PMs wote walitaka urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PMs wote walitaka urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nsololi, Sep 19, 2009.

 1. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Just in case kuna mtu atakuwa interested na makala haya ya Jenerali Ulimwengu

  Rai ya Jenerali


  Salim, Msuya, Warioba, Malecela, Sumaye? wote walitaka urais  Jenerali Ulimwengu
  Septemba 16, 2009


  NIMEJARIBU, kwa makala mbili za hivi karibuni, kuonyesha ni jinsi gani ofisi mbili kuu katika nchi zinavyoweza kuzaa migongano isiyokuwa ya lazima iwapo hazikuwekewa mipangilio inayoeleweka na iwapo watu wawili wanaoziendesha hawajengi mahusiano ya ‘kuiva.’
  Wiki jana nilidokeza kwamba baadhi ya matatizo yanayoweza kujitokeza kutokana na ofisi hizo kutoratibiwa vyema tumekwisha kuyashuhudia hapa nchini, hata kama hatupendi kuyajadili kinagaubaga. Muhimu ni kujua kiini cha tatizo, na kujua kwamba linaweza kujitokeza tena katika mazingira kama yale tuliyokwisha kuyashuhudia, hata kama wahusika watakuwa ni watu wengine, alimradi tatizo halijaondolewa.
  Itatusaidia sana, na itatupa manufaa iwapo tutajifunza kama Taifa kujenga mifumo, kusimika asasi na kusimamia michakato inayotokana na tafakuri pevu iliyosomeshwa na uzoefu wetu uliochanganyika na yale tuliyojifunza kutoka vitabuni na kutoka kwa binadamu wenzetu na mataifa ya wenzetu tangu Alfajiri ya Historia.
  Hii ina maana ya kufanya mambo kadhaa, mojawapo likiwa ni kujifunza kwa dhati na kwa bidii historia yetu ya kisiasa, kikatiba na kiutawala.
  Inawezekana siwatendei haki baadhi ya wanasiasa ninaokutana nao, lakini napata hisia kwamba wengi wao hawajishughulishi kuijua vyema historia hiyo na kuchota mafunzo maridhawa yaliyomo ndani yake.
  Iwapo historia ya nchi yao wenyewe hawaijui, na wala hawana ari yo yote ya kuitafiti, seuse kuwaambia waende wakachimbe historia za nchi nyingine na mataifa wasiyokuwa na nasaba nayo?
  Matokeo yake ni kwamba kila mara tunawasikia wanasiasa uchwara wakipiga domo kuhusu mambo ambayo, kwa hakika, hawayaelewi vyema, na matokeo yake wanatengeneza joto zaidi kuliko mwanga.
  Hata hivyo ukweli ni kwamba hatuna budi kujifunza yote haya, kwanza historia yetu na uzoefu tunaopata kutokana nayo, na pili historia za wenzetu na uzoefu tunaoweza kupata kutokana nayo.
  Weledi wa masuala ya nyumbani ni mzuri na unasaidia, lakini hauna lazima yo yote ya kuandamana na ‘ushamba’ kuhusu masuala ya binadamu wenzetu duniani kote, na kupitia vipindi vyote vya historia.
  Jambo jingine ambalo tunahitaji kujifunza ni kujizuia kuweka misingi ya utawala kwa kuangalia watu waliomo madarakani hivi leo na kutengeneza misingi ya utawala wetu kwa kujali zaidi ni nini wanataka hao tulio nao leo badala ya kujenga upeo wa kuangalia ni nini kitahitajika na Taifa letu, kadri litakavyokuwa likikua na kubadilika, miongo na hata karne kadhaa zijazo.
  Hii ina maana pia kwamba tunatakiwa kuacha kufikiria masuala yanayohusu mustakabali wa Taifa kwa kumuangalia yule aliye madarakani kwa sasa na kumtengenezea katiba tunayodhani inamfaa, au katiba anayoitaka yeye mwenyewe. Ukweli ni kwamba hatakuwapo siku zote, na kila mara tutalazimika kufanya mabadiliko ili kuifanya katiba ifanane na huyo aliye madarakani kwa wakati huo, ambao ni upuuzi.
  Tumeyaona haya zama za Nyerere. Ofisi ya waziri mkuu imechukua sura ya kubadilika mara kwa mara tangu Tanganyika iwe huru kwa sababu Mwalimu Nyerere alitaka kuwa na mpangilio wa kikatiba ambao ungempa uwanja wa kisiasa na kiutawala wa kufanya kile alichokitaka (kujenga Taifa la nchi changa masikini kuleta maendeleo ya haraka) bila kukwazwa na malumbano “yasiyoisha.”
  Kuasisiwa kwa Ofisi ya Rais na kufutwa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka mmoja baada ya Uhuru ulikuwa ndio mwanzo wa kuziweka ofisi hizi mbili katika mizani iliyobadilisha uwiano mara kwa mara baina ya sahani ya uzito na ile ya bidhaa, kiasi kwamba Esward Sokoine kama waziri mkuu wa Julius Nyerere hakuwa sawa na Joseph Warioba kama waziri mkuu wa Ali Hassan Mwinyi, wala Frederick Sumaye, chini ya Benjamin Mkapa, hakufanana kabisa na Edward Lowassa akiwa waziri mkuu wa Jakaya Kikwete.
  (Nadiriki kusema kwamba Mizengo Pinda atajaribu kwa uwezo wake wote kuwa tofauti kabisa na Lowassa.)
  Nakubali kwamba kila anayeshika ofisi anakuwa kapewa nafasi ya kuitumia ofisi hiyo kujenga himaya yake kwa kadri ya uwezo wake, na kwamba nguvu ya ofisi chini ya Mkuu A si sawa na nguvu ya ofisi hiyo hiyo chini ya Mkuu B. Kila mmoja huja na mbwembwe zake na viwango vya nishati na msukumo vitakavyomfanya atofautiane na yule aliyemtangulia na yule atakayemrithi.
  Hata hivyo, ni lazima masuala ya msingi yawekewe mipangilio, kanuni, taratibu na mizingo ili kuweka tofauti kati ya maudhui ya msingi ya ofisi na mbwembwe anazokuja nazo huyo anayeishika ofisi hiyo kwa kipindi fulani, na hayo maudhui ya msingi yasitegemee ‘kuiva’ au ‘kutoiva’ kwa washika ofisi wawili, kati ya rais na waziri mkuu.
  Kwangu mimi hili ni suala muhimu kwa sababu napenda kuzingatia ukweli kwamba hali yetu ya kisiasa imebadilika mno tangu wakati Nyerere alipokuwa akifanya majaribio ya kukasimu madaraka fulani fulani kwa mtu aliyemwita waziri mkuu.
  Mambo yamebadilika kiasi kwamba ye yote anayejaribu kuiga alichokuwa akifanya Nyerere bila kuangalia mazingira mapya atakuwa anajidanganya na wala hatapata mafanikio yo yote ya maana.
  Katika miaka ya mwanzo ya 1990, nikimsihi Mwalimu asaidie kuweka misingi ya kikatiba itakayotuongoza wakati yeye atakapokuwa hayupo, nilimwambia kwamba tofauti na Watanzania wengi walivyoamini kwamba Mwalimu alikuwa ni sehemu ya Katiba ya Tanzania, mimi nilikuwa naamini kwamba Katiba ya Tanzania ilikuwa ni sehemu ya Mwalimu.
  Katika masuala mengi, hususan yale aliyoyaona kama ya msingi katika uendeshaji wa nchi, alichokitaka Mwalimu ndicho kilichokuwa.
  Alipotaka asiwepo waziri mikuu, ikawa; alipotaka awepo waziri mkuu (mwaka 1977, nashuku wakati alipojiona anaanza kuchoka na anahitaji msaidizi), akamtengeneza; aliyempa ofisi hiyo akajiuzulu muda mfupi baadaye kwenda kupata ‘matibabu’ na aliporudi akamrudishia ofisi; alipofariki katika ajali Mwalimu akasema hadharani kwamba alikuwa akitumai kwamba huyo ndiye angekuwa mrithi wake (wakati alimteua Sokoine akiwa tayari ana makamu wa rais na rais wa Zanzibar, Aboud Jumbe).
  Kama tunakumbuka tamko la Mwalimu, kwamba kama Sokoine angeishi ndiye alikuwa anatarajiwa kuwa mrithi wa Mwalimu (si kutokana na kikao cho chote cha CCM bali uamuzi wa Mwalimu mwenyewe, bila kumshirikisha mtu), tujiulize iwapo Mwalimu alikusudia kwa wakati ule kuitumia ofisi ya waziri mkuu kama kituo cha mazoezi kwa mtu ambaye baadaye angekuwa rais?
  Jibu ni kwamba mwanzoni mwa mwaka 1984 kulitokea kile kilichoelezwa kama “kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa visiwani Zanzibar,” hali iliyomwondoa Jumbe madarakani kama Rais wa Zanizibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
  Kwa hiyo wakati wa kifo cha Sokoine, Jumbe alikuwa hayuko madarakani tena. Lakini alikuwapo makamu mpya, Ali Hassan Mwinyi, ambaye, kwa mantiki fulani, angetakiwa kuwa ndiye mrithi wa Mwalimu.
  Hata hivyo, uteuzi wa Salim kama waziri mkuu mara baada ya kifo cha Sokoine unaimarisha wazo kwamba ofisi hiyo alitaka kuitumia kama ofisi ya mafunzo kwa rais ajaye, kwani miezi 18 baadaye alimtaka Salim amrithi, utashi ambao haukutimia.
  Haishangazi, basi, kwamba tangu Sokoine ashike nafasi ya waziri mkuu kama sehemu ya maandalizi yake kabla ya kumrithi Nyerere, kila Mtanzania aliyewahi kuwa waziri mkuu (isipokuwa Kawawa) hatimaye alitaka kuwa rais, ingawaje hata hivyo hakuna hata mmoja aliyefanikiwa katika dhamira yake hiyo:
  Cleopa Msuya, Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba, John Malecela na Frederick Sumaye, kwa nyakati tofauti, wote wamejaribu kuwania urais wa Tanzania. Suala la kujiuliza ni: Kwa nini?
  Bila shaka ukweli kwamba Nyerere alikuwa ameitengeneza ofisi hiyo kama mahali pa mrithi wake wa baadaye kujiandaa umechangia hali hiyo, na kila waziri mkuu aliyeteuliwa alijiona kama Sokoine mwingine, kosa wanalofanya wale wanaodhani alichofanya Nyerere zama hizo kinaweza kufanyika tena leo.
  Ukweli mwingine ni kwamba waziri mkuu ndiye msaidizi mkuu wa rais kwa upande wa Tanganyika. (Visiwani hana madaraka yo yote, suala nitakalolijadili baadaye).
  Kwa kuwa kadri tunavyozidi kukomaa katika mfumo wa vyama vingi ndivyo itakavyokuwa vigumu kwa rais kutoka Visiwani, waziri mkuu anajitokeza kama nambari mbili kwa rais ingawaje yuko makamu wa rais, ambaye kikatiba ndiye nambari mbili (hili nalo linazua tatizo nitakalolijadili).
  Kwa maana hiyo, kama hili ninalolisema ni kweli, na kwa kuwa tumeona kila aliyewahi kuwa waziri mkuu ametaka pia kuwa rais, je inashangaza kwamba mtu ye yote atakayeteuliwa na rais na kuthibitishwa na bunge kuwa waziri mkuu atakuwa na ndoto za kuwa rais?
  Kama ni kweli atakuwa na njozi hizo, je, anaweza bado kufanya kazi chini ya rais mtendaji na bado wakaelewana?
  Inaendelea


   

  Attached Files:

 2. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
 3. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ni kweli waziri Mkuu woote waliopita walitaka urais kwa nyakati tofauti isipokuwa mzee RASHID KAWAWA. Hatujui itakuwaje kwa mzee Mizengo PINDA.
   
 4. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Lakini mi naona Pinda siasa zimemkalia kushoto, aligombea ubunge apate sehemu ya kula tu sio hasa kuingia kwenye pilika za siasa....!
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ongeza tu kwenye kibwa cha habari kwamba hata Nyerere mwenyewe aliwahi kuwa waziri mkuu kabla ya kuwa Rais.
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ningekuwa na uwezo, ningeweka limit kwamba ukishapata nafasi ya waziri mkuu, hauruhusiwi kugombea urais.

  Maana yangu ni kwamba nina mashaka kwamba huenda kuna conflict of interest na kwamba waziri mkuu anaweza asitende kazi zake vizuri especially anapokuwa pia anataka urais.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  naona we umemulewa jenerali...
   
 8. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Salim, Msuya, Warioba, Malecela, Sumaye na "LOWASA" AMBAYE BADO ANATAKA
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  To be more precise ambaye watanzania hatumtaki.
   
 10. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kama wewe humtaki ni mawazoo yakoooo...
   
 11. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani wao siyo raia wa nchi hii ?????? Kama na wewe unataka si ugombee tu halafu upate kura yako tu moja bila hata ya mwandani wako kuliko kulalama.
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kama tunaye MAKAMU wa RAIS, cheo hiki cha WAZIRI MKUU ni cha nini hasa? Mapesa yayotumika kuiendesha ofisi hii kwa mwaka mmoja yangetosha kabisa kununua madawati kwa shule zetu zote za msingi. Hiki cheo tungewaachia Kenya, Zimbabwe na wengine watakaoibiana kura ili kiwasaidie kutengeneza miafaka na kugawana ulaji.
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Ongezea hapo . Hata Lowasa nae anataka urais. Bahati mbaya hamna hata mmoja aliyefanikwa isipokuwa Nyerere peke yake.
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Gharama za kuziendesha ofisi ya makamu wa rais na ile ya waziri mkuu ni kubwa.Tanzania ni nchi masikini sana lakini jambo la kushangza tunazalisha vyeo vya kisiasa bila ya kuwapo sababu za msingi.Enzi za mzee Ruksa tuliwahi kuwa na cheo cha naibu waziri mkuu ambacho hata kwenye katiba hakipo.
  Tufike mahali tuondoe ofisi ya waziri mkuu,kazi zake zihamishiwe kwa makamu wa rais kwa maoni yangu.
  Hakuna sababu za msingi za kuendelea kubakia na waziri mkuu mwenye madaraka nusu nusu.Wenzetu wakenya na wazimbabwe wamekianzisha kwasababu za kuibiana kura.
   
 15. R

  Rayase Member

  #15
  Sep 22, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  to be honest natami kumwona Lowasa akiiingia kwe ushindani! He will struggle to prove tanzania they are wrong! Atachapa kazi! Tuweni wakweli the guy ni mchapa kazi kweli!
   
Loading...