Poleni sana wana Arusha


K

KIBAHA ONE

Member
Joined
Jan 16, 2013
Messages
35
Likes
0
Points
0
K

KIBAHA ONE

Member
Joined Jan 16, 2013
35 0 0
Habari za jioni wana J.

Tumepokea yote yaliyowasibu ndugu zetu wa Arusha kwa masikitiko makubwa sana, pia mwanzoni hatukuweza kuamini kuwa Tz imefikia kuwa nchi za Watu wanaoua wenzao kama wanauwa simba, nyati na wanyama wengine wa porini, kwa kweli inataka moyo kuamini yanayotokea. Kuna mambo yanaendelea kuumiza kichwani na ningependa Watawala wetu watupe majibu sahihi sisi Wanzania :-
  1. Kwa nini katika Chaguzi zote ndogo zilizofanyika tarehe 16.06.2013, kumetoka watu wengi kujeruhiwa kila kona ya Kata zilizofanya uchaguzi huo na hakuna hatua zozote stahili zilizochukuliwa ?.
  2. Hivi kwa nini Mkuu wa Wilaya ashiriki kuteka Wapiga kura na hakuna hata Kiongozi yeyote aliyejitokeza kukemea kitendo hicho ?
  3. Kwa nini Mwigulu Nchemba, Mwampamba, Nape na Juliana Shonza wanahuburi umwagaji wa damu katika majukwaa mbele ya Polisi, lakini mpaka sasa hawajachukuliwa hatua zozote na vyombo vya Usalama ?
  4. Hivi ni kwa nini Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeshindwa kulaani mauaji yaliyofanywa Arusha, kama tulivyozoea kwa matukio mengine yanayolikumba Taifa ?
  5. Kwa nini Viongozi wakuu wa Bunge wameshindwa hata kufika Arusha kuwajulia hali Majeruhi wa Bomu na Mhe mbunge Joshua Nasari ambaye alishambuliwa mchana kweupe huko Makuyuni ?
  6. Je, nitakuwa nimekosea kusema kuwa yote yaliyotokea Arusha na katika Kata zingine zilizofanya uchaguzi tarehe 16.06.2013, yaliratibiwa na kusimamiwa na CCM na Serikali yake ?

Natamani sana kama nitapata majibu ya maswali yangu.

Tanzania ni nchi yetu wote,
 
H

Honolulu

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
5,650
Likes
35
Points
145
H

Honolulu

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
5,650 35 145
Jakaya ndiye mratibu mkuu wa mauaji ya kidini na kisiasa yanayotokea kote nchini kwa sasa! Hakuna haja ya kumumunya maneno! Wala tusiwalaumu polisi! Hao polisi wanamtiii tu kadri ya viapo vyao kwake. Ukweli ndio huo!! Mwenye masikio ya kusikia na asikie!
 

Forum statistics

Threads 1,275,212
Members 490,932
Posts 30,535,930