Pitia hapa kabla ya kuanza mahusiano

Pitia hapa kabla ya kuanza mahusiano

MEKADDISHKEM

Senior Member
Joined
Sep 15, 2016
Posts
153
Reaction score
150
Mahusiano ni mazuri lakini yana pande mbili za uhai na mauti. Fuata njia hizi kabla ya kuanza mahusiano ili uyajengee uhai na sio mauti.

1. UNAANZISHA MAHUSIANO NA NANI?

Sio kila mtu ni wakuanzisha mahusiano nae sio kila mtu ni sahihi. Kumbuka sio kila king'aacho ni dhahabu. Kuna mahusiano mengine yataharibu ndoto zako.

Kabla ya kuanzisha mahusiano fanya uchunguzi wa awali. Huwezi kumrekebisha tabia mkubwa mwenzio lakini ukijua msingi aliyokulia itakusaidia

2. UNAANZISHA MAHUSIANO WAKATI GANI?

Chunga usianzishe mahusiano wakati una uhitaji sana wa ndoa utapata ambaye siye.

Usianzishe mahusiano Kama haupo tayari.

Usianzishe mahusiano mapya muda mfupi baada ya kuvunja mahusiano mengine.

Usianzishe mahusiano wakati una msongo wa mawazo.

Usianzishe mahusiano kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

Usianzishe mahusiano kwa kumhurumia mtu acha kuwa mama au baba huruma.

Usianzishe mahusiano kwa sababu ya ushawishi.

Usianzishe mahusiano wakati ukiwa umefurahi Sana hapa akili yako inakuwa haifikirii ipasavyo.

3. UNAANZISHA MAHUSIANO KWA SABABU GANI?

Awali la msingi jiulize kwanini unaanzisha mahusiano. Usianzishe mahusiano kwa sababu ya kuwafurahisha wazazi na marafiki.

Mdada usianzishe mahusiano kwa sababu muda umeenda. Wengine mnataka ndoa za kushangaza Dunia. Usianzishe mahusiano kwa ajili ya fedha

4. UNAANZISHA MAHUSIANO KWA NJIA GANI?

Njia utakayotumia kuanzisha mahusiano yako ni muhimu sana. Nakushauri usianzishe mahusiano kwenye mitandao ya kijamii, asilimia kubwa ya mahusiano ya social network ni maigizo.

Mchumba unayemuuona kama Cleopatra ukikutana nae hana makeup picha haijapita 360 utamkimbia.

Jiulize:

Umejipima na kujiona una uwezo wa kubeba changamoto za maisha upo tayari kufumba macho yako na kuyaelekeza kwa uliyemchagua?

Upo tayari kulipa gharama za mahusiano kama zifuatazo
a) Gharama ya mapungufu yake
b) Gharama ya uvumilivu
c) Gharama ya kupoteza haki zako kwa ajili ya uliyemchagua

5. PATA USHAURI SAHIHI KWA WALIOKUTANGULIA

Angalia mwenye ndoa ya mfano:

Unaweza kujiona upo sahihi kumbe umepotea. Kumbuka yale ambayo macho yako hayawezi kuyaona mwingine anaweza kukusaidia kuyaona. Pia kuwa makini nani unamuomba ushauri.

TAFAKARI UTACHUKUA HATUA GANI ENDAPO MAHUSIANO UNAYOINGIA YATAHARIBIKA?


God plans are Greater than our Dreams
 
Hope huu ujumbe utanisaidia ninapoanza kutafta mwenzi mpya
 
Hayo mambo muhimu sana, ila kwa kizAzi hichi cha kiokote watu wanaangalia tako na pesa kwanza. Mengine watavumiliana!
 
Hayo mambo muhimu sana, ila kwa kizAzi hichi cha kiokote watu wanaangalia tako na pesa kwanza. Mengine watavumiliana!
mkuu inabidi tubadilike
ndoa bila upendo hata uwe na fedha bado utajihisi upweke
 
Karibu chama la Bachelor, ukinipenda tunamaliza leoleo tu...Siku hizi kwa kudanganyana Mvulana Msichana ishakuwa poa poa tu
 
Back
Top Bottom