Polisi akataa hongo ya Sh680,000

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,720
155,325
JESHI la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watano, huku wanne wakidaiwa kutoa rushwa ya Sh680,000 baada ya kukamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya mirungi inayodaiwa kuingizwa kutoka nchi jirani.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Simon Sirro alisema jana kwamba watuhumiwa hao walikamatwa katika matukio mawili tofauti wilayani Magu jijini Mwanza wakiwa na kilo 520 za majani hayo yaliyopigwa marufuku nchini.
Kamanda Sirro alisema baada ya kukamatwa, watuhumiwa hao walimshawishi Koplo Benson Karokola kuchukua rushwa ya Sh680,000 ili waondoke na kidhibiti chao, lakini askari huyo alikataa.

Alisema katika tukio la kwanza Oktoba 8 mwaka huu saa 8:45 mchana, Koplo Kalokola alimkamata mtu mmoja (jina tunahifadhi) akiwa na kilo 20 za mirungi ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye dumu la mafuta ya kula la lita 20 eneo la Nata jijini Mwanza.
“Baada ya kumkamata Bakari, alijitokeza mtu mwingine aliyetambulika kwa jina la Juma Poyo ambaye alimwomba askari huyo kumuachia Bakari na kumtaka apokea Sh280,000 kwa madai kwamba wao ni wauzaji wazoefu hivyo wakipelekwa polisi wataaibika,” alieleza Kamanda Sirro na kuongeza kuwa mtoa rushwa huyo alitiwa mbaroni.

Alidai kuwa watuhumiwa wengine waliokamatwa Oktoba 9 mwaka huu kwa nyakati tofauti kati ya saa 3:00 hadi saa 4:00 asubuhi wilayani Magu wakiwa na kilo 500 za mirungi walizokuwa wakiziingiza nchini kutoka nchi jirani.
Alifafanua kuwa mwanamke huyo alishushwa kwenye basi la kampuni ya Zacharia na mwingine kwenye basi la kampuni ya Batco Ltd.

Baada ya kukamatwa, waliwaweka kwenye gari moja na kupelekwa jijini Mwanza lakini kabla ya kufika kituo cha polisi, mgtu mmoja (jina tunalo) alidandia gari na kumshawishi askari huyo kupokea Sh400,000 amwachie mtuhumiwa.
“Naye pia aliwekwa chini ya ulinzi na askari huyo na wote kufikishwa kituoni pamoja na fedha hizo. Hivyo tunawashikia wanne kwa tuhuma za kukamtwa na mirungi na kutaka kutoa rushwa huku mwingine kwa tuhuma za kukutwa na mirungi,” alieleza Sirro.
Kamanda Sirro alimpongeza Koplo Kalokola akimuelezea kuwa ni mfano wa kuigwa na kuwa jeshi hilo linaangalia utaratibu wa kumzawadia kutokana na uaminifu wake.

SOURCE:- M WANANCHI
 
Serikali ya CCM ni nadra sana kuzawadia waadilifu..... Koplo wa-watu ataendelea kula jua lake tu..... In CCM government there is no adequate system of appraising best performers in public service.... Ndio maana wafanyakazi wa umma wamekubuhu kwa utendaji mbovu, rushwa, vimtandao vya wizi wa mali za umma, job offering/appraisal based on nepotism/friendship rather than expertism..... Yaaaaani ni balaa tu..... Tushirikiane tuing'oe CCM madarakani hapo 31/10/2010..... Kura yako ndio mkombozi wako...Itumie!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom