Plate number za kigeni(SADC) -Tanzania

JMF

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
1,751
2,749
Salaam wakuu.
Naomba mwenye kufahamu kuhusu matumizi gari yenye plate number za kigeni (SADC) au nchi jirani kama Kenya nchini. Naomba ufafanuzi wa haya maswali au moja wapo kwa anayejua tafadhali.

1. Ni muda gani gari inaruhusiwa kuwepo nchini Tanzania kabla ya kutoka kurudi ilikotoka?
2. Gharama za kuingia na hiyo gari ni kiasi gani?
3. Ukitaka kuongeza siku inawezekana?
4. Ukiamua kuisajili rasmi Tanzania, utaratibu unakuwaje? Yaani kodi zitakuwa kama vile umeagiza kutoka Japan?

Natanguliza shukrani zangu dhati kwa michango yenu
 
Huwa ni miezi mitatu mkuu,kwa gari ndogo unalipia 25usd na gari kubwa unalipia 107usd kwa miezi mitatu,ikitokea dharura unaweza kuongeza siku,pia ukitaka kuisajili unakwenda nayo TRA,nadhani umenielewa
 
Asante k

Shukrani kwa mchango wako mkuu.
 
Salaam wakuu.
Naomba mwenye kufahamu kuhusu matumizi gari yenye plate number za kigeni (SADC) au nchi jirani kama Kenya nchini. Naomba ufafanuzi wa haya maswali au moja wapo kwa anayejua tafadhali.

1. Ni muda gani gari inaruhusiwa kuwepo nchini Tanzania kabla ya kutoka kurudi ilikotoka?
2. Gharama za kuingia na hiyo gari ni kiasi gani?
3. Ukitaka kuongeza siku inawezekana?
4. Ukiamua kuisajili rasmi Tanzania, utaratibu unakuwaje? Yaani kodi zitakuwa kama vile umeagiza kutoka Japan?

Natanguliza shukrani zangu dhati kwa michango yenu

Iko hivi
Gari lenye namba plates za SADC linatakiwa nchini kwa kipindi kisichozidi miezi 3, na unatakiwa u renew kila mwezi kwa gharama ya dola 25.Baada ya miezi 3 gari ni lazima liondoke nchini.
Ukitaka kulisajili tanzania utafanya yafuatayo
1.unapeleka gari kwenye ofisi ya tra iliyoko karibu nawe na unawambia dhumuni la kutaka kulisajili gari tz
2.Inabidi ufanye de-registration from country of origin
3. Inatakiwa uwe na clearance kutoka interpol kudhibitisha gari sio ya wiz
4. Baada ya hapo utaweza kulipa kodi na kupewa usajili wa tz. Kiwango cha kodi kinategemea mambo mengi
 
Back
Top Bottom