Moja ya madhaifu makubwa ya Chadema ni kuchelewa kwao kuchukua maamuzi katika masuala yaliyo waathiri kutoka nje ya Chama na hasa kama yapo ki-Propaganda. Chadema wapo haraka saana kucukua maamuzi ya haraka saana pale ambapo imewagusa moja kwa moja toka humo humo chamani na hasa kama hayo makosa yanagusa mahala/mtu nyeti hasa kimaslahi ya Chama ama yale yamefanywa kwa makusudi kwa malengo ambayo yanapelekea image mbaya.
Pamoja na u-haraka wao wa kuhandle na kurekebisha yale ambayo yanagusa chama moja kwa moja ni ajabu sana kuwa wamelifumbia macho suala ala makundi yaliyowazi ndani ya chama hadi hapa yalipofika kwa BAVICHA kudiriki kutoa tamko dhidi ya Dr. Slaa. Swali kubwa la kujiuliza hivi Chadema wana taratibu zianzofuata protocol ama kiongozi yeyote anaweza toa maamuzi ili mradi yupo na idara yake?
Makundi kwa Chama kichanga kama Chadema ni sumu na kabisa lisipotatuliwa ndipo hasa namna pekee ya kuimaliza Chadema. Kila mtu anajua athari za ‘divide and rule policy' ni most effective kwa maadui, huku wahusika pande zote kujiona wapo superior kuliko wenzao na hali kwa adui haijalishi kikubwa mjigawe na mjichukie.
Binafsi yangu na nitaomba wengine waunge mkono ni Lazima sasa wahuni na waasi wote wafukuzwe chamani. Waasi wote na wanaoendekeza uhuni wanajulikana na majina yao yote yapo mbele ya Kamati kuu leo.
Tunataka wote wafukuzwe na niseme bila kuuma maneno TUMECHOKA!
Mkuu Molemo,
Hapa ndipo mnapotakiwa umakini... Nyie si mlishasema kuwa Chadema ina maadui sana kiasi kwamba hao maadui wapo tayari kufanya lolote kwa ajili ya kukiangusha Chama? Hivi nipo curious, mmejipanga vipi na kiasi gani ili muweze kujua kama hio sio mbinu ya the so called adui kuhakikisha kuwa mnasambaratika kwa baadhi ya viongozi Chadema waonekane hawafai? Hivi huo uchunguzi huwa mnaufanya kwa muda wa kutosha na matokeo ya kuridhisha?
The way huwa wanahandle masuala yao ndiyo moja ya dhaifu kubwa lililopelekea ‘Ubovu' ambao kama hatua haitachukuliwa mapema kwa ku estimate huo ubovu itawa cost parefu. Kuwepo kwa makundi ndani ya Chama ni suala ambalo lilikuwa lipo wazi ila lilikosa ile uwazi wa huo mgawanyiko ambao kwa sasa umeshaoneshwa wazi tokana na tamko la BAVICHA.
Kufukuza wanachama huwa mnafanya kwa mikeke sana na kwa namna ya kuwadhalilisha (that's my IMO); kumbuka hao wanaofukuzwa pamoja na kwamba wapo considered as wasaliti – wanakuwa wametoka katika nafasi ambazo wanaijua vema CDM… Na wote twajua mtu wa kukumaliza vilivyo ni Yule wa karibu wao.
STRATEGIES za CDM kuwasimimisha hao viongozi ni kweli zinawaongezea sifa kubwa saana kuwa ni wawajibikaji na hawamchekei mtu… Ila inaleta matatizo matatizo makubwa ndani ya Chama, matatizo ambayo huwapotezea muda kuweka sawa na kuwatoa katika njia ya ku focus namna ya kujidhatiti na kuhakikisha ushindi… Wanaongeza idadi ya maadui wenye nguvu sana;
Kumbuka kuwa kuna tofauti ya kuongeza adui na kuongeza adui mwenye nguvu dhidi yako na mbaya kuliko ni kuwa wanazidi expose weakness zao na vile vile kuzidi kuelemewa hasa watumiwapo kwa ajili ya malengo ya propaganda ambazo zinaendeshwa dhidi yao… Kwa kweli CDM inatakiwa mjipange vilivyo sababu ni wazi kuwa iko targeted nje na ndani ya chama. Hio ni wrong timing kwa Chama, perfect timing kwa maadui.