PM: I hate death, prefer killings!

PM: I hate death, prefer killings!

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
8,592
Reaction score
17,560
Ni njema wana Jay Efu?

Kuna jambo la ajabu sana katika ulimwengu wa viongozi makatili. Wamejaa hofu ya kifo, lakini hawasiti kuua wengine. Wanachukia kifo kwao wenyewe, ila wanakipenda kifo cha wengine. Wanaficha udhaifu wao nyuma ya vyeo, sare, na mamlaka; lakini ndani yao, ni waoga kuliko raia wanaowatisha kwa risasi na magereza.

Viongozi hawa wamejaa unafiki. Wanaweka walinzi kila kona, magari ya kivita barabarani, na kamera kila pembe yote kwa hofu ya kufa. Wanajua walivyopanda milima ya maovu, na kwamba kilele chake ni kulipia damu waliyoimwaga. Lakini badala ya kutubu, wanaendelea kumwaga damu zaidi, wakidhani watakuwa salama kwa kumaliza mashahidi wote.

Ni upumbavu ulioje wa kuogopa kifo lakini kupenda mauaji! Wanaamini kuwa risasi, mabomu na mateso vitadumu milele, lakini historia haijawahi kuwa na huruma kwa muuaji. Wanaweza kuua wapinzani, waandishi, au wakosoaji, lakini hawawezi kuua ukweli.

Kifo wanachokikimbia ndicho kinachowasogelea kwa kasi zaidi. Wanaishi kwa hofu, wanalala kwa hofu, wanakula kwa hofu si kwa sababu wanapendwa, bali kwa sababu wamejenga utawala wa damu.

Na mwisho wa yote, dunia itawakumbuka si kama mashujaa, bali kama viongozi dhaifu waliopenda mauaji kuliko haki, waliotetemeka wakisikia neno kifo, ilhali waliwaandalia wengine kaburi.

PM if not AM....

Kunakaribia kukucha kwani giza limezidi


Ndio maana nasema: They hate death, but they prefer killings ie the hypocrisy of tyrants knows no limit.
20251111_183649.jpg
 
What a message! Mwenye masikio na askie na kutenda vema.
PM: I hate death [emoji36] [emoji19] [emoji88] [emoji58] [emoji854] [emoji846] [emoji36] [emoji19] [emoji88] [emoji58] [emoji854] [emoji846] [emoji36] [emoji19] [emoji88] [emoji58] [emoji854]
 
Wapo ambao wamenyooka lkn, kama Tundu Lissu.
 
Back
Top Bottom