Wadau mwenzenu nina shida ya fedha ya haraka nimepungukiwa kama Million nne, nipo Dar nimeamua kuuza Plot yangu fasta, Ipo Dodoma ni kiwanja cha mradi kilitolewa na CDA katika mradi wa April 2006, nilinunua kwa mtu Mwaka 2008 na kupata hati miliki kwa jina langu March 2009. Ni eneo lililokwisha endelea kwani Tayari kuna mitaa ya watu wanaishi, nimekilipia kodi ya ardhi mpaka mwaka wa fedha 2013/14.
Ukubwa wa kiwanja ni Sq Metre 631. Kipo Chidachi West, block 'F' ni walkable distance kutoka St John University, Bei ni Tshs Million 4.1 Hatimiliki ninayo hapa Dar sitaki dalali, kwa mnunuzi wa kweli ani-PM ili utaratibu wa kukiona ufanyike akiridhika tufanye biashara, kwa aliye Dodoma nitamuelekeza akakione mwenyewe kwani ni rahisi kufika nikimpa namba ya Kiwanja, akiridhika anistue.