Polisi aliyemwua Mwangosi avuliwa uaskari kabla kufikishwa mahakama ya kiraia

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
Mbaya wa Mwangosi avuliwa uaskari

ASKARI polisi aliyefyatu bomu lililomlipua na kumuua kinyama mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, David Mwangosi (40), amefikishwa katika mahakama ya kijeshi na kuvuliwa uaskari.

Vile vile, askari huyo mwenye cheo cha PC anatarajiwa kufikishwa katika mahakama za kiraia kujibu mashitaka yanayomkabili.

Habari kutoka ndani ya jeshi hilo mkoani Iringa zilimtaja askari huyo kuwa ni PC Pacificus Cleophace Simon (23), mwenye namba G2372. Ni askari wa FFU Iringa, na hajafikisha miaka mitatu kazini.
Inaelezwa kuwa askari huyo ambaye anadaiwa kukiri kuua bila kukusudia, ameshakula kiapo cha ungamo mbele ya mlinzi wa amani.

Kufikishwa katika mahakama ya kijeshi kwa askari huyo, kumekuja baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa awali ambao umebaini kuwa bomu alilofyatua ndilo lililosababisha kifo cha Mwangosi.

Kwa mujibu wa habari hizo, askari huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi mkoani Iringa na anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya kiraia wakati wowote.

Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa askari huyo huenda akapanda kizimbani baada ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema na Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, kukamilisha kazi zao ndani ya siku 30.
Hadi tunakwenda mitamboni, Kamanda wa

Polisi mkoani Iringa, Michael Kamhanda na IGP Mwema hawakupatikana kuthibitisha taarifa hizo.

Picha zilizopigwa kwenye tukio la mauaji ya Mwangosi, zilionyesha askari wakiwa wamemzingira na kumpiga, baadhi yao wakiwa na virungu, na wengine bastola. Mmoja miongoni mwao, ameshikilia bunduki na kuielekeza tumboni.
Vile vile, baadhi ya askari wamemtaja mwenzao aliyemlipua Mwangosi, wakataja na mahali anakoishi mjini Iringa.

Askari waliokuwepo siku ya tukio, walilieleza gazeti hili kwa sharti la kutotaja majina yao kwamba aliyemlipua Mwangosi na kumuua papo hapo yuko chini ya ulinzi tangu siku ya tukio akiwa na askari wengine walioonekana wakimpiga mwandishi huyo.

Mwangosi aliuawa Jumapili iliyopita katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa wakati akiripoti habari za ufunguzi wa tawi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), huku polisi wakiwazuia kufanya kazi yao ya kisiasa.
Bomu lililomlipua Mwangosi lilimjeruhi askari polisi aliyetambulika kwa jina la Aceli Mwampamba, aliyekuwa amekumbatiwa na mwandishi huyo wakati akishambuliwa na kundi la polis
i.
 
JINA LA MTUHUMIWA HUYU LINATOSHA KUWA NI FORGERY TUPU NA STUPID NAME Pacificus Cleophace Simon, HIVI HAKUNA ALIYESOMA NAYE AKATOA DETAILS ZAKE? 23YRS OLD, SAY BORN -1989, STD VII -2002, FORM IV-2006, MAFUNZO YA POLISI YAWEZEKANA 2008,AJIRA 2009- TODATE 3YRS, FUNGUKENI MTUPASHE MNAOANGUKIA MIAKA HIYO KAMA NI MWENZENU LETENI HABARI ZAKE HAPA JF NAJUA WATAKUWEMO WANAOMFAHAMU HATA KAMA ALITOKA SHULE ZA KATA ZENYE DIV IV TUPU
 
Ninachochangaa inasemekana amefikishwa mahakamani huku amefunikwa sura, sijapata kuona tukio kama hili mahakama kuruhusu mshtakiwa kufikishwa bila kuonekana sura, labda wanaotupa habari hizi hawako makini.
 
Hv hakuna hata mmoja alikuwa naye class moja?

Na enzi hizo shule za kata ilikuwa haijaenea kama leo!
 
Hv hakuna hata mmoja alikuwa naye class moja?

Na enzi hizo shule za kata ilikuwa haijaenea kama leo!

Utajuaje ni mbinu zile zile za Ulimboka kumtoa kichaa aliyeingia kanisa la walokole na kumsingizia ndiye aliyejeruhi Dr na kumtupa Mabwepande?
 
Huu ni uongo tena uliokomaa, hilo jina uki-google halipo katika shule yoyote ile ya sekondari.Ina maana jamaa ni darasa la saba?Hii filamu ni kama mkenya wa Kova.Kwa kifupi tumedanganywa kabisaaaaa!
 
Wenye ukweli watupashe, jamali hata ndani ya Polisi mtupe ukweli wa muuaji huyo wa Mwangosi.
 
sasa ukimshajua muuaji au ukigundua kuwa siyo yeye utafanyaje. jf kwa kelele zisizo na matokeo . YAKOWAPI YA ULIMBOKA tafuteni njia nyingine na sio kupiga kelele
 
sasa ukimshajua muuaji au ukigundua kuwa siyo yeye utafanyaje. jf kwa kelele zisizo na matokeo . YAKOWAPI YA ULIMBOKA tafuteni njia nyingine na sio kupiga kelele
attachment.php
 
JINA LA MTUHUMIWA HUYU LINATOSHA KUWA NI FORGERY TUPU NA STUPID NAME Pacificus Cleophace Simon, HIVI HAKUNA ALIYESOMA NAYE AKATOA DETAILS ZAKE? 23YRS OLD, SAY BORN -1989, STD VII -2002, FORM IV-2006, MAFUNZO YA POLISI YAWEZEKANA 2008,AJIRA 2009- TODATE 3YRS, FUNGUKENI MTUPASHE MNAOANGUKIA MIAKA HIYO KAMA NI MWENZENU LETENI HABARI ZAKE HAPA JF NAJUA WATAKUWEMO WANAOMFAHAMU HATA KAMA ALITOKA SHULE ZA KATA ZENYE DIV IV TUPU

Kwani Huyu jamaa hana hata jina la ukoo? Ni mtanzania gani ambao ana majina matatu halafu yote ni ya kizungu? Anyways zote ni movie tuu. Kwa anaefuatiliia, mnakumbuka reaction ya polisi kuhusu sababu za kifo cha marehemu they are very contradictory.
 
hili ni la kutengenezwa hakuna lolote, kwani hakuna mahakama za majeshi humu nchini kwetu?
 
yule jamaa si polisi,muuaji 2namjua na picha yake 2nayo wala hakua na mwili wa yule feki muuaji.IGP KWELI KWA HILI MMECHEMKA
 
sasa ukimshajua muuaji au ukigundua kuwa siyo yeye utafanyaje. jf kwa kelele zisizo na matokeo . YAKOWAPI YA ULIMBOKA tafuteni njia nyingine na sio kupiga kelele
Sasa wewe ulifuata nini hapa JF kama ewanakukera si uende huko FC
 
Kuna vi secondary vimeingia humu yaani reasoning zao hadi inakela. Sasa wewe unataka mtuhumiwa au unajadili secondary alisoma
 
Back
Top Bottom