Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
SPIKA wa Bunge mstaafu, Pius Msekwa, ameonya kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, anaweza kufungwa jela hadi miaka saba endapo atakaidi wito wa Bunge kutaka aende kujieleza kwa kauli zake, imefahamika.
Kwa mujibu wa Msekwa, kutoitikia wito wa Bunge ni kosa kwa mujibu wa sheria na kwamba adhabu yake inaweza kuwa kubwa kuliko inavyodhaniwa.
Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kinaitaka Kamati ya Maadili kumtaarifu Spika iwapo mtu amekataa kuitikia wito wa kamati bila ya kutoa sababu za maana.
Vyanzo vya kuaminika vya Raia Mwema kutoka ndani ya Bunge vimeeleza kwamba kwa sasa Bunge halitatoa taarifa yoyote kuhusu Makonda hadi wakati “mwafaka” utakapofika.
“Nikwambie hivi, kwa sasa Bunge halina taarifa yoyote ya kutoa kuhusu kuitwa au kutoitwa kwa Makonda bungeni. Hata hivyo, Bunge litatoa taarifa yake kuhusu jambo hilo kwa wakati mwafaka na bila shaka itakuwa kabla ya kuanza kwa mkutano ujao wa Bunge,” kilisema chanzo hicho kilichozungumza kwa masharti ya kutotajwa jina.
Maoni ya Msekwa
Akiandika kwa kirefu kwenye safu yake katika gazeti la serikali, Daily News, Msekwa alisema watu wengi wanafahamu zaidi kuhusu kosa la kuidharau Mahakama lakini hawafahamu sana kuhusu kosa la kudharau Bunge.
“Pengine hii inasababishwa zaidi na ukweli kwamba suala la kudharau Mahakama limeandikwa au kusemwa sana kwenye vyombo vya habari na hivyo linafahamika tofauti na dharau kwa Bunge.
“Hakuna mifano ya kutosha kwa watu walioadhibiwa kutokana na kudharau Bunge na pengine ndiyo maana watu wengi hawafahamu ukubwa wake. Lakini ni kosa kubwa na mtu anaweza kufungwa jela endapo wabunge watakubaliana hivyo,” ameandika Msekwa.
Msekwa alitumia sehemu kubwa ya makala yake hiyo kuelezea kuhusu tukio lililowahi kutokea kwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Augustine Mrema, ambaye nusura aende jela kwa kosa la kusema uongo bungeni.
Ilivyokuwa kwa Mrema
Suala la Mrema lilikuwa namna hii:- Mnamo Juni 16 mwaka 1998, wakati akichangia bungeni kwenye mjadala wa Wizara ya Fedha, Mrema (wakati huo akiwa Mbunge wa Jimbo la Temeke – Dar es Salaam) aliliambia Bunge kwamba kulikuwa na mpango wa siri wa kumuua yeye, Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Luteni Jenerali Imran Kombe.
Kutokana na uzito wa tuhuma hizo, aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Frederick Sumaye, aliinuka na kukanusha maelezo hayo ya Mrema na kuomba Spika (Msekwa) amtake Mrema atoe uthibitisho wa madai yake hayo.
Kutokana uzito wa tuhuma hizo, Spika alimtaka Mrema kuwasilisha bungeni ushahidi wa madai yake hayo katika kipindi cha siku tano kuanzia siku aliyotoa maelezo hayo.
Baada ya siku tano, Mrema aliwasilisha bungeni nyaraka za kuthibitisha madai yake hayo; ikiwamo iliyoonyesha kufanyika kwa mkutano wa kupanga mauaji hayo ulioelezwa kufanyika Aprili 4 mwaka 1996.
Pia, aliwasilisha barua nyingine iliyodaiwa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo kwenda kwa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi kumuagiza amshughulikie Mrema ipasavyo na pia barua iliyodaiwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM kwenda vyombo vya dola ikitaka mienendo ya viongozi wa upinzani ifuatiliwe kwa karibu.
Spika aliamua kuwa nyaraka hizo zinafaa kujadiliwa ili kwamba Bunge la Muungano lijiridhishe endapo zilikuwa za kweli au la.
Mrema alikuwa wa kwanza kuzungumza na katika maelezo yake, alisema aliyempa taarifa hizo kuhusu mkutano huo wa Aprili alikuwa marehemu Kombe ambaye alimwambia kabla hajauawa.
Jenerali Kombe aliuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi mkoani Arusha katika tukio lililoelezwa kuwa alifananishwa na mmoja wa majambazi wakubwa wa magari katika eneo la Afrika Mashariki.
Polisi kwa sababu ya ukweli kwamba mmoja kati ya waliokuwa kwenye orodha yake ya kuuawa alikuwa ameuawa tayari, Mrema alisema huo ni ushahidi wa wazi kwamba mkakati ule wa siri aliousema ulikuwa wa kweli.
Baada ya mjadala, wabunge walikubaliana kwamba nyaraka zile za Mrema hazikuwa za halali na Bunge likaazimia kumsimamisha bungeni kwa muda wote wa mkutano ule uliokuwa umebakia ambao ni siku 40.
Kwa mujibu wa Msekwa, kwa adhabu hiyo, Mrema alitakiwa kujihesabu kama mtu mwenye bahati kwa sababu Bunge lingeweza kuamua pia kulipeleka jambo hilo mahakamani moja kwa moja.
“Hata hivyo, Mrema anatakiwa kujihesabu kuwa mmoja wa watu wenye bahati kwa sababu ya adhabu hiyo nafuu aliyopewa.
“Kama Bunge lingeamua kutumia vema Sheria ya Kinga na Haki kama ilivyoelezwa kwenye kifungu kile cha 26, huenda adhabu ingekuwa mbaya zaidi,” ameandika Msekwa.
Hatua ambayo Bunge lingeweza kufuata wakati huo ni kutoa taarifa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kufungua kesi katika Mahakama ya Kisheria kuhusu jambo la mbunge kusema uongo bungeni.
Hii ni kwa sababu, wakati mtu anapotakiwa kutoa ushahidi wa nyaraka, Bunge linageuka kuwa Mahakama kwa mujibu wa Sheria hiyo ya Kinga.
Kwa sababu hiyo, aliyesema uongo bungeni anakuwa sawa na aliyesema uongo mahakamani na maana yake adhabu inaweza kuwa kifungo kisichozidi miaka saba jela.
Maelezo ya Spika huyo mstaafu yanaweza pia kumaanisha kwamba Makonda anaweza kutakiwa kuthibitisha maelezo yake kwamba “wabunge kazi yao bungeni ni kulala tu” jambo linalomaanisha itabidi ushahidi wake upitiwe.
Kwa sababu wakati wa kupitia nyaraka hizo Bunge linageuka kuwa Mahakama, kama ushahidi wa Makonda utaonekana ni uongo, maana yake ana hatari pia ya kufikishwa kama wabunge wataazimia hivyo.
Katika kumalizia makala yake hiyo, Msekwa aliandika kuwa “…ingawa Mrema alikuwa na bahati, hadhani kuwa mkosaji anayefuata anaweza kuwa na bahati ya namna hiyo”.
Makonda na Bunge
Hatua ya Makonda kuingia matatani na Bunge ilitokana na kitendo cha kuwaita baadhi ya wabunge kuhojiwa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam pasipo kuomba kibali cha Spika kama utaratibu unavyotaka.
Baada ya wabunge kuhoji hatua hiyo, Makonda alinukuliwa akidai kuwa hawezi kutikiswa na wabunge ambao kazi yao ni kulala tu bungeni.
Majibu hayo ya Makonda yaliwachukiza wabunge ambao walitaka mkuu huyo wa mkoa aitwe kujieleza bungeni kutokana na matamshi yake hayo.
Katika siku ya mwisho ya mkutano uliopita wa Bunge, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alieleza kukerwa kwake na kitendo cha wabunge wake kuitwa pasipo yeye kuarifiwa.
“Mambo haya ya ofisa mmoja hapa na pale kusahau mipaka ya kazi zao na kuvuka kidogo ni mambo ya kawaida, mahali panapohusika watachukua hatua za kuweka sawasawa tu, haya ni mambo ya kujisahau sahau hivi.
“Maana mimi naweza nikawa nawahitaji wabunge hapa kuna mambo tunatakiwa tufanye ambayo ni ya kitaifa, nimewaita wabunge mko hapa labda mko kwenye kamati, tunahitaji akidi, akikosekana mbunge mmoja inawezekana jambo hilo kwenye kamati lisipite.
“Kwa hiyo kama kuna junior officer (ofisa mdogo) huko anahitaji mbunge lazima aniambie, hatuwezi kwenda hivyo, kwa hakika tukienda tu kibabe kibabe namna hii, tutavuruga nchi haiwezekani, hatuwezi tukaenda hivi,” alisema Ndugai.[/ATTACH]