Polepole amshukia Hashim Rungwe Sipunda kama mwewe, ashangaa wamejitoa wapi wakati hawakuwemo kwenye uchaguzi

Mwenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole amesema anamshangaa sana mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda kwa kudai chama chake kimejitoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Polepole amesema CHAUMMA hakikuwepo kwenye uchaguzi kwa sababu hakuna mwanachama hata mmoja wa chama hicho aliyechukua fomu za kugombea.

Kadhalika chama hicho hakikupata kura hata moja katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Pia CHAUMMA hawana ofisi Mikoani, Wilayani wala kwenye Kata sasa wanajitoa kutokea wapi?......ameuliza na kushangaa ndugu Polepole.

Chanzo: Channel ten tv

Maendeleo hayana vyama!

Maswali ni mengi , Wanaomsikiliza Slowslow sijui huwa hawana akili ya kumhoji maswali?
 
Saa huyu bushman anaogopa nini?

Haka kamjamaa kana ugonjwa wa UNYAFUZI au Kwarshakor iliyochangamana na mtindio wa ubongo! Msikilize anapoongea kauli na vitendo vyake vinaonesha kabsa Slowslow is not physically and mentally health…!!
 
Mwenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole amesema anamshangaa sana mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda kwa kudai chama chake kimejitoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Polepole amesema CHAUMMA hakikuwepo kwenye uchaguzi kwa sababu hakuna mwanachama hata mmoja wa chama hicho aliyechukua fomu za kugombea.

Kadhalika chama hicho hakikupata kura hata moja katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Pia CHAUMMA hawana ofisi Mikoani, Wilayani wala kwenye Kata sasa wanajitoa kutokea wapi?......ameuliza na kushangaa ndugu Polepole.

Chanzo: Channel ten tv

Maendeleo hayana vyama!
Amezungumzia vipi na wale waliojitangaza watashiriki uchaguzi wakati hata hawana mwenyekiti wa kijiji mmoja?
 
Mtaani kwetu ccm wiki ilopita wamefanya party ya kusubir kuapishwa maana wana miaka10 serikali ya mtaa inaongozwa na chadema
 
Polepole ameongea kama mvutabangi au mnywa gongo. Mbona hatukumsikia akitema shudu vilipotoa tamko la kushiriki uchaguzi vile tulivyoambiwa eti vyama 11?

Hivyo 11 ana uthibitisho vingeshirikije wakati havina mgombea hata mtaa mmoja?
 
Ahangaike na ccm yake inayojifia.yeye anatujua sisi wanachama wa Chaumma tuliojiandikisha?
 
Vile vyama 11 vilivyosema vitashiriki katka uchaguzi kwani wagombea wake wapo mikoa gani?
Dhana ya kushiriki ni kubwa sio lazima awe na wapiga kura hata kuwaombea wagombea wa vyama vingine kura ni kushiriki pia , polepole nimemshangaa aliposema kuwa qqq"vyama vya siasa vilivuruga mchakato mapema kwa kuwahamasisha wananchi wajiandikishe, hapo tu nikamuona ni hopeless kabisa ...
 
Nadhani hili NENO KUJITOA linaweza kuwa liko sawa kutumia ma vyama vya siasa kwa maana ya
1. Kutokidhi vigezo kuchaguliwa
Mf A. Kutokuwa na mgombea
B. Kutochukua fomu
C. Kujaza fomu kimakosa
D. Kutokuwa na wanachama
2. Kukiuka masharti ya uchaguzi.
3. Kutoridhika na Tume
Sasa vyama vingine ni kweli havimo kwenye uchaguzi SM na kuwa automatically vimejitoa si kwa sababu Tume haiko vizuri bali havina mtu wa kugombea
Au walichaza fomu kimakosa na kuwa wa.ejitoa wenyewe
 
Ndio washajitoa sasa 😂😂😂

Kujitoa ni kujitoa tu ndugu pole pole
Wajitoe na ubunge basi,wanaokufa njaa ni hao waliojitoa,sasa kula kwa kutegemea mihuri au viwanja ndi bye bye,ningewaona wa maana Mbowe na Zitto wangeanza wao kujivua ubunge kwanza ili kuonyesha kweli kwamba wanapinga hayo wanayodai wameonewa,Zitto alikomalia korosho badala ya kutoa elimu kwa watu wake jinsi ya kujaza fomu za uchaguzi
 
Kwani tunaongelea wabunge au wagombea wa serikali za mitaa? Naona umeniacha njia panda kuwataja Mbowe na Zitto 🤷‍♂🤷‍♂🤔🤔🤔
 
Mwenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole amesema anamshangaa sana mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe Sipunda kwa kudai chama chake kimejitoa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Polepole amesema CHAUMMA hakikuwepo kwenye uchaguzi kwa sababu hakuna mwanachama hata mmoja wa chama hicho aliyechukua fomu za kugombea.

Kadhalika chama hicho hakikupata kura hata moja katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Pia CHAUMMA hawana ofisi Mikoani, Wilayani wala kwenye Kata sasa wanajitoa kutokea wapi?......ameuliza na kushangaa ndugu Polepole.

Chanzo: Channel ten tv

Maendeleo hayana vyama!
Vipi vile vyama viliyotangaza kushiriki, viliweka wagombea
 
Back
Top Bottom