puza46b
Member
- Nov 3, 2010
- 91
- 261
Iliandikwa mwaka jana...
Ndugu zangu wa Tanzania, poleni kwa mafuriko. Hii ni mara ya pili nalazimika kufafanua tatizo la mafuriko, na umuhimu wa watu kuamka na kujua kwamba huu ni mwanzo tu na tutashuhudia majanga mengi ya mafuriko mbeleni kama hali haitabadilika.
Kitu muhimu cha kuelewa hii siyo mara ya kwanza kuwa na mafuriko dar. Kwa sasa inatokea kila mwaka na vitu vingi vya thamani vinaharabika. Mtu aliyekuwa anajipanga kujenga inabidi arudi nyuma akanunue tena kitanda. Chakufumbua macho ni kwamba Mikocheni hawajalalamika kuhusu mafuriko na nakumbuka yalikuwa yakitokea sana huko.
Sababu kuu nne za kuongezeka matokeo ya mfuriko ni hizi.
1. Nyumba na mabati, na viwanya vya zege.
Mvua ikinyesha, miti na majani yanakuwa kama sifongo (sponge). Maji yanatiririka taratibu kwenye majani na kupunguza maji yanayoingia kwenye mikondo. Kutanuka kwa mji kumeongeza mabati yanaomwaga maji kwenye mikondo. Hii ndiyo sababu leo Bunju wanapata mafuriko ila miaka 20 iliyopita hilo halikuwa tatizo.
Kuna masuluhisho mawili kwenye hili tatizo lililoletwa na ukuwaji wa mji. La kwanza ni kila nyumba kuwa na jinsi ya kukusanya maji ya mvua hii itapunguza maji yanayoenda kwenye mifereji na kusaidia kutatua tatizo la upungufu wa maji. Suluhisho la pili ni serikali kuweka sehemu za mabwawa ya maji ya dhoruba (stormwater management ponds). Haya yanatumika sana sehemu ambazo ni tambarare. Kwa kifupi, design principle ni maji yanayoingia yanakuwa mengi kuliko maji yanayotokwa kwenye bwawa. Hili suluhisho linapendwa sana na landscape architecture kwa sababu linaongeza madhari ya mitaa. Shida linaongeza mbu ambao wanaweza kuwa managed kirahisi. Kufanikiwa suluhisho la pili kunahitaji miji kupangwa vizuri.
2. Kuharibiwa na kuzibwa mikondo ya maji.
Hili linaeleweka, watu wamejenga kwenye mabonde na wamezuia njia za maji kwenda baharini. Cha kutia aibu mtu msomi anaamua kuweka kifusi mbele ya nyumba yake akidhani maji ya mafuriko hayatafika kwake. Pia taka zinatupwa kwenye mifereji au mtu anaweka mchanga kuruhusu gari liingie kwake bila kuweka culvert/ njia ya maji. Hili tatizo ni sugu dar nzima. Waliosema maji hayazuliki kirahisi hawakukosea. Hili tatizo ni rahisi kutatua kama uma utaelemishwa. Pia kila mwanamtaa anatakiwa aangalie maslahi ya mtaa wake. Ukikaa kimya wakati nyumba inajengwa kwenye mkondo wa maji usilalamike siku kukiwa na mafuriko.
3. Mabadiliko ya hali ya hewa.
Ukiona wazungu wanaokaaa kwenye barafu wanajaribu kujitayarisha na ongezeko la joto duniani, wewe unayekaa kwenye equator inabidi upate hofu. Kila model za hali ya hewa zinaonyesha kuwa nchi masikini (Tanzania mojawapo) zitaathirika sana na hali ya hewa. Wezentu (wazungu) wanajitayarisha kwa sababu wanaelewa gharama za mafuriko (Home — Climate-ADAPT ). Sisi inabidi tuache kufumbia macho swala muhimu la kupanga miji yetu. Kwa kawaida miji mingi inadesigniwa kuhimili mvua nzito inayoweza tokea mara moja katika miaka mia moja (1:100 year event). Mabadiliko ya hali ya hewa yanalazimisha miji ya wezentu kuomba kampuni zifanye uhakiki wa miundo mbinu yao pale 1:200 year event ikitokea. Sasa daraja la wami limesombwa mara ngapi? Kuna kipindi nilishawahi kuuliza hivi inakuwaje daraja la wami linasombwa na maji kila mwaka na bado tunalijenga kwa style ile-ile? Sikupewa jibu.
4. Kutojipanga.
Hili pia linaeleweka: kwa nchi zilizoendelea kabla ya mtaa kujengwa inabidi kieleweka, barabara iko wapi, maji safi na maji taka yatapitia wapi, maji ya mvua yatatokaje, na umeme/gas itaingiaje.. kisha ndo watu wanapewa vibali vya kujenga. Sisi tunaanza na cha mwisho. Serikali inaweza ikaingia ubia na watu binafsi kutayarisha miji kukua. Tatizo sisi kila kitu ni dili na mfano mzuri ni kigamboni project. Serikali inatambua hilo na ndiyo maana land development Tanzania ni shida kwani serikali haitaki watu wanyonywe. Hili linaweza tatuliwa kwa kuwa na tender. Wanaotaka kuendeleza ardhi wawakilishe michoro yao na plan zao na waseme watauza ardhi kwa bei gani wakishaiendeleza. Kisha wapewe contract vigezo vikiwa mipango mizuri na bei ndogo.
Wazo la mwisho:
Ili nchi/mji uendelee, kila kitu inabidi kifanye kazi inavyostahili. Mji kusimama siku tatu kwa sababu ya mvua ni aibu. Tumesomesha wengi na wanalijua hili lakini haieleweki ni kwa nini bado tuna tatizo la kutojipanga. Ni kwa miujiza ya mungu hatuna tatizo la kipindupindu haswa ukiangalia ambavyo maji taka hayashughulikiwi.
Mh. Maghufuli anataka nchi iwe ya viwanda, kama tukijenga viwanda na hatujajitayarisha kuwapokea hao wanaotoka vijijini kuja kutafuta kazi kwenye viwanda, tutakuwa tunaweka mazingira ya kuwa na slum kama za Kibera (Nairobi) au favela (Brazili). Miji imbayo haijapangwa. Maendeleo tutakayoyapata yatakuwa yanapunguzwa kasi na matatizo kama haya ya mafuriko. Miundo mbinu inayojengwa haswa reli ni rahisi sana kuharibiwa na mvua. Dodoma inahatari Zaidi ya kuwa na mafuriko kwa sababu sehemu nyingi ni tambarare (na wenyeji wanapaita idodomela). Serikali inabidi ijipange.
Nawaachia hapo mtafakari.. Tanzania mpya inawezekana. Tupige kazi.. kila sehemu!!