Polisi ang'olewa meno sita Shinyanga

Polisi ang'olewa meno sita Shinyanga

Chacha Willy

Senior Member
Joined
Mar 30, 2014
Posts
103
Reaction score
36
Kumetokea tukio la aina yake katika mgodi wa madini ya almasi wa Mwaduiuliopo katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Pc Idd Makame(25) amejeruhiwa vibaya mdomoni kwa kung'olewa meno sita baada ya kupigwa jiwe kwa kutumia kombeo (kwa lugha ya kisukuma Nh'ago) na watu wanaodaiwa kuwa ni wachimbaji haramu wa madini katika mgodi wa Mwadui wakati akitimiza wajibu wake wa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

Tukio hilo limetokea Novemba 21,2014saa mb ili na robo usiku katika eneo la Tanex katika mgodi huo wakati askari huyo akiwa na askari wenzake wakiongeza nguvu baada ya askari wa kampuni ya ulinzi ya Zenneth inayolinda mgodi wa Mwadui kushindwa kuwadhibiti wachimbaji wadogo wa madini maarufu "Wabeshi" waliotaka kuingia kwa nguvu mgodini wakiwa na silaha za jadi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kampuni ya ulinzi ya Zenneth Security Services Limited inayolinda mgodi huo ilipata taarifa kuwa kuna wachimbaji haramu maarufu kwa jina la Wabeshi walitaka kuvamia mgodi wakiwa na silaha za jadi ikiwemo mishale, mikuki, virungu, makombeo, mapanga.

na fimbo. Kufuatia hali hiyo askari hao wa Zenneth walifika eneo la tukio kuwadhibiti Wabeshi hao lakini ghafla walianza kushambuliwa kwa silaha za jadi yakiwemo marungu, mishale, mikuki na makombeo. Baada ya kuona wanazidiwa nguvu,askari wa Zenneth walilazimika kuomba msaada wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) cha jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga.

Baada ya askari wa FFU kufika eneo la tukio nao walianza kushambuliwa na Wabeshi hao ,ndipo PC Idd akapigwa jiwe mdomoni kwa kutumia kombeo na kung'oka meno sita mdomoni na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu. Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Zenneth Security Services Limited Elisha Ndulu amethibitisha uwepo wa tukio hilo.

Naye mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum amesema Pc Idd alipigwa na kitu chenye ubapa mdomoni na kusababisha meno sita kung'oka na anaendelea kupatiwa matibabu,hali yake inaendelea vizuri. Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari wanawashikilia watu wanne kwa mahojiano zaidi na wanaendelea kufanya uchunguzi.
 
Wamezidi kutumika na maccm waache wadundwe tu...wajue wananchi hawafurahii wanayofanya...
 
Tanzania watu wanamaasira na hii CCM. Sio mbali kabla ya hii nchi kulipuka kama iliyotokea Tunisia.
 
Wange muua tu maana huo mgodi haulipi hata cent moja kwa Watanzania eti hadi 2018 ndo watafikiria kulipa mrabaha na kodi! 2013 walipata mother of all Pink Diamond yenye thamani sawa na Madeni yote ya Taifa! Almasi hiyo imepelekwa kwa Malkia!!! Grrrr
Kumetokea tukio la aina yake katika mgodi wa madini ya almasi wa Mwadui
uliopo katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Pc Idd Makame(25) amejeruhiwa vibaya mdomoni kwa kung'olewa meno sita baada ya kupigwa jiwe kwa kutumia kombeo (kwa lugha ya kisukuma Nh'ago) na watu wanaodaiwa kuwa ni wachimbaji haramu wa madini katika mgodi wa Mwadui wakati akitimiza wajibu wake wa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao Tukio hilo limetokea Novemba 21,2014saa mb ili na robo usiku katika eneo la Tanex katika mgodi huo wakati askari huyo akiwa na askari wenzake wakiongeza nguvu baada ya askari wa kampuni ya ulinzi ya Zenneth inayolinda mgodi wa Mwadui kushindwa kuwadhibiti wachimbaji wadogo wa madini maarufu "Wabeshi" waliotaka kuingia kwa nguvu mgodini wakiwa na silaha za jadi. Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa kampuni ya ulinzi ya Zenneth Security Services Limited inayolinda mgodi huo ilipata taarifa kuwa kuna wachimbaji haramu maarufu kwa jina la Wabeshi walitaka kuvamia mgodi wakiwa na silaha za jadi ikiwemo mishale,mikuki,virungu,makombeo,mapanga
na fimbo. Kufuatia hali hiyo askari hao wa Zenneth walifika eneo la tukio kuwadhibiti Wabeshi hao lakini ghafla walianza kushambuliwa kwa silaha za jadi yakiwemo marungu,mishale,mikuki
na makombeo. Baada ya kuona wanazidiwa nguvu,askari wa Zenneth walilazimika kuomba msaada wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) cha jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga. Baada ya askari wa FFU kufika eneo la tukio nao walianza kushambuliwa na Wabeshi hao ,ndipo PC Idd akapigwa jiwe mdomoni kwa kutumia kombeo na kung'oka meno sita mdomoni na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu. Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Zenneth Security Services Limited Elisha Ndulu amethibitisha uwepo wa tukio hilo. Naye mganga mfawidhi wa hospitali ya
mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum amesema Pc Idd alipigwa na kitu chenye ubapa mdomoni na kusababisha meno sita kung'oka na anaendelea kupatiwa matibabu,hali yake inaendelea vizuri. Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari wanawashikilia watu wanne kwa mahojiano zaidi na wanaendelea kufanya uchunguzi il
 
Kombeo ni silaha aliyotumia mfalme Daudi kumpiga Goliat! kingereza inaitwa flintstone! huyo ashkuru imetoa meno inatoaga ubongo
 
Ang'olewe tu mapolisi wanachosha na kukera wanapotumika kuumiza RAIA na akome kiherehere chake kapatikana
 
Hii taarifa nimeipenda sana, ila huyu mrusha kombeo ningemjua ningempa mbinu ya ziada ili next time anaporusha apige na kung'oa meno yote angalau haya mapoliccm yatumie akili.
Kilichoniudhi ni kuwaona watu wenye ardhi yao wanaitwa wachimbaji haramu.
Mungu atalipa tu na meno yatazidi kuwatoka, na mengine huko Dodoma hakukaliki kabisaaa
 
Wasukuma mmenipa raha sana! Kama kuna chance ya kulifadhiri kindi la Wabeshi mm ntachangia ili mlijenge Taifa hili.
 
Back
Top Bottom