PISHI: Wali mixer by tambi

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,913
Reaction score
67,434
Hellow mchana mwema

Leo tupike hiki chakula asili yake Madam B atasema

Kwanza chukua tambi zako ulizo kataka ndogo ndogo kisha weka kwenye sufuria ya mafuta yalio chemka kisha anza kuzikaanga mpaka zibadirike rangi na kuwa kahawia zisiungue

Baada ya hapo chukua mchele wako ulio uosha kisha tia kwenye sufuria anza kuukaanga na tambi

Baada ya hapo weka maji yako kama una tui la nazi tumia mimi nazi nakuja kuweka baadae baada ya maji kupungua kidogo
Kisha funika na upunguze moto moto weka mdogo kabisa na ukaee kwa muda mrefu
Baada ya hapo mm nikaweka nazi kisha nikageuza nikaacha nikaanza kupika mboga

Mboga kwa mimi natumia kuku rosti na wewe unaweza tumia samaki au nyama mboga yoyote ulio nayo
Nilianza kukaanga kuku kwanza

Kisha nikaweka vitunguu pamoja na hoho na karoti

Kisha nikaweka nyanya nilio saga

Baada ya nyanya kuiva nikaweka nazi

Baada ya hapo nipo nakula karibuni sana wote

Nipo tayari kwa kusimangwa 😂
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…