POINT OF NOTICE: CHADEMA wakija na tamko jingine refu..

Don't misunderstand me...ni zaidi ya kufukuzana..ni suala la maono, ni suala la sera n ni suala la mwelekeo wa chama. Kufukuza wanachama na kuacha mfumo unaotengeneza matatizo hautatatua tatizo.

Itakuwa ni sawa nakutupa mahindi yaliyokobolewa vibaya huku kuacha kufanyia matengenezo mashine iliyokoboa vibaya.

Kabla ya kutimua watu wajiulize : je mfumo wetu unaweza kuboreshwa vipi ili kupunguza na hata kuondoa baadhi ya matatizo?
 
Ni kweli kabisa Mkuu kwasababu ahadi tulizowaahidi wananchi mwaka 2010 hatujazitekeleza kama ile ya kubadilisha kigoma kuwa Dubai ya Afrika.......

Maandamano na utitiri wa viwanda vya uongo ndio sababu ya kushindwa utekelezaji wake,tulieni kama mnanyolewa nywele za kwapa muone mziki wa gamba.

Vipi na wewe utakuwepo mstari wa mbele msituni au wewe ni wa mtaa wa Togo miguu kwenye ndoo ya maji usiku na mchana ukiandika uongo na kumtetea babu kwenye mitandao.
 
Maandamano na utitiri wa viwanda vya uongo ndio sababu ya kushindwa utekelezaji wake,tulieni kama mnanyolewa nywele za kwapa muone mziki wa gamba.Vipi na wewe utakuwepo mstari wa mbele msituni au wewe ni wa mtaa wa Togo miguu kwenye ndoo ya maji usiku na mchana ukiandika uongo na kumtetea babu kwenye mitandao..........

Hapana nipo Mitaa ya Ngorongoro na Serengeti na katibu mkuu wenu tukiwinda tembo
 
Ukabila tena! Mbona mnapotoka?
Usitake kupotosha mada,kumtambua mtu kwa kabila yake si dhambi hata kidogo.Nimetaka kujua tu,au wewe unajua? ni kawaida hapa jamvini baadhi ya wanasiasa kuitwa,kufanyiwa dhihaka na utani kwa kabila,wajihi wake hata muonekano wake.Kinana ni msomali,JK ni ******,Mbowe ni mchaga.Babu?
 
Mkuu MM,

Nimewahi kuandika hapa, na nimewahi kuongea na marafiki zangu wanazi wa CDM, ni hivi CDM haikujengeka kwa kuwa they are good strategists, b'se they are smart, CDM imejengwa na udhaifu wa CCM. Mfano Kujengeka kwa chama kwa ajili ya kukemea Mafisadi, hiyo single wanasiasa wa CDM wakaifurahi sana wakaipiga kuanzia asubuhi mpaka jioni, J3 had J2, Jan hadi Dec, sasa single zenyewe/yenyewe zimechokwa/imechokwa kwenye masikio ya wengi, people are now searching what else is in CDM, the reality is that thing missing ....

CDM wamekuwa wazuri kuzungumzia mambo utekelezaji, [implementation issues] na hili ni jambo rahisi sana. na Rais au Kiongozi yeyote mkluu akipatia tu kwa bahati au kwa uweledi kuweka mtendaji mzuri kwenye wizara fulani, mifano mnayo au mkoa fulani etc... immediate hoja za CDM zinapotea kama upepo wa Kimbunga.

Narudia sijaona sera, alternative thinking ya CDM ya kututoa tulipo... I have just seen another cheap politics....

e.g. Mikutano na Maandamano ni lazima zifanyike ile jamaa wanaotegemea chama wapate fedha... not b'se there is clear direction or vision.
 
Kumfukuza mwanachama kwa kutofautiana katika maamuzi au misimamo ni kubaka demokrasia,wanachama wote wanahaki sawa katika kutoa maoni na kusikilizwa.Kwa kiongozi kutumia nafasi yake kufukuza watu ni dalili tosha uwezo wa kuongoza watu ni mdogo.

Kama JK alivoonesha udhaifu wake kwa kushindwa kuongoza nchi yenye asali, maziwa na matunda na kutufanya tule mizizi au mlo mmoja kwa siku.

(Sijui kwanini Watanzania ni masikini)
By JK.
 
Heshima mkuu MM ni ukweli usiopingika kuwa CDM inahitaji kufanya tathmini na kufanya
maamuzi mapya yatakayoonyesha mwelekeo yaani "way forward",kubwa ni kukubali kuwa
tatizo lipo then kulitatua tatizo.Bado CDM ni chama imara chenye nguvu ambacho kama
uongozi utajipanga upya hakiwezi kuyumbishwa na propaganda za waharibifu wa Chama
toka nje au ndani ya Chama na bado kinao uwezo wa kufanya wonders kwenye chaguzi zijazo.
 
Kama CHADEMA ngazi ya TAIFA wanazijua tofauti zao, kama wanaweza kukaa wakazizungumza, mapungufu ya kila mmoja yakawekwa wazi, unafiki wa kuchekeana huku hawaivi wala kuelewana wakauacha, ushauri huu wa MwanaKijiji unaweza kuzingatiwa.

Vinginevyo hawa jamaa hawana tofauti sana na wale wa CCM isipokuwa majina tu.
 
Mzee mwanakijiji umenena,wacahche wasiopenda kufikiri,kuthubutu akiwemo Precise pangolin wapo hapa wakijaribu kupindisha ushauri wako wenye hekima na busara.Kesho na kesho kutwa chama chao kikiyumba wanakimbilia mitaani kufanya vurugu kwa kisingizio cha maandamano na kutuhumu watu kununuliwa na Nape.
 
Don't misunderstand me...ni zaidi ya kufukuzana..ni suala la maono, n suala ka sera n ni suala la mwelekeo wa chama. Kufukuza wanachama na kuacha mfumo unaotengeneza matatuzo hautatatua tatizo.

Itakuwa ni sawa nakutupa mahindi yaliyokobolewa vibaya huku kuacha kufanyia matengenezo mashine iliyokoboa vibaya.

Kabla ya kutimua watu wajiulize : je mfumo wetu unaweza kuboreshwa vipi ili kupunguza na hata kuondoa baadhi ya matatizo?


Mimi sio mnazi wa CDM neither wa CCM, but I want to let you know... ugonjwa wa kufukuza sana hauna tofauti sana na ugonjwa wa Ubaguzi, hauishii kwenye mjumbe wa mtaa, siku zingine mwenyekiti wa Wilaya, then Mkoa etc, itakuwa hiyo ni sera forever...ukifukuza wangu, nitafukuza wako, nani asiyejua kwamba any active politicians ambaye alikuwa active for the past 20 years alikuwa mwana CCM.... so kumbe kila mtu alikuwa CCM so what is wrong with that? Alafu... kama imani, na malengo ya chama hayako wazi, au awareness iko chini inapima vipi kwamba huyu haelewi itikadi za chama na huyu analewa?

Naungana Mzee Mwanakijiji.

In short ameelewa kwamba taifa bado lina tatizo... no strong, structured, sustainable, organized political party ndio sasa tuwasaidie CDM kama wataweza... but my worry is... Tanzania ni nchi ya ajabu sana na watu wake pia... CDM ikishindwa 2015.... jua kutazuka another strong political party which we don't know now... kwa nini WaTanzania wanaingia kwenye vyama vya upinzani sio kwa ajili kuleta mabadiliko bali kushinda, so wakishindwa wanaua chama... trend... NCCR-Mageuzi, CUF.....
 
Usitake kupotosha mada,kumtambua mtu kwa kabila yake si dhambi hata kidogo.Nimetaka kujua tu,au wewe unajua? ni kawaida hapa jamvini baadhi ya wanasiasa kuitwa,kufanyiwa dhihaka na utani kwa kabila,wajihi wake hata muonekano wake.Kinana ni msomali,JK ni ******,Mbowe ni mchaga.Babu?

Taja kabila lako kwanza ndo uulize wengine makabila yao! Sipotoshi mada
 
Kama JK alivoonesha udhaifu wake kwa kushindwa kuongoza nchi yenye asali, maziwa na matunda na kutufanya tule mizizi au mlo mmoja kwa siku.

(Sijui kwanini Watanzania ni masikini)
By JK.
Ukizungumzia ASALI,kumbuka nyuki wanavyofanya kazi kwa bidii ili kuitengeneza na kuwa na ladha inayovutia,vile vile kwa ng'ombe anavyo chagua nyasi ili atoe MAZIWA bora.Kaka si matunda yote ni mazuri angalia kilichomkuta Adam na Eva baada ya kula TUNDA.Sasa wewe na wenzako siku zote msifanye kazi kwa bidii na kujituma mkae mkisubiri mzee wa mfuko wa cement Tsh 850 aje awanyweshe maziwa na kuwamwagia asali.
 
Moja ya madhaifu makubwa ya Chadema ni kuchelewa kwao kuchukua maamuzi katika masuala yaliyo waathiri kutoka nje ya Chama na hasa kama yapo ki-Propaganda. Chadema wapo haraka saana kucukua maamuzi ya haraka saana pale ambapo imewagusa moja kwa moja toka humo humo chamani na hasa kama hayo makosa yanagusa mahala/mtu nyeti hasa kimaslahi ya Chama ama yale yamefanywa kwa makusudi kwa malengo ambayo yanapelekea image mbaya.

Pamoja na u-haraka wao wa kuhandle na kurekebisha yale ambayo yanagusa chama moja kwa moja ni ajabu sana kuwa wamelifumbia macho suala ala makundi yaliyowazi ndani ya chama hadi hapa yalipofika kwa BAVICHA kudiriki kutoa tamko dhidi ya Dr. Slaa. Swali kubwa la kujiuliza hivi Chadema wana taratibu zianzofuata protocol ama kiongozi yeyote anaweza toa maamuzi ili mradi yupo na idara yake?

Makundi kwa Chama kichanga kama Chadema ni sumu na kabisa lisipotatuliwa ndipo hasa namna pekee ya kuimaliza Chadema. Kila mtu anajua athari za ‘divide and rule policy’ ni most effective kwa maadui, huku wahusika pande zote kujiona wapo superior kuliko wenzao na hali kwa adui haijalishi kikubwa mjigawe na mjichukie.



Mkuu Molemo,

Hapa ndipo mnapotakiwa umakini... Nyie si mlishasema kuwa Chadema ina maadui sana kiasi kwamba hao maadui wapo tayari kufanya lolote kwa ajili ya kukiangusha Chama? Hivi nipo curious, mmejipanga vipi na kiasi gani ili muweze kujua kama hio sio mbinu ya the so called adui kuhakikisha kuwa mnasambaratika kwa baadhi ya viongozi Chadema waonekane hawafai? Hivi huo uchunguzi huwa mnaufanya kwa muda wa kutosha na matokeo ya kuridhisha?

The way huwa wanahandle masuala yao ndiyo moja ya dhaifu kubwa lililopelekea ‘Ubovu’ ambao kama hatua haitachukuliwa mapema kwa ku estimate huo ubovu itawa cost parefu. Kuwepo kwa makundi ndani ya Chama ni suala ambalo lilikuwa lipo wazi ila lilikosa ile uwazi wa huo mgawanyiko ambao kwa sasa umeshaoneshwa wazi tokana na tamko la BAVICHA.

Kufukuza wanachama huwa mnafanya kwa mikeke sana na kwa namna ya kuwadhalilisha (that’s my IMO); kumbuka hao wanaofukuzwa pamoja na kwamba wapo considered as wasaliti – wanakuwa wametoka katika nafasi ambazo wanaijua vema CDM… Na wote twajua mtu wa kukumaliza vilivyo ni Yule wa karibu wao.

STRATEGIES za CDM kuwasimimisha hao viongozi ni kweli zinawaongezea sifa kubwa saana kuwa ni wawajibikaji na hawamchekei mtu… Ila inaleta matatizo matatizo makubwa ndani ya Chama, matatizo ambayo huwapotezea muda kuweka sawa na kuwatoa katika njia ya ku focus namna ya kujidhatiti na kuhakikisha ushindi… Wanaongeza idadi ya maadui wenye nguvu sana;

Kumbuka kuwa kuna tofauti ya kuongeza adui na kuongeza adui mwenye nguvu dhidi yako na mbaya kuliko ni kuwa wanazidi expose weakness zao na vile vile kuzidi kuelemewa hasa watumiwapo kwa ajili ya malengo ya propaganda ambazo zinaendeshwa dhidi yao… Kwa kweli CDM inatakiwa mjipange vilivyo sababu ni wazi kuwa iko targeted nje na ndani ya chama. Hio ni wrong timing kwa Chama, perfect timing kwa maadui.
AshaDii Maneno kuntu haya, maneno mujarabu, maneno yaliyojaa tafakuri jadidi. Mwenye masikio na alisikie neno hilo ambalo AshaDii awaambia mataifa. Kama CDM inataka kuwa imara zaidi basi wanachama, wapenzi na wanazi wake wasijifiche kwenye mchanga na kufumbia macho mambo ambayo hata mtoto mdogo anajua kuwa yapo. Makundi yapo lakini jinsi ya ku deal na hayo makundi kunahitaji weredi. Ukihamaki na kukurupuka kufukuzana uinaweza kuishia kukiacha chama kikiwa vipande vipande. Wanaofukuzwa nao walichaguliwa siyo waliteuliwa.

Nakala Molemo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom