngazi mbalimbali jambo ambalo alifanikiwa miaka 9 iliyopita.
Ugomvi ulianza mwaka 2014 wakati MAKANGA alipokujana familia yake mkoani ARUSHA na kisha kupokelewa na MOLLEL ambapo walikuwa wakifikia katika nyumba yake ambapo taarifa zinadai aliingiwa na tamaa baada ya kuona ya kwamba mme mwenzake amepiga hatua .
Lakini MAKANGA akiwa mjini ARUSHA inadaiwa alikutana na watoto wa mjini akiwemo MOSES KING”ORI huyu kwa wasiomjua anafanya kazi katika kampuni ya RIVERSIDE SHUTTLE ya mkoani Arusha ambapo inadaiwa kwamba alimwambia MAKANGA angempatia milioni 200 endapo angempatia kiwanja cha MIANZINI ambapo tayari alikuwa ameshakiuza na hakipo mikononi mwake ghafla MAKANGA alibadilika na ndipo akaanza njama za kutaka kukipora kiwanja hicho.
Itakumbukwa ya kwamba tayari wakati anakuja ARUSHA alikuwa ameshakuwa D.C wa KIBONDO na ndipo kwa kushirikiana na aliyekuwa mkuu wa upelelezi(RCO) DUWANI NYANDA wakapanga njama za kutaka kumpora MOLLEL kiwanja hicho kwani ahadi ya milioni 40 ilitolewana MAKANGA kwa DUWANI na askari waliokuwa chini ya ofisi yake endapo wangefanikiwa kumpatia mikononi. Na unajua jinsi baadhi ya askari wa ARUSHA walivyo na njaa ilikuwa ni balaa.
Mnamo mwezi Agosti mwaka 2014 MAKANGA akiwa D.C wa KIBONDO alikuja mkoani ARUSHA na kisha kukutana na DUWANI NYANDA na akampatia askari wane ambao walikwenda kwa miguu kutoka polisi ARUSHA hadi katikaofisi zake zilizopo jingo la NEW SAFARI HOTEL na kisha walipofika kazi ya kuanza kupekua hatimiliki katika ofisi hiyo ikaanza huku MOLLEL akiwekwa chini ya ulinzi ofisini kwake.
Wakiwa ofisini hapo walipekua kila kona lakini hawakufanikiwa kuipata hatimiliki hiyo na ndipo MAKANGA alipowaamuru askari kuvunja SAFE ya bwana MOLLEL lakini askari hao walipinga amri hiyo na ndipo shughuli ya upekuzi ikahamia nyumbani kwa bwana MOLLEL.
Askari walimchukua bwana MOLLEL hadi nyumbani kwake wakiambatana na MAKANGA na ndipo walipofika nyumbani kwake MAKANGA akaingia chumbani kwa mme mwenzake na kisha kuanza kufunua kitanda ,kabati,droo na hata kurusha nguo za ndani za mke wa MOLLEL kwa madai anatafuta hatimiliki hiyo.
Jitihada za kuipata hatimiliki hiyo ziligonga mwamba na ndipo wakamchukua MOLLEL hadi polisi na kumweka chini ya ulinzi wakimtishia kummaliza endapo asipowapatia hatimiliki hiyo na ndipo MOLLEL baada ya kuona hatari kubwa ya maisha mbeleni mwake aliamua kutoa siri ya kwamba hatimiliki hiyo iko mikononi mwa wakili wake DUNCAN OOLA ambaye alitafutwa na kuja kuikabidhi mikononi mwa polisi.
Jambo la ajabu wakiwa katika ofisi hizo DUWANI NYANDA na MAKANGA waliongea lugha ya kisukuma wakishauriana kuondoka na hatimiliki hadi MOSHI katika ofisi za msajili wa hatimiliki kwa lengo la kuibadili jina lakini kumbe wakili DUNCAN OOLA alikuwa akiwasikia vyema barabara na ndipo alipoomba taratibu za kukabidhi hatimiliki hiyo zifanyike ikiwa ni pamoja na kuandikisha fomu ya SEIZE hatua iliyotekelezwa na ndipo mpango wa kumpora hatimiliki hiyo ukashindikana ikakabidhiwa polisi hadi leo hii inasemekana bado ipo polisi ingawa hatuna uhakika kama bado ipo.
Baaada ya muda MOLLEL aliachiwa kwa dhamana na kisha kuondoka lakini kwa masharti ya kwamba kila jumatatu ya kila wiki anatakiwa kuripoti polisi sijui hapa polisi walitumia sheria gani?utaratibu huo wa kuripoti polisi umeisha katika siku za hivi karibuni na haijulikani uliisha vipi.
Sasa DUWANI NYANDA hayupo tena ARUSHA lakini kazi hiyo amemwachia RCO msaidizi STELLA ambaye anatajwa kutangaziwa dau endapo akifanikiwa kumkabidhi MAKANGA hatimiliki hiyo jambo ambalo STELLA anahangaika nalo hadi sasa ingawa taarifa zinadai kwa sasa yuko likizo nje ya mkoa wa ARUSHA.
MAELEZO YA KAMISHNA WA ARDHI.
Kamishna wa ardhi msaidizi kanda ya kazkazini,SUMA MWAKASITU ametolea ufafanuzi suala hili na kusema kwamba polisi wanafanya makosa makubwa kushikilia hatimilki hiyo endapo kama kesi imemalizika mahakamani.
MWAKASITU anafafanua kwamba polisi hawana mamlaka ya kuendelea kuishikilia hatimiliki hiyo kwa kuwa tayari kuna agizo limetolewa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali mkoani ARUSHA kwamba wamkabidhi hatimiliki hiyo bwana MOLLEL na hapa anasisitiza kwamba polisi hawako juu ya sheria .
MSAJILI WA HATI
Kuna mtu mmoja anaitwa bwana BUNDALA ni msajili wa hati kanda ya kazkazini huyu amekuwa akikwepa kuzungumzia suala hili na itakumbuka ya kwamba bwana MOLLEL mwaka juzi wakati sakata hili linaendelea alifika katika ofisi yake kuweka CAVIET kwa usalama wa hatimiliki yake lakini cha ajabu MAKANGA naye mwaka huu amefika katika ofisi hiyo hiyo kuweka CAVIET ina maana hapa CAVIET imewekwa juu ya CAVIET kituko cha mwaka ……
Jambo jingine ni kwamba ofisi ya msajili huyu inatajwa kupokea rushwa kutoka kwa MAKANGA na kutumia ukabila katika sakata hili kwa kuwa ilimkubalia MAKANGA kuweka CAVIET ihali wakijua ni makosa lakini pia hawakutaka kujipa muda kujiridhisha kwanza kabla ya kumkubalia kuweka CAVIET.
Jambo jingine ni kwamba ofisi hii walituma barua kwenda benki ya SAVINGS AND FINANCE mkoani ARUSHA kutaka kujua endapo MOLLEL amechukua mkopo katika benki hiyo au la baada ya tetesi kuzagaa kwamba bwana MOLLEL amechukua mkopo katika benki hiyo .
Lakini jambo la ajabu ni kwamba nakala ya CAVIET ilipelekwa benki hiyo lakini MOLLEL hakupewa nakala hadi leo ni kwamba alipigiwa simu na benki kwamba kuna barua yako hapa imetoka MOSHI na ndipo alipoenda akakuta CAVIET na sasa anahoji kwanini yeye hakupewa nakala na ofisi hiyo ihali ina nambari ya sanduku lake la posta? Hapa kuna jambo limejificha… lakini tutalibaini tu
USIKOSE EPISODE YA 3 MWANAJUKWAA AMBAPO TUTAMWANGAZIA HUYU MOSES KING”ORI NI NANI NA KWANINI AMETOA OFA YA KUNUNUA KIWANJA HICHO CHA MOLLEL KWA SH,MILIONI 200?
(ndugu wanajukwaa sahamani najaribu ku attach ile barua ya mwanasheria mkuu wa serikali kwenda polisi inaleta shida katika attachment lakini nakuhaidi punde muda si mrefu nitaitupa humu na nyie muweze kuiona nawaombeni radhi sana)
ALAMSIKI……………..