Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 299,016
- 751,663
Pamoja na kwamba tunaambiwa kwamba binadamu wote ni sawa ..hili ni kwa sehemu tu ya yale mahitaji ya lazima... Kiuhalisia tunatofautiana pakubwa sana!
Teja kamwe hawezi kufanana na konda wala konda hawezi kufanana na dereva....tuna rankings katika maisha
Cheo cha katibu mwenezi wa CCM ni tofauti kabisa na cha katibu mwenezi wa ACT japo viko kwenye rank moja...Hawa wawili wakiongea kitu kinachofanana impact itakuwa tofauti kabisa
Kwenye sakata la mchanga wa dhahabu bandarini katibu huyu mwenezi wa CCM anadai kuna mtu/watu walitaka kumhonga mkuu wa nchi dollar million moja karibia na nusu ambayo thamani yake kwa pesa yetu ni kama BILIONI MIA TATU
Haya si madai madogo wala mepesi
Huu ni zaidi ya uhujumu uchumi, huu ni uhaini. Madai ya uthubutu wa kutaka kumhonga mkuu wa nchi ni kashfa dharau na uchochezi mkubwa kabisa..... Kutaka kumhonga rais ni sawa na kutaka kuipeleka nchi mnadani...
Hili hapana kama taifa tuna heshima utu na hadhi yetu..kama kweli kuna mtu, watu ama taasisi alijaribu kufanya hivi na akakaliwa kimya tu na mamlaka husika, na bado tukaendelea kutumia kibubu dhoofu cha taifa kuunda tume kutafuta ukweli wa mchanga nachelea kusema kuna shida kubwa mahali
Nionavyo mimi Humphrey kakurupuka na kuropoka bila kujua kuwa maneno yake hayo yameidhalilisha pakubwa taasisi ya urais...kwamba inajaribiwa, tena si kwa kingine bali HONGO!!!!
Tufunike kombe mwanakharamu apite ....lakini basi hata kimyakimya tuambizane kwamba katibu mwenezi katia DOA kubwa la aibu nafasi yake chama chake, taasisi ya rais na nchi katika ujumla wake bila kujisahau yeye kama yeye na familia yake