Polisi Afrika Kusini yaua Waandamanaji

Mzalendo Mkuu

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
735
191
Habari kutoka BBC zinasema polisi nchini Afrika Kusini imefyatulia risasi wachimba madini waliokuwa wanaandamana kudai malipo ya mshahara zaidi. Watu 18 wamekufa.Afrika ileile na mambo yaleyale.
 
Je Ingekuwa Kipindi cha Ubaguzi si Tungeombwa Tuandamane wote Watanzania ili kulaani kitendo cha serekali kandamizi ya kikoloni na kibaguzi?
Sasa kwa sasa yupo Mkoloni Mweusi nani Bora? Duh Hatari!! Mauaji sasa ya weusi yanafanywa na mkolono Mweusi, nani wa kumfunga paka kengele?
 
Dah! Yani hata siamini jamaa wanaua wenzao utafikiri wanaua swala porini.Nguvu iliyotumika ni kubwa sana
 
One thing I know about South Africans...Ni arrogant na wajuaji sana. Sitashangaa wakianza kuchalazana bakora wenyewe kwa wenyewe.
 
Habari kutoka BBC zinasema polisi nchini Afrika Kusini imefyatulia risasi wachimba madini waliokuwa wanaandamana kudai malipo ya mshahara zaidi. Watu 18 wamekufa.Afrika ileile na mambo yaleyale.

waliokufa wamefika 30. serikali ya ccm inavyowaachia waandamanaji UCHWARA WA BONGO wanadhani ni dhaifu kumbe ni huruma na utu wa mheshimiwa rais. anao uwezo wa kuchukua hatua kama ile
 
What Type of these Mass Killing!! But Why? Just Killing!! Oh their Must be something Wrong!!
 
Ndio muone kwamba tumedanganywa sana mara mkoloni alikuwa mbaya, mara mkoloni alituuza utumwa mara ubaguzi wa rangi.... na ni wakati sasa wa kuungalia ukweli kwamba mzungu alikuwa hana jinsi bali kutufanya alivyotufanya na historia inakwenda inajirudia na ukweli unazidi kuonekana, miaka ya 1960 Dunia nzima ilaindamana kupinga sharpeville massacre miaka 50 baadae ANC wanaua waafrika kwa risasi!

Bado kitu kimoja kutokea kukamilisha mzunguko (cycle) tutaanza kuuzana tena wenyewe Ulaya au Uchina na baada ya hapo sasa ushahidi utakamilika kwamba hata utumwa sisi ndio tulikamata watu wetu na kuwapeleka kuwauza kwa waarabu au wazungu!

Nyerere sipati huko aliko!
 
jamani hawa polisi wanaua binadamu wenzao kama kuku Polisi wapunguziwe mipaka ya kutumia siraha za MOTo
 
Nimefuatilia hii story. Kumbe hawa jamaa walikuwa na silaha kama mapanga, visu na bastola, na jana yake waliwacharanga askari wawili kwa mapanga, na kuua wenzao 10 ambao inaonyesha walipingana hoja. Polisi walifyatua risasi wakati jamaa wanawafuata na mapanga ili wawashughulikie. Picha zinaonyesha jamaa wakiwafuata polisi mbio na mapanga, basi polisi wakikumbuka wenzao walivyouwawa wakaamua kuziachia. Angalia picha za waandamanaji wa tukio hili nilizoweka.

Taarifa zinasema pia huko bondeni polisi kuuwawa ni jambo dogo sana, na kwamba hakuna maandamano (protests) ambayo huwa ni ya amani hata siku moja.

Hali hii ni tofauti sana na polisi wa Tanzania ambao huua na kupiga waandamanaji wa amani wasio na silaha!
View attachment Mauaji Bondeni.pdf
 
Kuwa police bondeni ni zaidi ya ajira ni hatari.joh'berg huokotwa askari 9 wameuawa kila siku asubuhi .unapoapishwa kuwa police unakabidhiwa bastola papo hapo kwa usalama wako na raia .ni vema serikali ya zuma ikapunguza gape ya maisha kati ya tajiri na maskin ni kubwa mno pale
 
Ninaposoma habari zaidi juu ya polisi wa bondeni naona kama askari wa Marekani aliyeko Iraq au Afghanstan yuko salama zaidi ya polisi wa Afrika kusini pale Johannesburg
 
those policemen were just trigger happy walitaka kuwaua hao watu mara let me ask a simple question polisi akifyatua risasi angani how many people will not run watu wangapi wata baki hapo all the police had to do was shoot in the air to disperse the crowd simple psychology
 
Mkuu Mkenya, niliwahi kuishi bondeni nikiwa chuo. Polisi wa bondeni wanatembea na bastola wakati wote. Kuna polisi wawili walicharangwa na mapanga jana yake pamoja na kuwa na bastola na kutishia, na bastola zikaporwa! Wakati wa mauaji ya wasio Wasouth polisi walikuwa wanafyatua risasi juu hakuna anaejali hadi wanaua mtu.

Kuna wakati security guards walifanya mgomo, wakawa wakimshika mwenzao anaekwenda kazini, wanamtupa kwenye matairi ya treni inayotembea. Wa-south bwana ni bangi sana, wasikie tu. Nadhani kwa Afrika wa-South kwa ukatili wanashikilia namba one. Uliona walivyochoma watu moto watu wa Msumbji, Tanzania, Zimbabwe, Kongo kwa kuwa eti wanawachukulia kazi zao?
 
Back
Top Bottom