Polisi Arusha nao Pia Wanataka Amani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Arusha nao Pia Wanataka Amani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndallo, Nov 8, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,131
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Idadi kubwa ya polisi ambao jana walikua wamefurika katika viwanja vya mahakama waliomba viombo vya habari visaidie kuweka wazi mgogoro wa Arusha ili amani ipatikane.

  "Jamani tusaidieni leo tumekaa siku nzima hapa na jambo hili litaendelea sasa hali hiii itaendelea mpaka lini Arusha ni mji wa kimataifa, mnataka amani ipatikane andikeni kila kitu msiogope mtu ili amani irejee Arusha," alisema polisi mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini. Souce Gazeti la Mwananchi!

  Maoni yangu na mtazamo wangu ni kua hii imeshajidhihirisha kua hata hawa askari wanataka amani ndani ya jiji hili la Arusha na kwa mtazamo wangu inaoneka kabisa kua askari hawa wanapata amri kutoka ngazi za juu serikalini kuwazibiti wapinzani. Waziri wa mambo ya ndani tafadhali ingilia kati hili swala kwakua waziri mkuu bwana Mizengo Pinda kashashindwa kutatua migogoro kati ya polisi na wanachama wa Chadema.
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Waziri wa mambo ya ndani ataingiliaje wakati naye anaona na huenda anajaribu kufanikisha mikakati yote mizuri au mibaya dhidi ya viongozi wa vyama.
   
 3. mtoto wa mfugaj

  mtoto wa mfugaj Senior Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siasa siasa,siasa za bongo haziishi vioja,wananchi kama hawakutaki leave them alone.polisi mikwara ya nini?
   
 4. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  yaani polisi analalamikia kazi yake? Si bora aiache tu. Nalog off
   
Loading...