Please...sema hata neno tu, waweza kumuokoa huyu mama!


ka ushauri kangu kadogo kwako mtu mzima,usije ukaanza 'yale mambo yetu' na huyu mama(maana kaumizwa na hujui kwanini of all the people ka-open up kwako tu)hata kama ni mtandaoni.mzee usije ukapatwa huruma ukaona umpe bi mkubwa faraja ukijua ni kwenye net tu.ya watu kuchinjwa na strangers huanza hivihivi.Au pia inawezekana ukawa ni mtego mama chanja wako baadae akakuchombeza(kimtego)mzee ukafumaniwa mtandaoni.ni hayo tu mkubwa.
 
unajua wanaume wanavutiwa na vitu vingi; (tabia, uzuri, ...............n.k)
Kwa mfano: mwanamke anaweza kumwa mzuri kidogo ila the way anavyom handle mwanaume,,,,,eg ukirudi job au kwenye mizunguko the way anavyokupokea mnavyoongea duh unaweza hata kuwasahau washikaji. tatizo linakuja ukishaoa, duh atamwachia HG kiiiiiiiiiila KITU.

tatizo watu wakiwa kwenye uchumba wanapretend. hawataki kuishi kama walivyo bali wanaishi kuridhishana.

mimi naamini huyo mwanaume ukimhandle+caring kila siku atakuwa home na utakuwa na amani.

vilevile mkuu ungesikiliza pande zote mbili ili utupe story za pande zote ili tutoe maoni kutokana na pande zote.

NB: Mama akumbuke mmewe alikuwa anapenda nn mwanzon then ajaribu kuvirudisha
 
1. Maombi ya mtu mmoja ni tofauti sana na maombi ya mapatano - atafute waombaji wawili au zaidi (walio rohoni) wafunge na kuomba pamoja kwani Mungu anasema "lolote mtakalopatana duniani na kuomba, nitafanya"

2. Ajichunguze alimwomba Mungu ampe mume au alikurupuka? Kama alikurupuka, aombe sala ya toba kwanza.

3. Ajue kwenye maisha kuna majaribu mengi - alichukulie kama jaribu na aelewe kwenye kila jaribu kuna mlango wa kutokea hivyo asikate tamaa

4. Amsamehe mumewe aendelee kumhudumia, kumpenda na kujali familia yake (afanye wajibu wake)
5. Amwombee pia huyo mumewe - nguvu za giza zimtoke

Labda huyu mume ana wapenzi wengine na anamfanyia visa ili aondoke .............yeye asiondoke kwani mume huyo ni haki yake.

6. Awe pia na ujasiri wa kumwuliza mume wake - asimwogope - amwulize ............kulikoni???????????
Hope ushauri wangu utasaidia.
 
Ki ukweli Kuna mahala Mama alikosea, Yanawezza kuwa ni matokeo ya maswala fulani fulani, Honestly tabia hii haiwezi kuwa imetoka nmo where.

Huyu mama ange prioritize needs zake. mfano kama ni ndoa yake........au furaha na peace of mind.....kumuacha haitampa peace as well as kukaa. but asiondoke bt abadili mtazamo wa maisha...........................Asijali sana kutoka kwa mumewe, passwords nk visimuumize kichwa...

mume alale nje ndani...isiwe issue sana kwake................Unyumba nk. ni ngumu bt it will work with time. asi mhoji sana. ajali maisha yake....hivi sivyo ndoa should be, bt with prayers and these acts Hopeful................
 

Ahsante sana mkuu. Hili nadani lilikuwa linamsubua sana huyu mama. Alishaamua kunyamazia kila kitu. Hope atapata ujasiri wa kuongea na mume wake hata kama hatakuwa na uhakika wa majibu au matokea ya hayo maongezi!
 

Mkuu huu wasi wasi unatokea wapi? Kama angekuwa ni mwanamume mwenzangu ndo ameniomba ushauri ungesema hivyo? Halafu mbona watu kibao wanaomba ushauri kila siku na tunajadiliana na kubadilisha mawazo yanaisha? Na je huamini kwamba kuna watu wanatoa huduma kama hizi professionally?

Nadhani wanaume tuna tatizo kubwa. Kwani kila mwanamke lazima utembee naye? Mbona wapo wengi wamenizunguka. Iweje nihangaike na vivuli vya kwenye mtandao?

Hata hivyo jaribu kufuatilia DC ni mtu wa namna gani linapokuja suala la personal intergrity tena kwenye mambo ya ndoa. Vinginevyo wasi wasi wa namna hiyo unaweza kuwa unatupa picha yako mwenyewe.
 
Mimi namshauri a (MULTPLY HIS PRESENCE BY ZERO), yani azidishe na sifuri tu, maana kila namba ukizidisha na sifuri ataendelea kupata sifuri. Kama hana ulemavu ni wakati wake wa kufanya kazi kwa bidii zote ili awalee wanae wawili ambao ni zawadi toka kwa Mungu. Akipata muda wa kupumzika atoke na wanae akajipe raha nje ya nyumbani. Kama ana marafiki awapigie simu na kuchat kama anavyofanya yeye.
NB: asifanye uzinzi ili kumkomoa wala asiondoke maana madhara yake ni makubwa zaidi. Bado ana bank kubwa ya ndugu, watoto wake na marafiki.
 
wako wengi sana DC

Labda muulize kama yeye ni muaminifu kwenye ndoa yake?
 


samahani sana,labda umenielewa vibaya.angekua mwanaume pia ningesema nilichosema kwani msisitizo wangu sana ulikua,kama amepata pa kuongelea matatizo yake(kakuamini na kufunguka kwako),uhusiano waweza kukua toka mtandaoni hadi kukutana uso kwa uso,na huyu ni mgeni kabisa kwako,humfahamu,hata hujui kama anachokwambia ni ukweli halisi au vipi.sasa kutokana na matukio kadhaa niliyosikia na kusoma kuhusu watu waliodhuriwa na strangers(kwani wengi walikutana na watu au hadithi tofauti na walizosikia mtandaoni)waz just tryna be cautious mzee!natambua wapo wanaofanya hivi proffessionaly,umakini tu ndo ulikua msisitizo wangu,sijui hata umeelewa kitu gani.
Kuhusu your personal integrity,mi sio mgeni sana hapa japo sidhani kama pia toka kwenye post tu unaweza pata picha halisi ya mtu(mi si mtaalam wa mambo haya) ila kwa niliyo highlight hapo inanifanya nifikiri zaidi kuhusu hiyo P.I.yako.zaidi sana,SAMAHANI SANA KAMA NIMEKUKWAZA!
 
wako wengi sana DC

Labda muulize kama yeye ni muaminifu kwenye ndoa yake?

Hili amelisema wazi kuwa amekuwa mwanifu katika ndoa yake toka day zero. Ila hakuna jinsi yoyote ya ku-prove kama anasema ukweli.
 

Nashukuru sana kwa uelewa wako. Ni kweli wapo watu ambao wanatumia kila nafasi wanayoipata ku-advance interest tofauti na zile wanazoonesha mbele ya watu. Inawezekana na mimi nikawa mmoja wao kwa sababu mimi pia ni binadamu. Hata hivyo ningeweza kuleta hoja ya kuomba ushauri kama niwe na mahusiano naye au la na hakuna ambaye angenizuia. Maadamu mimi mwenyewe nimesema kuwa sina mpango wowote wa ku-take advantage, nadhani kwa upande wangu hilo linatosha. Halafu binafsi najua kuwa tuko wengi na kwa hiyo lazima tutakuwa na diversity ya kufikiria na ku-conceptualize mambo. Opinion zako zinaheshimika na ni haki yako mkuu.

Tuendelee na mjadala!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…