From Sir With Love
JF-Expert Member
- Sep 13, 2010
- 2,072
- 3,827
Nimeamka mapema leo, na kabla ya kutoka kitandani, nikawa nawaza watu mbali mbali hapa duniani wanaopitia masaibu tofauti tofauti.
1. Wazazi waliokuwa wanategemea kumzaa mtoto mzima lakini baada ya mama kujifungua, madaktari wanawapa taarifa kwamba wamezaa Mtoto mlemavu - Kama humjui Mungu unaweza ukasema au kutenda kitu cha ajabu.
2. Mzazi aliyeletewa taarifa ya kifo cha mwanawe. Sipati picha hayo maumivu.
3. Wote wanaoguza hospitali mbali mbali kwa muda mrefu na mfupi na hasa za serikali ambazo hawatoi chakula, na hivyo kumpelekea chakula mgonjwa kila siku Na ilhali, hali ni ngumu.
4. Waliopata taarifa za msiba wa wazazi, ndugu, Jamaa na marafiki.
5. Wote ambao wanatamani kufanya kazi lakini hawajapata nafasi ya kujiajiri au kuajiriwa kwa sababu ya ukosefu wa ajira au mtaji. Kupata usingizi wa kueleweka Kama hukai nyumbani ni ngumu.
6. Walio rubuniwa penzi kwa njia moja au nyingine, ilhali walikuwa waaminifu, aidha kwenye ndoa au kabla.
7. Mama anayelia kila siku kwa sababu ya ulevi wa mume wake. Kila shilingi anayopata baba inaishia baa mpaka ada za watoto zimekosekana.
Niwatakie Amani ya Mungu ishindayo amani yote. Mungu Na awaangazie nuru na kuwalinda, Mungu na awatangulie kwenye maisha yenu.
Sent using Jamii Forums mobile app