Point Blank: Tumekosea! Tuanze Upya!

Point Blank: Tumekosea! Tuanze Upya!

Joined
Jul 3, 2018
Posts
76
Reaction score
130
Katika jamii ya watu wenye ustaarabu na wanaoelekea kwenye ustaarabu kukubali kukosea ni jambo la kheri. Kamwe, kukosea hakumaanishi mwenye kufanya kosa hajui anachokifanya na si kwamba hajui kwa sababu hana uwezo wa kujua anachokifanya, lahasha! Pengine ni mbinu tu anayoitumia mhusika katika kutenda jambo fulani au kukamilisha mpango fulani unakuwa siyo sahihi ukilinganisha na kama angetumia mbinu nyingine.

Kukosea ni sehemu ya maisha ya binadamu, muhimu ni kiwango cha kukosea (kawaida, kati au sana). Kila tunapotekeleza majukumu yetu tunakumbana na mambo mengi ambayo kwayo tunajikuta tumekosea na ikibidi tunajirekebisha au tunapuuzia tu; hasa ikiwa madhara ya makosa yetu ni ''minimal''. Lakini, ikiwa madhara tarajiwa yaweza kuathiri mtiririko mzuri wa kinachofanyika ukiunganisha na kilichokuwepo, basi ni budi kujitafakari na kurudi kwenye njia sahihi.

Ninawapongeza, viongozi, mashabiki na wachezaji wa klabu ya Simba Ivory Coast kwa kufanya uchaguzi wa viongozi wao wa juu chini ya mfumo mpya wa umiliki wa timu, kwa amani na ufanisi mkubwa. Ni kipindi kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu sana, lakini pia kulikuwa na ''tension'' kubwa kwa pande zote; yaani, wagombea, wachezaji na mashabiki kwa upande mmoja na serikali kwa upande mwingine kama mdau muhimu wa michezo na ulinzi wa amani.

Viongozi wameshapatikana, kilichobaki sasa ni kuchapa kazi kwa kuzingatia sheria za soka za kimataifa (FIFA), sheria za nchi, sheria za TFF, kanuni na taratibu zenu za ndani ya klabu. Kamwe msiendekeze migogoro, hata ikitokea tumieni njia bora zausuluhishi wa ndani kwa ndani ili kuifikisha klabu yenu pendwa juu zaidi kwenye mafanikio.
Hekima na busara hutoka kwa Mungu, hakuna mwanadamu anayeweza kuwagaiwieni au kuwafanya mwe na hekima bali ni Mola pekee. Basi ombeni hekima iliyo ya kweli ili mkatekeleze majukumu yenu kwa ufanisi na haki.
Zingatieni, mchezo wa mpira wa miguu ndio pekee wenye kuwapa furaha wapenzi na mashabiki wa soka.

Kwenu Klabu ya Yanga (The senior football club ever), mnacho kibarua mbele yenu cha kuinusuru timu yenu na anguko la uongozi. Aminini ya kuwa viongozi wazuri wapo ndani yenu wenyewe, tafakarini kwa dhati mpate viongozi watakaoifanya timu iwaburudishe mashabiki na wafuasi wadau wa soka ili kusaidia kuwaongezea siku za kuishi. Furaha huzidisha siku za kuishi bali huzuni hufupisha maisha yetu. Kumbuka Mungu hakutuumbia huzuni bali furaha na ndio maana katika uumbaji wake alifanya kila alichodhani kitamfanya mwanadamu aishi kwa amani na furaha pasipo kukengeuka.


Kila mwanadamu alipewa mamlaka kamili ya kujitawala chini ya uangalizi wa muumba na ndio maana ni Mungu tu aliyekuwa na uwezo wa kupatikana kwa viongozi watii kwake, waadilifu, wapenzi, wenye rehema kwa watu wao n.k. Ikitokea akashika nafasi ya uongozi mtu ambaye hakuwa chaguo la Mungu, aliisababishia shida jamii yake. Wanajangwani wa Nyasaland mshirikisheni Mungu kuwapata viongozi ambao klabu itawakubali.
Good day! JF Home of Great Thinkers!

 
Nimeona thread ipo jukwaa la siasa nikaanza kusoma nikajua itakua inamhusu jiwe na DAB lakini mwisho thread ikaelekea kwenye mambo ya Simba Sc na Vyura Sc.

Content imeeleweka lakini, asante mkuu.
 
Nimeona thread ipo jukwaa la siasa nikaanza kusoma nikajua itakua inamhusu jiwe na DAB lakini mwisho thread ikaelekea kwenye mambo ya Simba Sc na Vyura Sc.

Content imeeleweka lakini, asante mkuu.
Afadhali umenisaidia kuiacha ilivyo, kwanza vitu aina hii halafu virefu huwa napita zangu.
 
Nikikuta mke wangu Nuru anasoma mada kama hii nampa taraka tatu. Nyambafu kabisa.
 
peleka jukwaa la mpira bwana sisi tuko bize na makonda na EU wanaotaka tu-Ambaruttiane
 
Back
Top Bottom