Pole January Makamba

Pole January Makamba

MKAMA6

Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
65
Reaction score
110
Ndugu wana jf na wa Tanzania kwa ujumla ,leo katika sikukuu hizi za Noel na Mwaka mpya na taka niwapashe yaliyo jili katika jijij la Mwanza .Jana nili bahatika kukutana na January Makamba katika hotel ya Victoria Palace,alitukusanya tulikuwa Wachungaji na Wainjilisti 152 kutoka kakitika madhebu mbalimbali ya kikristo katika mikoa ya Mwanza,Geita,Shinyanga,Mara,na Kagera.Kikao kilianza saa mbili na dakika hamsini na tisa usiku na kumalizika saa tano na dakika ishilini na tatu usiku.Katika kikao hicho January alikuwa amevalia suti yake nyeusi na shati nyeupe ikiambatana na tai nyekundu, kweli kijana ulipendeza kwa vazi hilo cha kunisiki tisha ni pale ulipo anza kujifananisha na nabii Yeremia,nilikusikiliza ukisoma kitabu cha Yeremia moja na kwamba kwa maneno yaliyomo katika kitabu hicho yanakushawishi kutangaza nia ya kugombea uraisi mwaka 2015 vivyo unatuomba sisi watumishi wa Bwana tukuunge mkono na tuwashawishi waumini wetu pia.Ndugu January nikweli unashauku ya kuwa Raisi wa Tanzania lakini naomba nikuulize kupitia waraka huu maswali yafuatayo

1. Watanzania wameshuudia chama chako kupitia wabunge wake mkimzushia mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani kwamba alifanya siasa za udini kwa kukutana na watumishi wa Bwana kule Arusha ,sasa hiki ulicho kifanya jana ni Kuharalisha udini au ulikuwa unabadili dini?.

2.Mfuasi wako uliye mtuma kuandaa kikao hicho,Bwana Mustafa kada wa chama cha mabinduzi nikati ya watuhumiwa ,wa mipago hovu ya kuandaa vijana waliyo kwenda na nia ya kudhuru kule Kigoma hivi majuzi sasa nikuulize unapata wapi mamlaka ya kimahadili ya kuandaliwa kikao na mtuhumiwa wa utesi tena kikao na watumishi wa Bwana uoni kwamba unamsanifu Mungu?.

3.Ulitupatia posho ya shillingi elfu hamsini kwa kila mmoja wetu,ulitupatia chakula na vinywaji ,ulitukodishia hoteli, ulitukudishia gari aina ya costa no T926 BDP mali ya bwana Mukeshi ambayo ndiyo ili beba mabaunsa wa Matata kwenda Kigoma hivi majuzi,gharama zote ni takribani millioni ishilini tunashukuru lakini tujiulize,hizo pesa za kutuonga ulipata wapi?,kwanini unataka kununua Uraisi?,Je kwa pesa hiyo unge chonga madawati mangapi kwa ajili ya watoto wanao kaa chini uko Bumbuli? na je unafikili kutuonga sisi utakuwa umewaonga na waumini wetu?.

4.Wewe ni mshilika wa Bwana Rowasa,ambaye pia anakiu ya Uraisi kama wewe lakini pia wewe pia ni mshilika wa Ngeleja ambaye pia kiu ya Uraisi sasa niku ulize tumpigie debe nani kati yenu? ,au mnatafuta kura za sambusa yaani wawili tujitoe mmoja apite?.

5.Umelifanyia nini taifa mpaka uone unaweza kuwania Uraisi,wakati suala la tozo za simu ambalo ni mzigo wa dhambi kwa wananchi,limekushinda ukiwa kama naibu waziri wa wizara usika au una maslahi na makampuni ya mawasiliano,kama sivyo uoni ukiwa Raisi utaleta na kodi ya kusikiliza redio.

6.Unalisemeaje suala la operationi tokomeza ujangili ambayo imetesa na kuuwa wasiyo na atia wakati watuhumiwa wa ujangili akiwemo kinana katibu mkuu wa chama chako bado wana kula bata?.

7'Tuambie nini kimekushawishi kuwa na nia ya kuwa Raisi?.

8.Tuambie nikiongozi ghani wa upinzani unaona anaweza kuwa Raisi kama wewe utopata fursa ya kuwania uraisi?.

9.Kunatetesi kuwa wewe na baba yako mlishiliki kumuondoa Sherukindo kwenye nafasi ya kuwania ubunge jimbo la Bumbulina kukupitisha wewe bila kupingwa kwenye CCM,Sherukindo aliye kuwa mwenyekiti wa kamati yakudumu ya Bunge ya nishati na madini ambaye alisimama kidete juu ya kashfa ya Rich mond iliyo muondoa Rowasa kwenye kiti cha uwaziri mkuu,ambaye ni swahiba mkubwa kabisa wa Mzee Makamba baba yako aliye kuwa katibu mkuu wa CCM?[Comflictof interest] leo ukifanikiwa kuwa raisi si utatengeneza mamlaka ya kifamilia?.

10.Nikumbushe ile divishion four ya formu six kule kigoma uli isafisha lini?.Au na wewe ni muhumini wa division five

11.Niambie leo unawambia nini wa endesha boda boda wa Mwanza au unaomba day waka?.

Mwisho jipime

-----------------------

 
Last edited by a moderator:
Hivi bado siku ngapi kufika 2014? Bado yako mengi yanakuja tuandae masikio tu!
 
Umelishwa, umepewa usafiri wa kuja na kurudi na wa ndani,umelipiwa chumba, vinywaji nadhani na umelipiwa na zinaa ulio ifanya mwza. Baada yayote umepewa na 50000. Nahumo kwenye kikao hukuyasema haya mbele ya January unatuletea sisi huku je unataka tukujibu nini wakati ww ulionana na January uso kwa uso kama sio mbumbavu ninani?
 
Alichofanya mleta uzi ni kufikisha ujumbe tu kuwa maikakati ya chini kwa chini ishaanza na JM anauchu wa hii kitu URAISI. Ama hakika ukicheka na nyani utavuna mabua. Tulicheka na manyani weeeeeeeeeeeeeeee sasa mabua twavuna. Yameanzia makanisani tusubiri na CD za wale jamaa. KAZI IPO.
 
Hivi mtu mlikiwa nae masaa yote pale kwanini haya maswala usimuulize pale pale nadhani angekupa majibu stahiki,sasa umeyaleta hapa kutaka kumdhalilisha au kutaka nini? Sijaelewa nia yakuleta haya hapa

Sasa angepata posho kweli kama angeuliza maswali wakati wa mkutano? Kwani kila mkutano una muda wa maswali na majibu?
 
aah ww c mjanja mgemshawishi mfanye vikao kama 10 kabla ya 2015 na posho iwe laki moja, halafu hamuwashawishi waumini wenu
 
Naona vijana wamechoka kuwa Taifa la kesho... Chadema Zitto anataka kuwa rais, CCM January Makamba, Nccr ni Kafulila. Ngoja tuone vibabu vs tuvijana...patamu hapo.
 
Wamarekani wanataka Makamba Jr awe Rais, wanaamini chini ya Makamba Jr Masilahi yao yatakuwa salama...Fedha za kumuwezesha tayari zipo...
 
Back
Top Bottom