Pishi la Biriani

amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
16,103
30,991
Kwanza tuelewane hapa ni mapishi two in one wali ulioonyoka(basmati rice namanisha basmati siyo ile ya shinyanga ukiichemsha inashikamana kama ugali ) na ule mchuzi wake mzito
MAHITAJI YA MCHUZI HAPA TUFANYE KUKU NDO ANAYENOGA MAANA MIE BIRIANI LA NG'OMBE HAPANA PENDA

MAHITAJI YA MCHUZI WA BIRIANI
1.KUKU MZIMA mate vipande kulingana na family yako
2.VITUNGUU MAJI vikubwa chukua 6-8
3.Viungo vitunguu swaumu,ndimu,ciurry powder na giligilani
4.Nyanya za kawaida chukua 8 pia chukua tomato paste ya kipakti kwa kuongeza rangi ya mchuzi
5.Maziwa mtindi
6Karrot, hoho
7.Chumvi kama unapenda kuweka maroyco mchuzi mix utanunua.
8.mafuta ya kula

JINSI YA KUANDAA
Baada ya kumkata kuku vipande vipande muoshe atakate kisha mkamulie ndimu,weka chumvi,vitunguu swaumu,weka currypowder.(hapa unamlowanisha kuku kukata shombo kama wa kizungu kama wa kienyeji mchemshe kabisa)

Chukua mafuta ya kula kiasi yachemsha kwenye sufuria yakipata moto weka vitunguu maji kaaamga mpaka viwe vya brown,weka nyanya(toa mbegu a.k.a mahirizi ya ndani yake )nyanya zikishaiva weka wale kuku uliowaloweka/wachemsha,kaanga wapate kuingia nyanya kisha weka tomato paste yote na currypowder kaanga mpaka ile harufu ya tomato paste iishe kisha weka karrot baada ya kuzikata style uitakayo kaanga kidogo weka kikombe kimoja cha maziwa mtindi ujazo unaweza kutumia vile vikombe vya thermos hapa kaanga hakikisha maziwa mtindi yanaiva kukata harufu ya maziwa mtindi na rangi ile nyeupe ya mtindi ipotee(mtindi unasaidia kuongeza uzito na ladha ya mchuzi KUMBUKA BILA MTINDI HUU MCHUZI HAUJAKAMILIKA).
Ukimaliza weka hoho kata style unayoitaka weka ndimu,weka giligilani kaanga kidogo sana kisha weka maji kidogo kuongeza mchuzi kumbuka huu mchuzi ni mzito ikichemka kidogo ipua tayari kwa kuliwa.

MAHITAJI YA KUPIKA WALI
1.BASMATI RICE AU PISHORI Pima vikombe kulingana na ukubwa wa familia yako
2.Rangi za chakula food colour(rangi 3 au 2 red,yellow&green zinapendeza sana)
3.mafuta ya kula kiasi kulingana na mchele wako
CHUKUA BASMATI RICE(pishori) PIMA VIKOMBE KULINGANA NA FAMILY YAKO ILA KUMBUKA HUU MCHELE KWA KUVIMBA NI HATARI
Huu mchele hauoshwi unauchemsha na maji mengi ukishachemka kabisa na kuchangamka chuja maji,usiive kabisa yaani uive nusu(usiogope kuuchemsha maana haushikamani labda pishori ya shinyanga)
Chukua sufuari weka jikoni yachemshe yakipata moto weka huo mchele uliochemsha uingie mafuta chukua rangi zake zichanganye na maji kidogo mwagia moja rangi moja, inayofata rangi nyingine inayofata rangi ingine(kuwa makini na rangi usidishe yaani kila rangi kidogo kidogo)kisha toa moto wa chini ya jiko utoe wote kisha yale maji uliyoyachuja mwagia kidogo kisha funikia na moto juu ili uive kabisa.
Baada ya kusubiria kama dakika 6 toa mfuniko changanya wali ili rangi zichanganyike ziwe na tafsira nzuri.
Pakua kwenye sahani wali na mchuzi wake mwagia kwa juu.
Pembeni mixer ya mango na passion juice,ndizi ukipenda unatengeneza na saladi.

Kumbuka biriani ina mapishi mengi kuna ile ya kukaanga vitunguu pembeni mie siifagiliagi kuna ile wanachanganya kabisa wali na mchuzi(somali type)mie siipendi hii pia.
Naipendelea hii simple na tamu sana pia kuna wengine waweka tangawizi giligilani,kotmir hiriki.Kwenye chakula viungo vikiwa vingi chakula kinakera
Bon appetite
Kongosho BADILI TABIA Asprin Mtambuzi he he he siku nitakupikia uje ule Madame B Paloma Kipaji Halisi Mentor YNNAH arabella KOKUTONA Preta Nivea Kaizer Filipo marejesho Arushaone Mrembo by Nature figganigga Heaven on earth cacico gfsonwin snowhite mimisa King'asti Smile ladyfurahia
Wana JF chef wote mnakaribishwa
 
Kwanza tuelewane hapa ni mapishi two in one wali ulioonyoka(basmati rice namanisha basmati siyo ile ya shinyanga ukiichemsha inashikamana kama ugali ) na ule mchuzi wake mzito
MAHITAJI YA MCHUZI HAPA TUFANYE KUKU NDO ANAYENOGA MAANA MIE BIRIANI LA NG'OMBE HAPANA PENDA

MAHITAJI YA MCHUZI WA BIRIANI
1.KUKU MZIMA mate vipande kulingana na family yako
2.VITUNGUU MAJI vikubwa chukua 6-8
3.Viungo vitunguu swaumu,ndimu,ciurry powder na giligilani
4.Nyanya za kawaida chukua 8 pia chukua tomato paste ya kipakti kwa kuongeza rangi ya mchuzi
5.Maziwa mtindi
6Karrot, hoho
7.Chumvi kama unapenda kuweka maroyco mchuzi mix utanunua.
8.mafuta ya kula

JINSI YA KUANDAA
Baada ya kumkata kuku vipande vipande muoshe atakate kisha mkamulie ndimu,weka chumvi,vitunguu swaumu,weka currypowder.(hapa unamlowanisha kuku kukata shombo kama wa kizungu kama wa kienyeji mchemshe kabisa)

Chukua mafuta ya kula kiasi yachemsha kwenye sufuria yakipata moto weka vitunguu maji kaaamga mpaka viwe vya brown,weka nyanya(toa mbegu a.k.a mahirizi ya ndani yake )nyanya zikishaiva weka wale kuku uliowaloweka/wachemsha,kaanga wapate kuingia nyanya kisha weka tomato paste yote na currypowder kaanga mpaka ile harufu ya tomato paste iishe kisha weka karrot baada ya kuzikata style uitakayo kaanga kidogo weka kikombe kimoja cha maziwa mtindi ujazo unaweza kutumia vile vikombe vya thermos hapa kaanga hakikisha maziwa mtindi yanaiva kukata harufu ya maziwa mtindi na rangi ile nyeupe ya mtindi ipotee(mtindi unasaidia kuongeza uzito na ladha ya mchuzi KUMBUKA BILA MTINDI HUU MCHUZI HAUJAKAMILIKA).
Ukimaliza weka hoho kata style unayoitaka weka ndimu,weka giligilani kaanga kidogo sana kisha weka maji kidogo kuongeza mchuzi kumbuka huu mchuzi ni mzito ikichemka kidogo ipua tayari kwa kuliwa.

MAHITAJI YA KUPIKA WALI
1.BASMATI RICE AU PISHORI Pima vikombe kulingana na ukubwa wa familia yako
2.Rangi za chakula food colour(rangi 3 au 2 red,yellow&green zinapendeza sana)
3.mafuta ya kula kiasi kulingana na mchele wako
CHUKUA BASMATI RICE(pishori) PIMA VIKOMBE KULINGANA NA FAMILY YAKO ILA KUMBUKA HUU MCHELE KWA KUVIMBA NI HATARI
Huu mchele hauoshwi unauchemsha na maji mengi ukishachemka kabisa na kuchangamka chuja maji,usiive kabisa yaani uive nusu(usiogope kuuchemsha maana haushikamani labda pishori ya shinyanga)
Chukua sufuari weka jikoni yachemshe yakipata moto weka huo mchele uliochemsha uingie mafuta chukua rangi zake zichanganye na maji kidogo mwagia moja rangi moja, inayofata rangi nyingine inayofata rangi ingine(kuwa makini na rangi usidishe yaani kila rangi kidogo kidogo)kisha toa moto wa chini ya jiko utoe wote kisha yale maji uliyoyachuja mwagia kidogo kisha funikia na moto juu ili uive kabisa.
Baada ya kusubiria kama dakika 6 toa mfuniko changanya wali ili rangi zichanganyike ziwe na tafsira nzuri.
Pakua kwenye sahani wali na mchuzi wake mwagia kwa juu.
Pembeni mixer ya mango na passion juice,ndizi ukipenda unatengeneza na saladi.

Kumbuka biriani ina mapishi mengi kuna ile ya kukaanga vitunguu pembeni mie siifagiliagi kuna ile wanachanganya kabisa wali na mchuzi(somali type)mie siipendi hii pia.
Naipendelea hii simple na tamu sana pia kuna wengine waweka tangawizi giligilani,kotmir hiriki.Kwenye chakula viungo vikiwa vingi chakula kinakera
Bon appetite Kongosho BADILI TABIA Asprin Mtambuzi he he he siku nitakupikia uje ule Madame B Paloma Kipaji Halisi Mentor YNNAH arabella KOKUTONA Preta Nivea Kaizer Filipo marejesho Arushaone @Blaki Woman Mrembo by Nature figganigga Heaven on earth cacico gfsonwin snowhite mimisa King'asti Smile ladyfurahia @

oh merci boucoup amu!
nalipendaga birian lakin sikuwahi kupata nguvu ya kujaribu kulipika!
ahsante sana odo!
 
Last edited by a moderator:
unajua mie mtu alikuwaga akisema anapika
biriani nilijua ina macomplikesheni kibao kummbe walaa!!!!!!

asante best amu
 
Last edited by a moderator:
Thanks amu kwa mwaliko likiiva tu nistue
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: amu
amu nasubiri mwaliko wa kuja kufuturu ukiniandalia hadi DAKU nayo nashukuru kwa mikono na miguu
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: amu
Asante sana amu umetuondolea shombo la verossa nitajaribu siku moja nione kweli sijawahi pika bii makitu
mimi napendelea sana wadudu wa baharini natafuta sana kujifunza kuwatengeneza na wali na chipsi mara chache nilizoenda kule bongoyo kisiwani nimejifunza mengi najua kuwaunga prons na wali hivi ndio vyakula vyangu nikija kwako oh nitakuheshimu sana chips samaki,prons na wali,ngisi na chochote etc napenda sana pia napenda sana biriani la maini ya ngo'mbe i like that kuna dada mmja niliishi naye mwatrabu dah alikuwa ananifurahisha sana na biriani na kuku,maini,ngombe wacheni tu saumu tunaaribiana jamani.
 
Last edited by a moderator:
unajua mie mtu alikuwaga akisema anapika
biriani nilijua ina macomplikesheni kibao kummbe walaa!!!!!!

asante best amu
kweli kabisa best hizo complications zinasababisha maviungoooooo kibao amabayo hayana hata kazi sanasana yanakereketa kwenye koo wakati wa kula hii simple way na taaaamu balaaa
 
Thanks amu, umenipa sababu ya kukaa jikoni this weekend
 
Last edited by a moderator:
amu tafadhari kwa hili pishi mi udenda tu hapa
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: amu
hilo biriani la kuku sijawai kulipika nshazoea birian la nyama ya kitimoto sasa amu itabidi kesho jioni nije pale wakoma unifundishe namna ya kuliandaa kwani #Baba Abwene anapenda sana chakula hicho nataka nimpe mahanjumati ya kitanga, si unajua ndoa best lazima uijenge wewe mwanamke?
 
mhhh no comment
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom