Polepole: Kuna uwezekano wa kufungua dirisha la usajili endapo Edward Lowassa atataka kujiunga

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
4,512
6,856
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amezungumzia uwezekano wa kufungua dirisha la usajili la chama hicho, endapo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa atataka kujiunga.

Polepole ameiambia Times Fm wiki hii kuwa mchakato wa kumpokea mtu aliyekuwa mwanachama wa chama hicho hufanywa kwa mujibu wa Katiba ya chama na kwamba utataribu huo utazingatiwa.

Alisema kwa kawaida ni lazima watakaa vikao kadhaa kumjadili ili kufahamu kama ujio wake una manufaa yoyote kwenye chama.
“Mwanachama wa CCM aliyehama na kujiunga na chama kingine cha siasa, akitaka kujiunga tena na CCM atapeleka maombi yake kwenye tawi lake analoishi. Atajadiliwa na vikao vinavyohusika, na uamuzi wa mwisho wa kukubaliwa au kukataliwa utafanywa na Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ngazi ya Wilaya,” Polepole alisoma ibara ya 13 (5) ya Katiba ya chama hicho.


Hata hivyo, Polepole alieleza kuwa kutokana na uhalisia, ni rahisi kutabiri kama mtu anayetaka kurejea ndani ya chama hicho atakubaliwa au la.
“Kwa bahati nzuri sisi huwa tuko very predictable (tunabashirika). Kwahiyo kuna watu najua hata wakiomba kujiunga na CCM tutawakataa,” aliongeza

Miezi kadhaa iliyopita, Lowassa akiwa kwenye mikutano ya kampeni kwenye chaguzi ndogo, alisema kuwa Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliwahi kumtaka arejee ndani ya chama hicho lakini alimjibu, “uamuzi wangu haukuwa wa kubahatisha.

Lowassa alihama CCM na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo mwaka 2015, ambapo alipewa nafasi ya kugombea urais akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
 
Sasa wanamtaka wa nini? Magufuli mimi ndiyo maana simpendi hata kidogo!
 
Wananchi tukuamue tusijidhalilishe kwenda kupiga kura itakuaje?

Lakini kwa mambo yalivyo, usishangae tume ya uchaguzi kutangaza mshindi tena kwa kura za kishindo.
 
Kama uatamsikia katika mahojiano haya, utamuelewa nini anamaanisha nanini chama chake kinasimamia
 
Hovyo kabisa,nilidhani kuna uwezekano wa kutibu vichaa sugu ili tuweze kusonga haraka.
 
tume haiwezi kuwa huru kiasi cha kila mgombea kutangazwa mshindi
Mambo mengine ni kujiaibisha. Umeleta uzi watu wachangie. Unaanza mwenyewe kuharibu uchangiaji. Unajitoa mwenyewe ufahamu kiasi hiki? Tume huru hutangaza kura za kila mgombea alizopata ndani ya sanduku la kura. Kamwe haitangazi kura nje ya hapo. Haiongezi wala haipunguzi kura halali alizopata mgombea kwa sababu yoyote ile. Tume huru haifungamani na mgombea yeyote kwa lolote liwalo. Ndio maana halisi ya kuwa huru. Inaheshimu kila kura ya mpiga kura. Inawaheshimu wapiga kura wote. Inaheshimu matakwa yao waliyoonyesha kwenye sanduku la kura. Kupata mshindi lazima kuwepo ushindani. Kila ushindani una kanuni, masharti na vigezo. Tume huru inahakikisha washindani wanapewa mazingira sahihi na stahiki bila ubaguzi. Mmoja atakuwa mshindi. Tume huru haitangazi yeyote bali mshindi tu. Tume huru inatangaza mshindi kwa mujibu wa kanuni na sheria husika kwa haki na uwazi. Binti yako wa chekechea angesoma andiko lako angeona aibu kuwa na baba wa hovyo kiasi hicho! Baba anaandika kwa geat thinkers kuwa tume huru ni huru ikitangaza kila mgombea mshindi! Dhana ya ushindani inapotea. Ushindani wa haki na uwazi katikai kila hatua hutoa mshindi halali na kweli. Mchato huo usimamiwa na tume huru. Aliyeshindwa anakubali na kumpongeza mshindi. Ushindani huru na haki unawezekana chini ya tume huru tu. Sio tume huru jina bali tume huru halisi!
 
Back
Top Bottom