Baba mzazi wa Mtanzania aliyeuawa huko Israel awasili Huko Israel

EricMan

JF-Expert Member
Oct 5, 2017
1,725
2,924
Baba mzazi wa Mtanzania aliyeuawa huko Israel, Joshua Mollel yuko nchini humo kwa mwaliko wa Wizara Mambo ya Nje ya nchi hiyo ambapo akiwa huko alishiriki hafla ya kutoa heshima kwa Watanzania wawili waliouawa kwenye mapigano kati ya Israel na Hamas huko Gaza.

Desemba 14, 2023, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, January Makamba alieleza kwamba walipokea taarifa kutoka Serikali ya Israel ikiwajulisha kwamba Joshua aliuawa na Hamas tangu Oktoba 7, 2023.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Desemba27, 2023, Naibu Balozi wa Israel katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda, Dvora Dorsman Yarkoni amesema Loitu Mollel ambaye ni baba mzazi wa Joshua Mollel yuko Israel alikokwenda kwa mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi hiyo.

Amesema katika ziara yake, Mollel ameshiriki hafla kutoa heshima kwa Watanzania wawili waliouawa na kikundi cha Hamas huko Gaza (Clemence Mtenga na Joshua Mollel), hafla iliyoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Eli Cohen.

(Imeandikwa na Peter Elias na Sute Kamwelwe)

mwananchiupdates
 
Wanatoa vip heshima na mwili wanao Hamas ? Na ule wa kwanza si ulishazikwa wa Mtega...

Mbona mnachanganya!?
 
Siasa ni nyingi duniani
Unaweza kujiuliza kun haja gani huyu mzee kwenda mpaka huko!?

Hapa kuna siri kubwa kwa kweli kama dada FaizaFoxy alivyosema ,hapa kuna tatizo kubwa kwa kweli.

Kuna yule aliyekufa ukraine mbona wazazi wake hawajakwenda ?
 
VIta za watu weupe ila wanakufa Wa Tanzania wanafunzi.

Russia hivyo hvyo

Israel hivyo hivyo
 
Najaribu tu kujiuliza, hivi ni kwa nini wazazi wa yule mwanafunzi mwingine Mtanzania aliyeuawa huko Israel nao hawakualikwa pia?Kwa nini amealikwa huyu mmoja tu????? Naona kama kuna double standards. Anyway, tuwaachie wao wenyewe.
Wahuni hawa wanatuchezea ,eti uliona wapi wakristo wakitoa salamu na maiti haipo 😅

Hawa maiti wanayo maana wanadai bado inashikiliwa mateka na Hamas.
 
Najaribu tu kujiuliza, hivi ni kwa nini wazazi wa yule mwanafunzi mwingine Mtanzania aliyeuawa huko Israel nao hawakualikwa pia?Kwa nini amealikwa huyu mmoja tu????? Naona kama kuna double standards. Anyway, tuwaachie wao wenyewe.
Mbona walienda kwenda kuchukua Maiti Israel walienda wawili kufuata mwili ulitaka waende tena?
 
Najaribu tu kujiuliza, hivi ni kwa nini wazazi wa yule mwanafunzi mwingine Mtanzania aliyeuawa huko Israel nao hawakualikwa pia?Kwa nini amealikwa huyu mmoja tu????? Naona kama kuna double standards. Anyway, tuwaachie wao wenyewe.
Huenda marehemu alishobokea upande wa mayahudi akipigana na Hamasi.

Usipoiachia akili yoko ijisimamie unaweza kuwachukia Hamas Kwa propaganda za wazayuni.

Dunia Ina Siri
 
Unaweza kujiuliza kun haja gani huyu mzee kwenda mpaka huko!?

Hapa kuna siri kubwa kwa kweli kama dada FaizaFoxy alivyosema ,hapa kuna tatizo kubwa kwa kweli.

Kuna yule aliyekufa ukraine mbona wazazi wake hawajakwenda ?
kijana kuwa na adabu unamuita ajuza wa miaka 60 Dada (binti)
 
Unaweza kujiuliza kun haja gani huyu mzee kwenda mpaka huko!?

Hapa kuna siri kubwa kwa kweli kama dada FaizaFoxy alivyosema ,hapa kuna tatizo kubwa kwa kweli.

Kuna yule aliyekufa ukraine mbona wazazi wake hawajakwenda ?
Unajua ya kwamba huo mwili wa kijana wake haujapatikana????
 
Unaweza kujiuliza kun haja gani huyu mzee kwenda mpaka huko!?

Hapa kuna siri kubwa kwa kweli kama dada FaizaFoxy alivyosema ,hapa kuna tatizo kubwa kwa kweli.

Kuna yule aliyekufa ukraine mbona wazazi wake hawajakwenda ?
Mzee kaenda kulipwa fadhila baada ya mwanae kufia vitani
 
Back
Top Bottom