Synod
JF-Expert Member
- Oct 10, 2016
- 4,091
- 4,028
Mkuu kwanza Poleni wakenya wote.Ama kwa kweli kazi ya ukomando ni wito, ni kazi ya watu wachache, inahitaji ukichaa fulani kuifanya, maana haingii akilini kwamba unakwenda kupambana na mazombi yaliyokuja kufa, yapo tayari kujilipua kwa misingi ya kidini na hayajaja yakiwa na nia ya kupona wala kutoka salama. Komando wa nchi yoyote anastahili pongezi popote alipo.
Lakini nikukumbushe kuwa kazi ya jeshi linapokuja suala la kifo hakuna tofauti na hao magaidi wa kujitoa muhanga. Tofauti ni kuwa gaidi anajitoa kufa kwa maslahi binafsi wakati mwanajeshi anajitoa hata kufa kwa maslahi ya taifa.
Hawa wanajeshi ni wazalendo wa kwanza.