KIPIGO alichokipata ‘First Lady' wa Chadema, Josephine Mushumbusi (pichani) katika maandamano ya chama hicho kushinikiza kurudiwa upya kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, kimetafsiriwa kama ni mkosi wa tatu uliomkumba mwanaharakati huyo tangu aingie katika siasa.
Wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa wanasema kuwa, Josephine anayetambulishwa kama mchumba au mke wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbroad Peter Slaa pamoja na ujasiri wake, bado ameendelea kukutwa na mikosi.
Wakitaja baadhi ya matukio, wadau hao wa siasa walisema kuwa, mkosi wa kwanza wa ni kitendo cha mumewe wa awali, Aminieli Mahimbo kumfikisha mahakamani Dk. Slaa baada ya kumkacha kwenye ndoa yeye na kuibukia kwa mwanasiasa huyo.
Mkosi wa pili unatajwa kuwa ni kitendo cha Dk. Slaa kuvunjika mkono katika ajali ya kuanguka bafuni wakati akioga hasa ikizingatiwa kuwa, alikuwa katika harakati za kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Agosti mwaka jana.
Kumbukumbu zinaonesha kwambaJosephine anakuwa ni ‘First Lady' wa kwanza kupata kipigo kutoka kwa jeshi la polisi kati ya wote waliowahi kujihusisha na siasa za Tanzania kwa migongo ya waume zao waliowania urais.
Hata hivyo, mwanamke huyo ameonekana ni jasiri na mkomavu kisiasa huku akiaminiwa kuwa, uvumilivu wake umemfikisha kwenye majukumu aliyonayo sasa.
Januari 5 mwaka huu, vurugu kubwa ilitokea jijini Arusha na kusababisha viongozi kadhaa wa Chadema, akiwemo Mwenyekita Taifa, Freeman Mboye na Katibu Mkuu, Dk. Slaa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kukaidi amri ya kutoandamana kushinikiza kurudiwa kwa uchaguzi wa Meya.
Katika vurugu hizo watu wawili wanadaiwa kupoteza maisha na sita kujeruhiwa.
Tags:
UCHAGUZI,
risasi11
Share Twitter Facebook