sir j
JF-Expert Member
- Mar 7, 2016
- 319
- 214
Pole sana ndugu na jamaa mnaoteseka katika nchi yenu. Maumivu yenu ni maumivu yangu pia, Najua mlikuwa na malengo mazito ila binadamu sio wa kuamini hata kidogo. Nimeshuhudia mkijaribu kutafuta pa kujishikiza kwa muda kama huna ndugu, jamaa au mchumba pale, unaishia kuambiwa "tukikupa nafasi alafu post yako ikatangazwa kesho si utatukimbia hebu subiri post yako inatoka mda si mrefu"
Pengine ungeamua kuingia mkataba wa mwaka au miaka, au ulitamani usome kozi fupi ya mwaka au miezi sita ila kwasababu unasikia post yako ipo karibu basi unaamua kuacha na kuisubiri. Umesubiri mwaka sasa na miezi, bila majibu.
Nakumbuka uliambiwa oooh mara unaandaliwa fedha ya kujikimu ili uendapo huko usiangaike kuisubiri,, njia ya mwongo ilivyo fupi siku zikakimbia ikafika mda uliohaidiwa pole sana. Basi ooh tunasubiri bajeti ya kikao chetu ili tuanze mwaka mpya wa noti na wewe utakuwa miongoni, mimi binafsi nikajiuliza "hivi mbona miaka ya nyuma ilikuwa wenzako wanaitwa kabla ya kikao hicho?!, hivi hawakujua kwamba wewe upo,!?, ila basi tu nikaona ngoja nikubali kama wengi wakubalivyo bila kushirikisha fikra zao.
Ila Muumba na kuumbua akazisogeza siku na kikao kikaisha bila wewe kufikiriwa, pole sana.
Sasa ikaibuka nyingine mpya kwa kuwa maneno hayalipiwi, wakaja na nyingine nzuri kuliko eti tunataka tuwatoe kwanza wasio stahili ili wewe uje uingie,,,,, nikawaza pia hivi wewe na wale MNA uhusiano gani. Kwa roho ya busara itokayo mdomoni na si kwingineko ukaambiwa ni jua moja na na nusu au majua mawili na haitozidi hapo, na kufikia 13/08/ ndo majua mawili yakawa yamekamilika bila dalili za wewe kuitwa pole sana.
Cha kushangaza, wanasema aliyeshiba msikilize kauli usimwangalie tumbo,,,, wakushiba wakasema "jiajilini usisubiri kuitwa," hivi kweli kwanini niliamua kwenda hadi huko kama ni kujiajili si ningeenda Veta, sido, bagamoyo, au ningeshika jembe" ila nawaangalia kwa dharau maans si kila kitamkwacho mdomoni uchujwa na akili, mengine utokea tu katika kwenye mzunguko wa chakula.
Kaka yako, alikwambia ukajitolee ili uwe unapata uzoefu, ili pia nikajiuliza hivi ukitoka huko unakojitolea utakula nini, utakunywa nini, pole sana.
Pole sana ndugu yangu maana naona unatafuta kila njia uishi kama binadamu wengine, umekopa mtaji umeanza ujasilia mali, sasa je ukiitwa utakuwa bado unakumbumba uliyoyasoma au kichwani sasa umejaza bei za nyanya, soko la mihogo, jinsi ya kupata abiria wa bodaboda yako na jinsi ya kuziba pancha za baiskeli,,, kwa jicho la mbali nawahurumia wale unaowapelekea hiyo elimu ya kachumbari maana mpaka sasa naona vitunguu ndo vimezidi nyanya na matokeo yake ni kuzalisha mabomu kama sio mabogasi, pole sana.
Nakupa pole wewe, ila niwape pole pia wale waliokutegemea, najua walikutambua kuwa unaweza kuwa mwanasheria mzuri, au injinia ila wakasema nenda ualimu na udaktari mwanetu huko ndiko kuna uhakika wa kuitwa, leo wakikuona unaamka mikono mashavuni, huku ukilaani ns kulaumu, na kula vyao,,, wanachukia ila hawana jinsi maana kilio cha wanakielewa tu.
Bora wangetoa orodha na siku ya kuitwa au wakasema hatuna uwezo wa kukuita, naamini leo hii ungekuwa mbali kwani ungepigana bila kuangalia nyuma, lakini sasa kila unapopiga hatua, lazima ugeuke kusubiri kuitwa pole sana.
Siwezi kusema mengi maana hata haya machache kwa asiyejua uchungu ulio nao, anayaona ni matusi, ujinga, na upumbafu, maana uchungu wa mwana anaujua mwana mwenyewe pindi ajikwaapo kidole.
Mbali na yote nakuombea kwa Mungu ndugu yangu,,, nawe omba wenda sikitiko la ujumbe huu likafungua baraka, japo nina mashaka na unachokwenda kukifanya maana, ulishakata tamaa mwaka mzima hadi waliokupungia mkono wakati unatoka leo hii uko nao pole sana.
NI MAWAZO YANGU YALIYONITOKEA USIKU WA LEO, WALA SIJAJUA NIMEYAANDIKAJE NA SIJUI NIMEMWANDIKIA NANI, Ila pole Mungu akusaidie, kilio chako ndio kilio changu.