PolePole: Lowassa na Membe Tupa Nje Mapema Tu.

PolePole: Lowassa na Membe Tupa Nje Mapema Tu.

Eddy wewe nani ndani ccm majambazi? Achana Na Polepole maji marefu kwako hajakurupuka wewe unaganga njaa kwa huyo fisadi Na mwizi Mkuu hata hayati baba wa taifa alitusihi tumwogope mkimbilia ikulu

Ukimuona mtu anapakimbilia ikulu kwa kutoa pesa muogopeni kama ukoma " mwl. Nyerere"
 
Tatizo Lowassa ameshika kila mahali....

everybody knows, hamuwezi kuzuia...............
 
Huyu dogo kweli ni mpuuzi,LOWASA hawezi kukubali jina lake kuondolewa make alishahaidiwa kuwa hii ni zamu yake,lowasa ndiye rais wengne wasindikizaji tu!
 
Eddy wewe nani ndani ccm majambazi? Achana Na Polepole maji marefu kwako hajakurupuka wewe unaganga njaa kwa huyo fisadi Na mwizi Mkuu hata hayati baba wa taifa alitusihi tumwogope mkimbilia ikulu

watanzania wamechoka na umasikini na ubabaishaji, wanataka mabadiliko wanataka maendeleo wanataka kukimbia mchakamchaka, hawataki tena porojo na longolongo, hatuchagui mtu lofa hatutaki wapiga ramli wanasema watatutajirisha wakati wao hawana kitu, hatutaki mtu wa kuanza kufungua ngo ikulu na kutembeza bakuli.

safari hii hatufanyi majaribio eti nipeni miaka mitano muone kwendazako, tunataka mtu mwenye uwezo wa kuyasimamia anayoyazungumza, watu wa kushikwa pua wanaobebwa kwa mbereko hawana nafasi tena. lowasa kanyaga twende.

Mwambieni polepole akamwambie aliyemtuma hakatwi wala hakeketwi mtu mwaka huu
 
Eddy wewe nani ndani ccm majambazi? Achana Na Polepole maji marefu kwako hajakurupuka wewe unaganga njaa kwa huyo fisadi Na mwizi Mkuu hata hayati baba wa taifa alitusihi tumwogope mkimbilia ikulu

achana na mimi, sigangi njaa kama wewe, kama polepole anawakatia mumpe promo mumeula wa chuya, kama kweli ni mwanccm na vigezo anavyo akachukue form nae agombee sio kukaa kukebehi watu. ccm inaendeshwa kidemokrasia kila mtu anahaki ya kugombea na kujinadi. acheni hizo.
 
Kijana Mashuhuri ,Mmoja wa Wajumbe kwenye Tume ya katiba Mpya Yaani Tume ya Warioba ,amejimbambanua na kusema yeye ni mwanachama wa ccm, pia anakitakia Chama chake afya Njema ,Amesema kwamba , Kutokana na Makundi Makubwa mawili ndani ya CCM, yaani Team Membe na Team Lowassa. "Haya makundi yatakimaliza Chama" Watu hawa wawili hawaruhusiwi kufika kwenye Kamati kuu yaani CC. kinachotakiwa Majina yao yaondolewe Mapema Sana wakati wa kumtafuta Mgombea Uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi.

wewe Mwana CCM na wewe mwananchi unaonaje na Ushauri wa Ndugu PolePole? Leta Maoni yako siyo Matusi.

Wakatwe kabla ya kufika kwenye CC!! watakatiwa kwenye chombo gani? nijuavyo mimi watachujwa watabakia wagombea 5 then waende mkutano mkuu kwa kupigiwa kura abakie mmoja. ok wanaokumbuka vizuri wataweka sawa.

Hoja yake nadhani pia hayuko sahihi, chaguzi bila makundi yanayounga mkono yatakosekana vipi! Hata Rais Kikwete 1995 alivyoshindwa na mzee Mkapa alitangaza kuvunja kundi lake na kuwa pamoja na Mkapa, kiongozi mmoja wa CCm alisema Kikwete akishinda nahama nchi japo mpaka sasa yupo. hiyo yote ni ishara kwamba makundi hayapingiki na sio dhambi hata kidogo iwapo nia ni kuunga mkono tu na atakayeshinda kuungana naye.
 
Polepole hajawahi kuchaguliwa hata kiranja wa bweni, atachambuaje wagombea? Hiyo kadi ya ccm anayomiliki atuambie ni namba ngapi ya tawi gani? Haka kajamaa kashenzi tu.

Kwahiyo hutaki mtu mwingine atowe wazo lake isipokuwa wewe?wewe na katiba ya nchi nani yupo juu?hivi mbona mnashindwa kudhibiti mihemuko yenu?
 
Back
Top Bottom