Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,343
- 217,380
Ugomvi wa wakubwa wenu Pharmacy board dhidi ya Tfda sasa unawaumiza , makubaliano mliyoyafikia kati yenu na Tfda wakati ule wa yale mafunzo yenu ya ADDO yamepuuzwa ! Bila shaka mnayakumbuka , sasa mnanyang'anywa dawa zenu mlizonunua kwa mikopo ya FINCA kama vile mliiba ! msubiri kufungwa kwa madeni ! Pharmacy board haitambui hizo ADDO zenu japo vyeti vyenu vilitoka Wizara ya afya , maajabu ya mwaka ! Kuna tetesi kwamba kila kilichofanywa na tfda , pharmacy board itakipinga ! Harufu ya ARV feki inanukia , kwamba wenye ARV wana ushawishi mzito kwenye board na kwa vile tfda ndiyo ilifichua hayo mambo , tutaona ! ( tuchukulie kama tetesi ) bali mwenye kuyajua zaidi atufunue , hakuna haja ya matusi , nawasilisha.