POINT OF NOTICE: CHADEMA wakija na tamko jingine refu..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Kamati Kuu ya CHADEMA inapokutana katika siku hizi mbili ikitoka na tamko jingine la kuiomba serikali au kuitaka serikali ifanye a, b na c utakuwa ugomvi.

Ije na muongozo kwa viongozi wake, iweke mwelekeo wa wazi wa mabadiliko ndani ya chama, na ikamilishe nidhamu. CDM haiwezi kwenda katika uchaguzi mkuu wa 2015 au wa serikali za mitaa wa 2014 ikiwa na migawanyiko ya ajabu na ikiendeleza siasa za kucheza zero distance na CCM.

Wasipokuja na mwelekeo mzuri wa kujenga chama na kukiimarisha na mwitikio wa kisera dhidi ya mashambulizi ya CCM kuna watu itabidi tuwaite wajiuzulu nafasi zao CDM.

Imetosha kutoa matamko yenye malalamishi na yenye kutujulisha kitu ambacho karibu wote tunakijua. Tunataka tuone CDM ikianzisha mabadiliko ya ndani ya muundo wake ili kiweze kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu...
 
Kamati Kuu ya CHADEMA inapokutana katika siku hizi mbili ikitoka na tamko jingine la kuiomba serikali au kuitaka serikali ifanye a, b na c utakuwa ugomvi. Ije na muongozo kwa viongozi wake, iweke mwelekeo wa wazi wa mabadiliko ndani ya chama, na ikamilishe nidhamu. CDM haiwezi kwenda katika uchaguzi mkuu wa 2015 au wa serikali za mitaa wa 2014 ikiwa na migawanyiko ya ajabu na ikiendeleza siasa za kucheza zero distance na CCM. Wasipokuja na mwelekeo mzuri wa kujenga chama na kukiimarisha na mwitikio wa kisera dhidi ya mashambulizi ya CCM kuna watu itabidi tuwaite wajiuzulu nafasi zao CDM.

Imetosha kutoa matamko yenye malalamishi na yenye kutujulisha kitu ambacho karibu wote tunakijua. Tunataka tuone CDM ikianzisha mabadiliko ya ndani ya muundo wake ili kiweze kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu...

Mkuu tatizo la wapenzi, wanamahaba na wanazi wa CDM ni kufukia kichwa kwenye mchanga kama mbuni huku mwili mzima uko nje. Hawataki kusikia maneno ambayo yatawasaidia kujiimarisha. Wapenzi wa CDM wanaona lango la ikulu eti liko wazi hivyo wao wako kwenye mbio za kuingia hata kama wataingia wakiwa vipande. Hawajipangi kuingia kwa murua na kwa papara hiyo mwisho watafika mmoja mmoja na kukuta lango limefungwa na itabidi wasubiri tena hadi 2020, Insh'Allah.

Nakala TUMBIRI Ritz Molemo Ben Saanane OSOKONI Mwita Maranya
 
Last edited by a moderator:
Kamati Kuu ya CHADEMA inapokutana katika siku hizi mbili ikitoka na tamko jingine la kuiomba serikali au kuitaka serikali ifanye a, b na c utakuwa ugomvi.

Ije na muongozo kwa viongozi wake, iweke mwelekeo wa wazi wa mabadiliko ndani ya chama, na ikamilishe nidhamu. CDM haiwezi kwenda katika uchaguzi mkuu wa 2015 au wa serikali za mitaa wa 2014 ikiwa na migawanyiko ya ajabu na ikiendeleza siasa za kucheza zero distance na CCM.

Wasipokuja na mwelekeo mzuri wa kujenga chama na kukiimarisha na mwitikio wa kisera dhidi ya mashambulizi ya CCM kuna watu itabidi tuwaite wajiuzulu nafasi zao CDM.

Imetosha kutoa matamko yenye malalamishi na yenye kutujulisha kitu ambacho karibu wote tunakijua. Tunataka tuone CDM ikianzisha mabadiliko ya ndani ya muundo wake ili kiweze kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu.......

Mzee Mwanakijiji,ninakuunga mkono kwa asilimia mia moja.Imefika mahali sasa ni lazima yachukuliwe maamuzi mazito sana.Ni lazima nidhamu ndani ya chama iheshimiwe.

Binafsi yangu na nitaomba wengine waunge mkono ni Lazima sasa wahuni na waasi wote wafukuzwe chamani.
Waasi wote na wanaoendekeza uhuni wanajulikana na majina yao yote yapo mbele ya Kamati kuu leo.

Tunataka wote wafukuzwe na niseme bila kuuma maneno TUMECHOKA!
 
Mkuu tatizo la wapenzi, wanamahaba na wanazi wa CDM ni kufukia kichwa kwenye mchanga kama mbuni huku mwili mzima uko nje. Hawataki kusikia maneno ambayo yatawasaidia kujiimarisha. Wapenzi wa CDM wanaona lango la ikulu eti liko wazi hivyo wao wako kwenye mbio za kuingia hata kama wataingia wakiwa vipande. Hawajipangi kuingia kwa murua na kwa papara hiyo mwisho watafika mmoja mmoja na kukuta lango limefungwa na itabidi wasubiri tena hadi 2020, Insh'Allah.

Nakala TUMBIRI Ritz Molemo Ben Saanane OSOKONI Mwita Maranya.........

Kimbunga siamini kama umefurahishwa na alichosema Mwanakijiji.Nina uhakika ulitaka aseme kingine.
 
Mzee Mwanakijiji,ninakuunga mkono kwa asilimia mia moja.Imefika mahali sasa ni lazima yachukuliwe maamuzi mazito sana.Ni lazima nidhamu ndani ya chama iheshimiwe.

Binafsi yangu na nitaomba wengine waunge mkono ni Lazima sasa wahuni na waasi wote wafukuzwe chamani.
Waasi wote na wanaoendekeza uhuni wanajulikana na majina yao yote yapo mbele ya Kamati kuu leo.

Tunataka wote wafukuzwe na niseme bila kuuma maneno TUMECHOKA!
Kwa hiyo mkuu Molemo leo kuna kufukuzana kwenye chama? Angalieni yasije kuwapata yaliyotupata kule Tanga. Masula ya kufukuza kwenye chama mara nyingi huwa hayajengi hasa mnapofukuzana kwa hisia tu kwamba huyu kapewa pesa na CCM ili kukivuruga chama. Huenda kikulacho ki nguoni mwako manake wengine walichaguliwa na wana CDM hivyo wana wapambe na wanazi wengi tu.

Kimbunga siamini kama umefurahishwa na alichosema Mwanakijiji.Nina uhakika ulitaka aseme kingine.

Mkuu Molemo ushauri wa Mwanakijiji ni mzuri lakini ninyi hamtaki kusikia kwamba kuna migawanyiko ndani ya CDM.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Molemo ushauri wa Mwanakijiji ni mzuri lakini ninyi hamtaki kusikia kwamba kuna migawanyiko ndani ya CDM.

Kimbunga acha kuvuruga mada ya Mwanakijiji kwa makusudi kwa sababu unakesha kuvuruga mada zote za Chadema kwa malengo unayoyajua wewe.Lakini mmechemsha.
 
Last edited by a moderator:
Kimbunga siamini kama umefurahishwa na alichosema Mwanakijiji.Nina uhakika ulitaka aseme kingine.
Haya sasa wewe muingizie maneno ya kuwapamba viongozi wako wanaopotoka kila kukicha kwa kuja na hoja nyepesi,mikakati isiyotekelezeka,uzandiki,maneno ya hovyo hovyo katika majukwaa ya siasa lakini bado mnawaona watakatifu.
 
Kimbunga acha kuvuruga mada ya Mwanakijiji kwa makusudi kwa sababu unakesha kuvuruga mada zote za Chadema kwa malengo unayoyajua wewe.Lakini mmechemsha.

Haya Molemo nanyamaza watakuja wengine nao wachangie. Nitarudi baadaye ngoja nikatafute chochote ili watoto wacheke na wenzao tarehe 25 na kisha mwezi wa kwanza waende shule.
 
Last edited by a moderator:
Mleta hoja nakuunga mkono; lakini labda nikuombe kitu kimoja unaweza kufafanua ni mabadiliko yapi yafanyike ndani ya CDM? Binafsi naamini sera za CDM ni nzuri sana na ndo maana hata CCM wanaanza kuzifuatilia kinyemela ili kuzifanyia kazi. Tatizo kubwa ni kwamba CCM ina watu wenye pesa ambao kwao kuhonga watu na kuwapandikiza ndani ya CDM ili wavuruge wale wenye malengo mema ni mkakati endelevu. Na kuwatambua inakuwa vigumu kwa kuwa CDM bado ni changa. Baada ya uchaguzi wa 2010 baadhi ya waliopandikizwa tayari wameishabainika na ndo hao hao sasa wanaoendeleza marumbano kuwa CDM ina mapungufu.

Tuwe makini sana na hao watu na tutumie muda mwingi kufuatilia nyendo zao. Bahati nzuri baadhi ya wana JF mitaani hawajulikani kama ni wanachama wa CDM au la! Na hao ndo wanaweza kutumika kuleta habari za uhakika hapa tofauti na wale ambao wanafahamika na wanatetea maslahi yao binafsi.
 
Kamati Kuu ya CHADEMA inapokutana katika siku hizi mbili ikitoka na tamko jingine la kuiomba serikali au kuitaka serikali ifanye a, b na c utakuwa ugomvi.

Ije na muongozo kwa viongozi wake, iweke mwelekeo wa wazi wa mabadiliko ndani ya chama, na ikamilishe nidhamu. CDM haiwezi kwenda katika uchaguzi mkuu wa 2015 au wa serikali za mitaa wa 2014 ikiwa na migawanyiko ya ajabu na ikiendeleza siasa za kucheza zero distance na CCM.

Wasipokuja na mwelekeo mzuri wa kujenga chama na kukiimarisha na mwitikio wa kisera dhidi ya mashambulizi ya CCM kuna watu itabidi tuwaite wajiuzulu nafasi zao CDM.

Imetosha kutoa matamko yenye malalamishi na yenye kutujulisha kitu ambacho karibu wote tunakijua. Tunataka tuone CDM ikianzisha mabadiliko ya ndani ya muundo wake ili kiweze kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu...

Mwanakijiji,I concur with you sir.Its time for CDM to sack all Traitors and put them in dustbin.
Inatakiwa CDM kiwe na msimamo mkali dhidi ya hayawani wote wa kisiasa.Eti mwendawazimu mmoja anaibuka na kusema tena hadharani Dr Slaa afukuzwe....Its Shame,very Shame! Halafu CDM ichekelee malaya wa kisiasa kama huyu?
 
Last edited by a moderator:
Kumfukuza mwanachama kwa kutofautiana katika maamuzi au misimamo ni kubaka demokrasia,wanachama wote wanahaki sawa katika kutoa maoni na kusikilizwa.Kwa kiongozi kutumia nafasi yake kufukuza watu ni dalili tosha uwezo wa kuongoza watu ni mdogo.
 
Tutashuhudia coment za kuunga mkono hii thread kwa vile ni Mwanakijiji kaiweka,angeiweka mwingine hapa mitusi ingekuwa kibao.Mwanakijiji umenena vema kweli inatakiwa viongozi wa CDM kutafakari sana juu ya mambo yanayojitokeza ndani ya chama ambayo yanahitaji ufafanuzi,bila kusahau katibu kumiliki kadi ya chama pinzani,matamko mbalimbali ya vijana wa CDM kutaka baadhi ya viongozi wang'oke katika nafasi zao za uongozi pia na tathimini ya matamko mbalimbali yanayotolewa na chma kama yanaleta ufanisi au yanaishia midomoni tu.Wenye masikio na akili watasikiliza ushauri uliotoa mkuu.
 
Moja ya madhaifu makubwa ya Chadema ni kuchelewa kwao kuchukua maamuzi katika masuala yaliyo waathiri kutoka nje ya Chama na hasa kama yapo ki-Propaganda. Chadema wapo haraka saana kucukua maamuzi ya haraka saana pale ambapo imewagusa moja kwa moja toka humo humo chamani na hasa kama hayo makosa yanagusa mahala/mtu nyeti hasa kimaslahi ya Chama ama yale yamefanywa kwa makusudi kwa malengo ambayo yanapelekea image mbaya.

Pamoja na u-haraka wao wa kuhandle na kurekebisha yale ambayo yanagusa chama moja kwa moja ni ajabu sana kuwa wamelifumbia macho suala ala makundi yaliyowazi ndani ya chama hadi hapa yalipofika kwa BAVICHA kudiriki kutoa tamko dhidi ya Dr. Slaa. Swali kubwa la kujiuliza hivi Chadema wana taratibu zianzofuata protocol ama kiongozi yeyote anaweza toa maamuzi ili mradi yupo na idara yake?

Makundi kwa Chama kichanga kama Chadema ni sumu na kabisa lisipotatuliwa ndipo hasa namna pekee ya kuimaliza Chadema. Kila mtu anajua athari za ‘divide and rule policy' ni most effective kwa maadui, huku wahusika pande zote kujiona wapo superior kuliko wenzao na hali kwa adui haijalishi kikubwa mjigawe na mjichukie.

Binafsi yangu na nitaomba wengine waunge mkono ni Lazima sasa wahuni na waasi wote wafukuzwe chamani. Waasi wote na wanaoendekeza uhuni wanajulikana na majina yao yote yapo mbele ya Kamati kuu leo.

Tunataka wote wafukuzwe na niseme bila kuuma maneno TUMECHOKA!

Mkuu Molemo,

Hapa ndipo mnapotakiwa umakini... Nyie si mlishasema kuwa Chadema ina maadui sana kiasi kwamba hao maadui wapo tayari kufanya lolote kwa ajili ya kukiangusha Chama? Hivi nipo curious, mmejipanga vipi na kiasi gani ili muweze kujua kama hio sio mbinu ya the so called adui kuhakikisha kuwa mnasambaratika kwa baadhi ya viongozi Chadema waonekane hawafai? Hivi huo uchunguzi huwa mnaufanya kwa muda wa kutosha na matokeo ya kuridhisha?

The way huwa wanahandle masuala yao ndiyo moja ya dhaifu kubwa lililopelekea ‘Ubovu' ambao kama hatua haitachukuliwa mapema kwa ku estimate huo ubovu itawa cost parefu. Kuwepo kwa makundi ndani ya Chama ni suala ambalo lilikuwa lipo wazi ila lilikosa ile uwazi wa huo mgawanyiko ambao kwa sasa umeshaoneshwa wazi tokana na tamko la BAVICHA.

Kufukuza wanachama huwa mnafanya kwa mikeke sana na kwa namna ya kuwadhalilisha (that's my IMO); kumbuka hao wanaofukuzwa pamoja na kwamba wapo considered as wasaliti – wanakuwa wametoka katika nafasi ambazo wanaijua vema CDM… Na wote twajua mtu wa kukumaliza vilivyo ni Yule wa karibu wao.

STRATEGIES za CDM kuwasimimisha hao viongozi ni kweli zinawaongezea sifa kubwa saana kuwa ni wawajibikaji na hawamchekei mtu… Ila inaleta matatizo matatizo makubwa ndani ya Chama, matatizo ambayo huwapotezea muda kuweka sawa na kuwatoa katika njia ya ku focus namna ya kujidhatiti na kuhakikisha ushindi… Wanaongeza idadi ya maadui wenye nguvu sana;

Kumbuka kuwa kuna tofauti ya kuongeza adui na kuongeza adui mwenye nguvu dhidi yako na mbaya kuliko ni kuwa wanazidi expose weakness zao na vile vile kuzidi kuelemewa hasa watumiwapo kwa ajili ya malengo ya propaganda ambazo zinaendeshwa dhidi yao… Kwa kweli CDM inatakiwa mjipange vilivyo sababu ni wazi kuwa iko targeted nje na ndani ya chama. Hio ni wrong timing kwa Chama, perfect timing kwa maadui.
 
huwezi kwenda vitani huku risasi zenu mnarushiana wenyewe mwisho mtakosa watu wa kwenda vitani wote watakuwa wameuana kwa "friendly fire". They need to do it now or else.. tumewabembeleza sana na kuwalilia na kama kuwashauri imetosha.
 
Kumfukuza mwanachama kwa kutofautiana katika maamuzi au misimamo ni kubaka demokrasia,wanachama wote wanahaki sawa katika kutoa maoni na kusikilizwa.Kwa kiongozi kutumia nafasi yake kufukuza watu ni dalili tosha uwezo wa kuongoza watu ni mdogo.
Vipi Mnataka tuajiri katibu Mkuu wa kisomali kama nyinyi?
 
Kamati Kuu ya CHADEMA inapokutana katika siku hizi mbili ikitoka na tamko jingine la kuiomba serikali au kuitaka serikali ifanye a, b na c utakuwa ugomvi.

Ije na muongozo kwa viongozi wake, iweke mwelekeo wa wazi wa mabadiliko ndani ya chama, na ikamilishe nidhamu. CDM haiwezi kwenda katika uchaguzi mkuu wa 2015 au wa serikali za mitaa wa 2014 ikiwa na migawanyiko ya ajabu na ikiendeleza siasa za kucheza zero distance na CCM.

Wasipokuja na mwelekeo mzuri wa kujenga chama na kukiimarisha na mwitikio wa kisera dhidi ya mashambulizi ya CCM kuna watu itabidi tuwaite wajiuzulu nafasi zao CDM.

Imetosha kutoa matamko yenye malalamishi na yenye kutujulisha kitu ambacho karibu wote tunakijua. Tunataka tuone CDM ikianzisha mabadiliko ya ndani ya muundo wake ili kiweze kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu...

Asante sana Mkuu kwa mada yako nzuri.Inatakiwa CDM wawape watanzania zawadi ya Xmass kwa kufukuza waasi wote.
Nina imani mnawajua waasi wote kwa sababu mkuu Molemo amesema majina yao yapo mbele ya Kamati kuu.
Mimi nitasaidia kuwataja ninaowajua wanaoongoza huo uasi.Kuna Mtela Mwampamba,Habib Mchange,Juliana shonza,Eddo Mwamalala na anayejiita Katibu wa Bavicha Mwanza.
 
Last edited by a moderator:
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom