Polepole ameishajivua gamba la Ukristo?

Hekima ,ujuzi
Kajifunze Tena maandiko
 
Yesu mwenyewe aliwaahidi watu wa enzi hizo kuwa atarudi lakini hao walioahidiwa hata mifupa yao ilishageuka vumbi tangu karne nyingi zilizopita lakini hajarudi.
Ila Polepole amewaweza sana, ndiyo mnakaa mkao wa kukata mawasiliano lakini anapiga binju anawapoteza maboya mkija kustuka 'keshawakojolea' bao.
 
BTW, unataka aseme muda sahihi muzime mtandao?
Atafikishaje ujumbe wa Mungu wa kutenda haki?
 
Yesu mwenyewe aliwaahidi watu wa enzi hizo kuwa atarudi lakini hao walioahidiwa hata mifupa yao ilishageuka vumbi tangu karne nyingi zilizopita lakini hajarudi.
Kwani Yesu alisema atarudi siku gani na saa ngapi?
 
Mleta mada ulisha wahi kuosoma kitabu cha Tobit ukakutana na kisa cha malaika aliye sema uwongo kwa ajili ya Jambo fulani .

Uwe tu mkweli wewe ni wale wale wana mtandao kama sio chawa wa ccm na mama yenu na mwanae.
 
Ukiniambia utaongea na mimi saa tatu, ukaongea saa nne, umeishaniambia uongo. Vinginevyo usiseme specific time. Au vipi
Basi kama hivyo hata wachezaji wa mpira wana dhambi.

Ukitaka kumpiga mtu chenga, unatishia kama unaenda kushoto lakini unaenda kulia hiyo nayo ni dhambi maana umemdanganya mpinzani wako.

Vipi kuhusu penati zinazopigwa, unaona kabisa kipa karuka kulia na mpira unaenda kushoto.
 
BTW, unataka aseme muda sahihi muzime mtandao?
Atafikishaje ujumbe wa Mungu wa kutenda haki?
"Msema kweli ni mpenzi wa Mungu" Hiyo methali imeishafutwa?
 
Kama ni hivyo, basi tusiwanyoshee vidole wote wanaosema uongo na kutuibia
Kuiba kwa manufaa yako kwa nia ovu haiwezi kupata kibali cha Mungu.
Kwani kuuwa siyo dhambi?
Mbona Samson na Gideon waliuwa adui zao?
Hawakuuwa kwa Nia ovu bali nia njema ya kukomboa watu wengi, yaani taifa lao.
Daudi alipouwa kwa manufaa yake alipata adhabu toka kwa Mungu. Aliuwa kwa kumpeleka Askari wake vitani akafe ili amuoe mke wake aliye mtamani baada ya kumuona akiwa mtupu anaoga.
 
Vipi pale alipo sema kizazi hiki hakita pita kabla ya kushuhudia ujio wake wa pili, alikua anasemea kizazi gani labda?
Ngoja waje wajuzi watatuambia. Ila nijuavyo mimi, Yesu hakusema siku wala saa ya kuja kwake. Huyo mheshimiwa huwa anataja siku na saa exactly
 
"Msema kweli ni mpenzi wa Mungu" Hiyo methali imeishafutwa?
Rudi kwenye Bible utaona Abraham baba wa Iman anadanganya watu kuwa Sarah ni dada yake na si mkewe. .. ukisoma hiyo part rud hapa kuna kitu ntakuelekeza kuhusu uongo ambao ni dhambi na ule ambao una thawab kwa mwenyez MUNGU. ....

Mfano: unapokwepa kumwambia mwanao kua alipatikana after sex na unamdanganya kuwa mlimwokota hospital
 
Teh teh. Mfano wako unaonesha watu wote wana dhambi. Kama ni hivyo, tusilaumiane. Mheshimiwa anawalaumu wenye dhambi wakati na yeye ana dhambi. Kama ni mechi basi 0-0
 
Nipe mifano ya Agano Jipya. Mambo mengi ya Agano la Kale Yesu alipokuja aliyafanyia ammendment. Wakati wa Agano la kale ilikuwa halali kuua, Yesu akaja akaibadilisha sheria hiyo. Hivisasa kuua ni dhambi. Vivyo hivyo kusema uongo ni dhambi katika Agano Jipya. Kasome habari za Anania na Safira. Walikufa immediately baada ya kusema uongo. Hapo vipi, mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…