Polisi amwaga unga kwa kutishia kuua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi amwaga unga kwa kutishia kuua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jan 31, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,058
  Likes Received: 6,835
  Trophy Points: 280
  JESHI la polisi Mkoa wa Rukwa limewafukuza kazi askari wake wawili kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya mmoja kutishia kumuua mwenzake kwa kumpiga risasi wakati wakiwa lindoni.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Isuto Matage alisema jana kuwa jeshi hilo limechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa askari huyo alikuwa amekwenda kinyume na sheria za kijeshi na alistahili kufukuzwa kazi.

  Alimtaja askari huyo kuwa ni F 6399 PC Halfa Iddy Munuka ambaye amefukuzwa kazi tangu Januari 15 mwaka huu kwa kosa la kumtishia kumpiga risasi askari mwenzake F2458 PC Yona wakiwa lindoni katika benki ya NMB tawi la Mpanda Septemba 7 mwaka 2007.

  Pia kosa la pili lililochangia kumfukuzisha kazi ni kitendo chake cha kutelekeza silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30 pembeni mwa chumba cha mahabusu.

  Kamanda huyo aliongeza kuwa baada ya askari huyo kutelekeza silaha hiyo iliokotwa na afisa mkaguzi na yeye alikamatwa alfajiri yake na kushtakiwa Febuari 14 mwaka jana katika mahakama za kijeshi na baada ya uchunguzi kufanyika na kubainika ilitolewa azimio la kufukuzwa kazi.

  Mantage alisema kuwa pia jeshi hilo limemfukuza kazi Askari Polisi F.5767 PC Michael Mangi wa kituo cha Namanyere wilayani Nkasi kwa tuhuma za kuiba fedha benki kwa njia ya 'ATM CARD' kwenye akaunti ya mwananchi mmoja mkazi wa mjini humo.

  Kamanda huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 16 mwaka huu, ambapo askari huyo anadaiwa kuiba fedha za Kasesaunga Joseph (50) mkazi wa kitongoji cha Ipanda mjini Namanyere ambaye aliibiwa fedha hizo kiasi cha shilingi 1,063,000 kwa njia ya huduma ya kuhamisha fedha ya benki hiyo iitwayo NMB ATM CARD.

  Kamanda huyo alisema kuwa polisi huyo alipata namba za siri za mwananchi huyo baada ya kumkuta lindo PC Mangi kwenye benki hiyo na kumuomba amfundishe namna ya kutumia kadi ya ATM.

  Kamanda Mantage alisema kuwa mtuhumiwa akihojiwa baada ya kutiwa nguvuni na polisi alikiri kosa hilo na jeshi la polisi kuchukua uamuzi wa kumfukuza kazi.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...