Pitso Mosimame: Ulaya wanabagua makocha kutoka Afrika

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,738
15,211
Kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns,Al Ahly ambaye kwa sasa anafundisha klabu ya Al-Wehda ya United Arab Emirates Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini,amesema sio kwamba makocha wa Afrika hawana vigezo vya kufundisha timu za Ulaya, bali timu za Ulaya ndio hazitaki kukubali kuajiri makocha wa Afrika.

“Mpira hauhusu wapi unatokea. Tunaweza kuzunguka na kuleta visingizio lakini ni rahisi tu, Ulaya haitaki kuajiri Makocha wa Kiafrika.

“Kazi yangu ni kujenga imani na kumbukumbu ya kudumu kwa Makocha wa Kiafrika na kuwafanya waseme ‘Angalia,Ninafikiria kuna kitu Afrika’, tuwape nafasi.

Ulaya bado haikubali kocha wa Kiafrika. Wanakuja kununua wachezaji kuwasaidia washinde Klabu Bingwa Ulaya.

“Sadio Mane na Mohamed Salah walikuja kuwasaidia Liverpool kushinda Klabu Bingwa kama Neymar na Messi.

“Kama ukiangalia usajili,kiasi gani walilipa kuwasajili Sadio Mane na Mo Salah na kiasi gani walilipa kwa wachezaji wa Amerika Kusini.?”

“Wanatakiwa kubadili mitazamo yao kwa Waafrika. Kylian Mbappe ana asili ya Afrika. Sawa na N’Golo Kante na Karim Benzema. Ulaya inalishwa na Afrika.

“Nilikuwa naangalia klabu bingwa Ulaya, nikaona wachezaji Waafrika wote wanacheza. Sasa wako wapi makocha wa Afrika? Wana wachezaji wa Afrika tu. Unaweza kusema makocha wa Afrika wanatakiwa wawe na ubora fulani, ni sawa, Mimi nipo hapa”. Amesema Pitso Mosimane kupitia AD Sports.

Akiwa na Makombe matatu ya Klabu Bingwa Afrika, hakuna kocha wa Afrika aliyeshinda idadi hiyo ya makombe kama Pitso.

“Makocha wangapi wa Ulaya wameshinda Klabu Bingwa Ulaya mara 3? Si wengi. Carlo Ancelotti mara 4 ,Pep Guardiola pengine mara tatu, Jurgen Klopp mara moja, kwa hiyo ni vigumu” aliongeza.

“Kama ukishinda klabu bingwa Afrika, haimanishi pia ninaweza kushinda Asia au Ulaya?
Unadhani klabu kama Bayern Munich itakuja kwangu?!

“Kiuhalisia. hawatakuja ila tuache kusema kuhusu Bayern. Tuongee kuhusu Red Bull Salzburg, Leipzig au West Ham. Unadhani wana kocha ambaye ameshinda makombe kama mimi? hakuna hata mmoja.”
 
Ulaya kugumu jaman ,ifike hatua wakubali tu ...cheki kina

Potchetno wanavohangaika ...

Lampard ndio Hana hamu kabisa ..

Kina Rooney wanashusha team daraja ...

Kompany mpaka sasa haelewi anakosea wapi na Burnley yake ,Kila game Ni kichapo ,..

Steven Gerrard katimuliwa mapema Sana baada ya kushindwa Kazi Aston Villa wakati rangers alikuwa anawasha ....

Cheki ten hag anavochanganyikiwa na united ...

Ulaya sio poa kama huna pumzi ya kibabe kama Kina pep ,Carlo ,Klopp hata ukipewa club Ni game 10 ushapoteana ...
 
Ameongea ukweli, bado ubaguzi huo upo ila ipo siku yupo ataevunja hiyo miiko
Sio kwamba makocha wa Afrika hawana ubora bali ni maamuzi tu ya wamiliki wenyewe
 
Ulaya kugumu jaman ,ifike hatua wakubali tu ...cheki kina

Potchetno wanavohangaika ...

Lampard ndio Hana hamu kabisa ..

Kina Rooney wanashusha team daraja ...

Steven Gerrard katimuliwa mapema Sana baada ya kushindwa Kazi Aston Villa wakati rangers alikuwa anawasha ....

Cheki ten hag anavochanganyikiwa na united ...

Ulaya sio poa kama huna pumzi ya kibabe kama Kuna pep ,Carlo ,Klopp hata ukipewa club Ni game 10 ushapoteana ...
Wameshajaribu kuwapa akina Pitso wakashindwa?
 
Niliona wakati anafundisha Al ahly kwenye klabu bingwa ya dunia, muda mwingi timu ilikaa nyuma. Ile ilikuwa nafasi take kuonyesha makocha wa Africa Wana kitu. Kocha wa Morocco alivyofanya kombe la dunia akitaka timu ni rahisi kupata Ila akubali kuanzia timu za chini na.akionyesha uwezo atachukuliwa.
Huwezi kuanza moja kwa moja timu kubwa kwani hata kina Klop walianzia timu ndogo mpaka wakachukuliwa timu kubwa.
 
Umesoma?
 
Kama timu zetu zabongo tu haziamin makocha waafrika itakua huko ulaya acheni unaa
 
Na Mimi niliwahi kutaka kuamini hivyo lakini ni hisia tu.

Omar Daf ni Head coach wa timu ya Amiens ya ufaransa.
Kabla ya klabu hii alikuwa Dijon.
Huyu ni msenegali..
Alikuwa ni beki 3 kwenye kikosi cha Senegal ya 2002

Habib Beye....ni head coach wa Avranches ya ufaransa.
Huyu nae ni msenegali..na Aliwahi kuja na Simba wa terranga Tanzania kule mwanza kipindi cha maximo.

Hizi ni timu za championship Kule France.

Zulte waregem timu aliyokuwa anachezea Novatus Miroshi ilikuwa ikifundishwa na msenegali mwaka Jana akaharibu.wakatimua.
Zulte ilikuwa ligi kuu ya ubelgiji.
Ubelgiji ni ulaya.
 
Yeye akipata nafasi aitumue vizuri kuonyesha uwezo wake.Hayo mengine yanabaki kua maamuzi ya wenye timu.Afrika uku kuna msemo wetu tunasema kwa makubaliano ya pande zote mbili.
 
Na Mimi niliwahi kutaka kuamini hivyo lakini ni hisia tu.

Omar Daf ni Head coach wa timu ya Amiens ya ufaransa.
Kabla ya klabu hii alikuwa Dijon.
Huyu ni msenegali..
Alikuwa ni beki 3 kwenye kikosi cha Senegal ya 2002

Habib Beye....ni head coach wa Avranches ya ufaransa.
Huyu nae ni msenegali..na Aliwahi kuja na Simba wa terranga Tanzania kule mwanza kipindi cha maximo.

Hizi ni timu za championship Kule France.

Zulte waregem timu aliyokuwa anachezea Novatus Miroshi ilikuwa ikifundishwa na msenegali mwaka Jana akaharibu.wakatimua.
Zulte ilikuwa ligi kuu ya ubelgiji.
Ubelgiji ni ulaya.
Sawa
 
Kocha wa zamani wa Mamelodi Sundowns,Al Ahly ambaye kwa sasa anafundisha klabu ya Al-Wehda ya United Arab Emirates Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini,amesema sio kwamba makocha wa Afrika hawana vigezo vya kufundisha timu za Ulaya, bali timu za Ulaya ndio hazitaki kukubali kuajiri makocha wa Afrika.

“Mpira hauhusu wapi unatokea.
Tunaweza kuzunguka na kuleta visingizio lakini ni rahisi tu, Ulaya haitaki kuajiri Makocha wa Kiafrika.

“Kazi yangu ni kujenga imani na kumbukumbu ya kudumu kwa Makocha wa Kiafrika na kuwafanya waseme ‘Angalia,Ninafikiria kuna kitu Afrika’, tuwape nafasi.

Ulaya bado haikubali kocha wa Kiafrika. Wanakuja kununua wachezaji kuwasaidia washinde Klabu Bingwa Ulaya.

“Sadio Mane na Mohamed Salah walikuja kuwasaidia Liverpool kushinda Klabu Bingwa kama Neymar na Messi.

“Kama ukiangalia usajili,kiasi gani walilipa kuwasajili Sadio Mane na Mo Salah na kiasi gani walilipa kwa wachezaji wa Amerika Kusini.?”

“Wanatakiwa kubadili mitazamo yao kwa Waafrika. Kylian Mbappe ana asili ya Afrika. Sawa na N’Golo Kante na Karim Benzema. Ulaya inalishwa na Afrika.

“Nilikuwa naangalia klabu bingwa Ulaya, nikaona wachezaji Waafrika wote wanacheza.
Sasa wako wapi makocha wa Afrika?Wana wachezaji wa Afrika tu.
Unaweza kusema makocha wa Afrika wanatakiwa wawe na ubora fulani, ni sawa, Mimi nipo hapa”. Amesema Pitso Mosimane kupitia AD Sports.

Akiwa na Makombe matatu ya Klabu Bingwa Afrika, hakuna kocha wa Afrika aliyeshinda idadi hiyo ya makombe kama Pitso.

“Makocha wangapi wa Ulaya wameshinda Klabu Bingwa Ulaya mara 3? Si wengi. Carlo Ancelotti mara 4 ,Pep Guardiola pengine mara tatu, Jurgen Klopp mara moja, kwa hiyo ni vigumu” aliongeza.

“Kama ukishinda klabu bingwa Afrika, haimanishi pia ninaweza kushinda Asia au Ulaya?
Unadhani klabu kama Bayern Munich itakuja kwangu?!

“Kiuhalisia. hawatakuja ila tuache kusema kuhusu Bayern. Tuongee kuhusu Red Bull Salzburg,Leipzig au West Ham. Unadhani wana kocha ambaye ameshinda makombe kama mimi? hakuna hata mmoja.”
Makocha wa kiafrika au weusi?
 
Back
Top Bottom