R Mbuna
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 2,295
- 5,458
Habari za wakati huu wana jukwaa.
Hii habari imenisikitisha sana na imenikera sana kwa jinsi polisi wanavyolazimisha kuwapa watu makosa ili hali ni raia mwema tu.
Niende kwenye mkasa ambao umepelekea kuleta hili bandiko humu jukwaani, kuna kijana anauza duka huko maeneo ya Mbagala sasa juzi siku ya Jumapili mida ya saa mbili usiku alikuwa ameenda kupunguza nywele baada ya kuona zimekuwa ndefu kichwani kwake.
Kabla hajafika eneo la saluni alikutana na polisi njiani wakamwambia kwa nini anazurura usiku, yeye akajieleza kuwa anaenda kupunguza nywele na hakai mbali na pale walipomkuta polisi. Hivyo polisi wale ambao walikuwa na gari yao ya doria wakamwambia leo utaenda kulala ndani kesho utaenda mahakamani kwa sababu ya uzururaji.
Bahati nzuri kuna watu walimuona wakati anakamatwa na kila mtu alishangaa jinsi ya ukamataji ule kwa sababu ni kijana ambaye ni mtaratibu sana na wala hana kawaida ya kukaa vijiweni yeye kutwa anashinda kwenye duka lake tu.
Kijana mwenyewe masikini ya Mungu ni mlokole hata hiyo sigara katika maisha yake hajawahi kuvuta analia mpaka anatia huruma. Ameniambia kaka kama wamenifungulia hiyo kesi waambie wakanipime mkojo ili wajiridhishe kama katika maisha yangu nimeshawahi kutumia kilevi cha aina yoyote.
Wanalazimisha wapewe hongo hawa jamaa sio watu wazuri ndio maana wananchi hawatoi ushirikiano kwa hii taasisi ya serikali kwa sababu wakati mwingine huwa wananyanyasa raia bila sababu za msingi.
Tunaomba waziri mwenye dhamana aangalie sana hii idara yake ya polisi hii sio poa kabisa.