Poleni waathirika, shukrani na hongera kwa makomando kwa kukamilisha shughuli

Toyota escudo

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
3,346
2,000
Ama kwa kweli kazi ya ukomando ni wito, ni kazi ya watu wachache, inahitaji ukichaa fulani kuifanya, maana haingii akilini kwamba unakwenda kupambana na mazombi yaliyokuja kufa, yapo tayari kujilipua kwa misingi ya kidini na hayajaja yakiwa na nia ya kupona wala kutoka salama. Komando wa nchi yoyote anastahili pongezi popote alipo.
Mkuu kwanza Poleni wakenya wote.

Lakini nikukumbushe kuwa kazi ya jeshi linapokuja suala la kifo hakuna tofauti na hao magaidi wa kujitoa muhanga. Tofauti ni kuwa gaidi anajitoa kufa kwa maslahi binafsi wakati mwanajeshi anajitoa hata kufa kwa maslahi ya taifa.

Hawa wanajeshi ni wazalendo wa kwanza.
 
Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
12,245
2,000
Waziri wa ulinzi amehutubia na kusema jengo lote la hoteli ya Dusit lenye orofa saba lipo salama baada ya mapambano makali baina ya makomando na magaidi wa kujitolea mhanga. Hadi sasa imeripotiwa vifo vya watu sita.
Ama kwa kweli kazi ya ukomando ni wito, ni kazi ya watu wachache, inahitaji ukichaa fulani kuifanya, maana haingii akilini kwamba unakwenda kupambana na mazombi yaliyokuja kufa, yapo tayari kujilipua kwa misingi ya kidini na hayajaja yakiwa na nia ya kupona wala kutoka salama. Komando wa nchi yoyote anastahili pongezi popote alipo.
Wakenya tuzidi kuiombea nchi yetu na kutoa ushirikiano wowote kwa wana usalama kila tunapohitajika.

Matiang’i: All Dusit buildings now secure
poleni sana jirani zetu, pole Mheshimiwa sana Rais Uhuru, rais ninayekukubali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
REDEEMER.

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
8,938
2,000
Hivi kumbe mpaka leo bado wanawatesa? Na US troops na Royal Army juu? Dah aisee
 
Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
12,245
2,000
Mimi ninadhani hili ni kipindi kigumu kwa wakenya na si vizuri kutoa habari zisizokua na uhakika kwa lengo la kutaka kupata sifa, hadi asubuhi hii bado magaidi yanalipua mabumu, hii habari ya kusifia makomando kumaliza kazi chanzo chake ni kipindi?.

Hakuna hata chombo cha habari kilichotaja ushiriki wa makomandoo wa Kenya, wanataja POLISI, KDF, hao wanapambana na majambazi hapo Nairobi, na askari kazu, hao makomandoo mbona hawajatajwa popote pale, hizi sifa za kijinga mtaacha lini wakati nchi unaendelea kushambuliwa?, badilikeni na mjue uwezo wenu bado ni mdogo mnahitaji kujifunza zaidi badala ya kuendelea kusifia makomandoo ambao hawapo na hawana uwezo.

Sent using Jamii Forums mobile app
hivi Makomando jeshi gani?
unapotaja KDF je Makomando sio sehemu ya KDF?
MK254 saidia hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
rutegeramisi gwategera

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
419
500
Waziri wa ulinzi amehutubia na kusema jengo lote la hoteli ya Dusit lenye orofa saba lipo salama baada ya mapambano makali baina ya makomando na magaidi wa kujitolea mhanga. Hadi sasa imeripotiwa vifo vya watu sita.
Ama kwa kweli kazi ya ukomando ni wito, ni kazi ya watu wachache, inahitaji ukichaa fulani kuifanya, maana haingii akilini kwamba unakwenda kupambana na mazombi yaliyokuja kufa, yapo tayari kujilipua kwa misingi ya kidini na hayajaja yakiwa na nia ya kupona wala kutoka salama. Komando wa nchi yoyote anastahili pongezi popote alipo.
Wakenya tuzidi kuiombea nchi yetu na kutoa ushirikiano wowote kwa wana usalama kila tunapohitajika.

Matiang’i: All Dusit buildings now secure
Aisee poleni Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
12,245
2,000
Dah wabongo bhana kwa kuchonga hatujambo! Kwani makomando wako wapo vitengo gani? Makamando wapo ndani ya KDF kwa Kenya kama ilivyo kwa JWTZ tanzania. Hata ndani ya polisi kuna makomandoo...mashambulizi ya kigaidi sio jambo la Kenya tu bali ulimwengu mzima na kudeal na magaidi tena ndani ya majengo ambayo ndani yake kuna Raia wema sio jambo jepesi ...linahitaji trained personnel. Kwa hili vyombo vya usalama Kenya vinahitaji pongezi maana vifo ni vichache kuliko mpango wa hao wahalifu wasio na huruma.
@soine bora umeona umbumbu na ujuaji wa huyo jamaaa. Mara nyingine bora kunyamaza kimya kuliko kufungua domo linalonuka. Unajifanya kujua kumbe hajui chochote...heko wanajeahinna wana usalama wa Kenya
hivi Makomando jeshi gani?
unapotaja KDF je Makomando sio sehemu ya KDF?
MK254 saidia hili

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
14,406
2,000
Jamaa wamekuja kuadhimisha miaka mitatu (3) tangu shambulio lao la mwisho lililofanyika 15.01.2016.
wakarudi 15.01.2019.
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
22,047
2,000
hivi Makomando jeshi gani?
unapotaja KDF je Makomando sio sehemu ya KDF?
MK254 saidia hili

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwenye jeshi lolote huwa kuna kundi maalum ambalo huitwa special forces, hata huko kwenu kunao ambao huonyeshwa kwenye tamasha la kitaifa.
Hawa jamaa hupitia mafunzo ya kila aina na huchaguliwa ndani ya jeshi, ili ujiunge nao lazima upitie mazoezi yasiyo ya kawaida, kule Marekani kuna makundi mbali mbali ya aina hii wakiwemo Navy SEALS, Delta Force n.k.
Yaani usaili wa Navy SEAL unapitia mambo makubwa hata kabla hujachaguliwa kuanza mafunzo.....

mkuu pole kwa kujibu lakini nilikuwa namasuta huyobkanya boya asiyeelewa kuwa kila jeshi lina kikundi chenye mafunzo maalum ya ukomandoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,452
2,000
th
kama wameshindwa watuombe msaada tuko vizuri...
th
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,443
2,000
Dah wabongo bhana kwa kuchonga hatujambo! Kwani makomando wako wapo vitengo gani? Makamando wapo ndani ya KDF kwa Kenya kama ilivyo kwa JWTZ tanzania. Hata ndani ya polisi kuna makomandoo...mashambulizi ya kigaidi sio jambo la Kenya tu bali ulimwengu mzima na kudeal na magaidi tena ndani ya majengo ambayo ndani yake kuna Raia wema sio jambo jepesi ...linahitaji trained personnel. Kwa hili vyombo vya usalama Kenya vinahitaji pongezi maana vifo ni vichache kuliko mpango wa hao wahalifu wasio na huruma.
Unaposema vifo ni vichache, ulitegemea kuanzia watu wangapi ndio useme ni vichache, na hadi sasa waliokufa ni wangapi?, subiri hadi tukio lifike mwisho ndio useme hivyo. Kuhusu makomandoo wanapatikana Katika jeshi la Ulinzi pekee na ni watu maalumu ndani ya Jeshi la ulinzi wanaopewa mafunzo maalumu, hawapatikani POLISI kama unavyodai.

Kawaida ni pale wanapoombwa kushiriki tukio endapo majeshi na wanajeshi wa kawaida wameshindwa. Wakati wa West gate attack hao makomandoo walikua wapi mbona magaidi yalitamba kwa zaidi ya siku NNE, kwasababu kule KDF walifanya vibaya, husikii kutajwa makomandoo, ila kwasababu kuna dalili za kufanya vizuri this time, ndio unasikia makomandoo, subiri mwisho kama hao magaidi hawatokamatwa, hutosikia makomandoo wakitajwa tena, wakenya ni watu wa kupenda sifa za kijinga always.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
10,742
2,000
Inaripotiwa kwamba Watu 15 wameuawa ktk shambulio la Kigaidi lililotokea ktk Hotel kubwa ya kifahari ya DusitD2 Jijini Nairobi Kenya, aidha Kundi la Kigaidi la Al-Shabaab limedai kuhusika ktk shambulio hilo.#MillardAyoUPDATES (AFP) millardayo on Twitter
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,443
2,000
@soine bora umeona umbumbu na ujuaji wa huyo jamaaa. Mara nyingine bora kunyamaza kimya kuliko kufungua domo linalonuka. Unajifanya kujua kumbe hajui chochote...heko wanajeahinna wana usalama wa Kenya

Sent using Jamii Forums mobile app
Heko wakati hakuna hata gaidi hata mmoja hadi sasa aliyekamatwa na idadi ya waliouliwa inaongezeka?, very weak security organs, nchi imegeuzwa kuwa punching bag na Alshabab, bure kabisa ninyi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,044
2,000
Hali ilivyokuwa kama ilivyoripotiwa na mwandishi maarufu wa habari za uchunguzi Bw. Allan Namu wa nchini Kenya. Allan Namu asubuhu ya tukio walikuwa wanapita maeneo ya Westland jijini Nairobi na walipofika mtaa wa Riverside Drive ghafla wakajikuta katikati ya eneo la tukio .Walihatarisha maisha yao kwa kusimama na kurekodi hatua kwa hatua kilichokuwa kinatokea.
Source : africa uncensored
On the afternoon of Tuesday, 15th January, 2019, armed gunmen stormed into 14 Riverside, a corporate campus in Westlands, Nairobi that hosts offices of several corporates, a restaurant and a hotel, DusitD2. The Africa Uncensored crew, which was nearby, was the first at the scene and this is a compilation of how the attack unfolded. Source : Africa uncensored.
Walikuwa wanajua mchongo hao
 
Adnan1984

Member
Dec 6, 2018
23
45
Mbona hao Al shabbabu hawavamii Tz, Uganda, Rwanda, Burundi, Zanzibar, Sudani na kwingineko badala yake wavamie Kenya? Hii ni zaidi ya mara moja wanavamia kenya .Hivo tusiangalie tukio tuangalie sababu zipi zinapelekea kenya avamiwe? Logically huwezi ondoa tatizo bila kujua chanzo ni nn.
Wakae chini wajirekebishe na kuokoa maisha ya wakenya wanaokufa bila hatia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom