Naandika kwa huzuni kubwa na kughafilika sana, Mimi ni mtumishi halmashauri fulani, tatizo lilianzia idara ya utumishi nilikopa mkopo wa kujikimu/ life start-up kupitia mfuko wa jamii wa PSPF kupitia bank washiriki TPB. Afisa utumishi wakati anaingiza makato walikosea code ya bank na makato yangu hayaelekezwi banki husika yanabaki hazina, kila nikifuatilia wananiambia niandike barua kwa katibu mkuu hazina, nimeandika barua lakini kuipitisha kwa mkurugenzi tu ili ipigwe muhuri imetumia miezi miwili naambiwa nisubiri, hapo hapo banki wameandika barua kwa afisa utumishi na afisa utumishi akatengeneza mkopo mwingine wa malipo ya TPB/ Tanzania postal bank, nimelalamika hadi kwa mkirugenzi lakini sipati ufumbuzi, wanajamvi naombeni msaada maana natamani hata niache kazi za kitumwa