Pitia hapa kabla ya kuanza mahusiano

Pitia hapa kabla ya kuanza mahusiano

Ujumbe poa sana!


Ila hatutouzingatia..
 
Mahusiano ni mazuri lakini yana pande mbili za uhai na mauti fuata njia hizi kabla ya kuanza mahusiano ili uyajengee uhai na sio mauti
1UNAANZISHA MAHUSIANO NA NAN
-Sio kila mtu ni wakuanzisha mahusiano nae sio kila mtu ni sahihi.Kumbuka sio kila king'aacho ni dhahabu
-kuna mahusiano mengine yataharibu ndoto zako
-kabla ya kuanzisha mahusiano fanya uchunguzi wa awali huwezi kumrekebisha tabia mkubwa mwenzio.Lakini ukijua msingi aliyokulia itakusaidia

2. UNAANZISHA MAHUSIANO WAKATI GANI
-Chunga usianzishe mahusiano wakati unauhitaji Sana wa ndoa utapata ambaye siye
-Usianzishe mahusiano Kama haupo tayari
-Usianzishe mahusiano mengine muda mfupi baada ya kuvunja mahusiano mengine
-Usianzishe mahusiano wakati unamsongo wa mawazo
-usianzishe mahusiano kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi
-Usianzishe mahusiano kwa kumhurumia mtu acha kuwa mama au baba huruma
-usianzishe mahusiano kwa sababu ya ushawishi
-Usianzishe mahusiano wakati ukiwa umefurahi Sana hapa akili yako inakuwa haifikirii ipasavyo

3.UNAANZISHA MAHUSIANO KWA SABABU GAN?
awali LA. msingi jiulize kwa nini unaanzisha mahusiano .Usianzishe mahusiano kwa sababu ya kuwa furahisha wazazi na marafiki
-Mdada usianzishe mahusiano kwa sababu muda umeenda
-wengine mnataka ndoa za kushangaza Dunia
-usianzishe mahusiano kwa ajili ya fedha

4.UNAANZISHA MAHUSIANO KWA NJIA GANI
njia utakayo tumia kuanzisha mahusiano yako ni muhimu Sana
nakushauri usianzishe mahusiano kwenye mitandao ya kijamii Asilimia kubwa ya mahusiano ya social network ni maigizo mchumba unaye muuona Kama Cleopatra ukikutana nae Hana make up picha haijapita 360 utamkimbia
Jiulize........
-Umejipima na kujiona unauwezo wa kubeba changamoto Za maisha upo tayari kufumba macho yako na kuyaelekeza kwa uliye mchagua
-upo tayari kulipa gharama Zach mahusiano Kama zifutazo
a) Gharama ya mapungufu yake
b) Gharama ya uvumilivu
c) Gharama ya kupoteza haki zako kwa ajili ya uliyemchagua

5.PATA USHAURI SAHIHI KWA WALIO KUTANGULIA
angalia mwenye ndoa ya mfano
unaweza kujiona upo sahihi kumbe umepotea
kumbuka Yale ambayo macho yako hayawezi kuyaona mwingine anaweza kukusaidia kuyaona
-pia kuwa makini Nani unamuomba ushauri

TAFAKARI UTACHUKUA HATUA GANI ENDAPO MAHUSIANO UNAYOINGIA YATAHARIBIKA?


God plans are Greater than our Dreams
Watu wabaya. Yaani umegonga point za maana afu watu wamekunyima ata like moja
 
Karibu chama la Bachelor, ukinipenda tunamaliza leoleo tu...Siku hizi kwa kudanganyana Mvulana Msichana ishakuwa poa poa tu
Baada ya kumalizana yanaibuka
-majeraha ya moyo
-kuvunjiwa heshima
Na kuacha alama mbaya mioyoni mwa watu isiyo sahaulika
kwa nini usitafute mmoja ukajiungamanishe naye mbele za Mungu utulie mkuu
 
Baada ya kumalizana yanaibuka
-majeraha ya moyo
-kuvunjiwa heshima
Na kuacha alama mbaya mioyoni mwa watu isiyo sahaulika
kwa nini usitafute mmoja ukajiungamanishe naye mbele za Mungu utulie mkuu
Tutatulia mkuu usijali..mahusiano ya siku hizi pasua kichwa
 
Kama ulimaanisha pia kwa ajili ya uchumba nadhani pia kabla ya kuanzisha mahusiano (uchumba) mwombe sana Mungu akuletee/akukutanishe na mtu sahihi.
 
Back
Top Bottom