Sikwangalasyene
Member
- Jul 3, 2018
- 76
- 130
Kukataa sifa ya udhaifu hadharani ni kukiri kuwa u dhaifu pasipo mdhaifu kujua. Yamkini, ni kwa bahati mbaya mtu mmoja au taasisi moja yaweza kuona mambo au viashiria vya utendaji hafifu vya mtu au taasisi nyingine na kujiridhisha kwamba tatizo ni udhaifu (incapacity) kitabia, kiutendaji, kimfumo au kimwenendo kwa ujumla. Kama ndivyo, busara zinaelekeza mlengwa wa udhaifu anakuwa amesaidiwa kwa sababu anakuwa amepata fursa ya kujichunguza ili kuona udhaifu wake upo katika nyanja zipi za maisha yake au utendaji wake au wa taasisi yake. Ni fursa nzuri ya kufanya marekebisho.
Ikiwa mtu au taasisi iwayo yote itabainika ina udhaifu na kisha mtu au mkuu wa taasisi mwenye dhamana akaukataa udhaifu tena kwa nguvu kubwa na mihemko ni dhahiri MTU AU TAASISI HIYO INAKUWA IMETHIBITISHA KUWA NI DHAIFU BILA SHAKA. Naam! Kuukataa udhaifu ni udhaifu wenyewe! Tena kwenye media kunafanya hata wale ambao walikuwa hawakujui kuwa ni dhaifu kiasi gani wanakujua vema.
Weakness is just weakness it can never be treated as an offence anyway!
I stand to be corrected (This is my weakness).