Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikienea kuwa katika mabadiliko ya katiba ya chama hicho yaliyopitishwa mjini Dodoma hivi karibuni, kumeingizwa kipengele ambacho kinamfanya Rais Magufuli kupitishwa kutetea nafasi yake hiyo bila kupingwa.
Uvumi huo umekanushwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole Jumapili hii. Amewataka Watanzania kuzipuuza taarifa hizo akisema kwamba ni za upotoshaji kwakuwa katika mkutano huo wa dharura hapakuwa na ajenda kama hiyo wala mjadala wa utaratibu wa kumpata mgombea urais wa mwaka 2020.
“Hili jambo la kupinga ni uongo. Hakuna kikao chochote tulichojadili suala la kugombea kwa maana ya kuomba nafasi ya kupeperusha bendera mwaka 2020,” alisema.
Hata hivyo alisema kuwa suala hilo lipo kwenye utamaduni wa CCM wa siku nyingi kwamba Rais aliyepo anapitishwa kwa muhula unaofuata ingawa hakuna anayezuiwa kuchukua fomu ya kumpinga.
“Kila baada ya miaka mitano watu wanaruhusiwa kuchukua fomu. Hata mwaka 2010 walifanya hivyo. Lakini kwa aliyefanya kazi nzuri tutampa tena nafasi. Hatujaondoa haki hiyo ya kidemokrasia ndani ya chama.
Source: Bongo 5