Please don't do this!!

Chibidu

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
387
49
Ndugu zangu maisha ya kila mwanadamu yana thamani kubwa hapa duniani. Kila mtu anapenda kuishi kwa kadiri Mungu alivyompangia maisha yake. Na kila mtu ana mchango wake katika muendelezo wa hii dunia, awe mkubwa au mdogo.

Mimi nimeona leo tukumbushane tu juu ya tabia ambazo zinachangia sana katika kuondoa uhai wa mwanadamu hapa duniani siku hizi, hasa miongoni mwa vijana. Najua wengine watasema "Kifo kikipangwa, kimepangwa", au "Siku yako ikifika utaondoka tu". Sidhani kama hoja hizo ni za msingi sana maana Mungu ametuumba ili tuitawale hii dunia na sio itutawale. Kwa maana hiyo kuna vitu tunaweza kuvizuia visitokee.


Tabia ninayoizungumzia hapa ni ile ya baadhi ya watu kupenda kutumia simu zao za mkononi wakati wakiwa wanaendesha magari, aidha kutuma ujumbe mfupi ama kuongea kwa muda mrefu. Tabia hii kwa kweli si nzuri hata kidogo kwa kuwa inaondoa maisha ya watu wasio na hatia na hata kuwafanya wengine wawe na ulemavu maishani mwao. kwanini usisubiri mpaka ufike mwisho wa safari yako ndipo uanze kuandika ujumbe? au la kama huo ujumbe ni wa muhimu sana kwanini usiegeshe gari pembeni, umalize kutuma ujumbe kisha uendelee na safari yako? Nakumbuka miaka miwili au mitatu iliyopita jamaa yangu mmoja alifariki papo hapo baada ya kugonga mti wakati akiwa anatuma sms huku akiwa anaendesha gari akitokea Bagamoyo kuja Dar. Jamani tuiache hii tabia itatumaliza.

Najua mara nyingi tumekuwa tukiambiana kuhusu mambo haya, lakini nimeona si vibaya tukikumbusha maana binadamu huwa tuna tabia ya kusahau. Tuache hiyo tabia ni hatari kwa maisha yetu na tuwapendao.

Kama huamini hebu angalia hii clip. Inawezekana kuwa ulishawahi kuiona lakini si vibaya ukarudia tena kuiangalia. Ajali.Ujumbe wangu ndio huo kwa leo.
 
Ukiamini mungu ndipo utaanza kuamini hizi habari za siku yako na upuuzi mwingine kama huo, your destiny to a large part is in your own hand, hamna mungu wala shetani, mungu na shetani ni wewe mwenyewe.
 
Ukiamini mungu ndipo utaanza kuamini hizi habari za siku yako na upuuzi mwingine kama huo, your destiny to a large part is in your own hand, hamna mungu wala shetani, mungu na shetani ni wewe mwenyewe.

Hayo ni mawazo pia, na una uhuru wakuamini hivyo. Lakini hilo halikuwa wazo la msingi. Wazo la msingi ni kuwa tujiepushe na ajali zinazoweza kukingika, hasa zile zinazotokana na watumizi ya simu barabarani.

Kuna wengine siku hizi, utaona mtu anaendesha pikipiki au baiskeli naye anataka kutuma sms wakati anaendesha, are u serious? Hapa utasema ni kazi ya nani?.
 
Last edited:
Back
Top Bottom