Piramidi za Giza nchini Misri

Bilionea kid

JF-Expert Member
Oct 19, 2018
581
516
Kwanza nawasalimu wote wa jf member na wasio member, poleni na majukumu, MUNGU Ni mwema

Kama kichwa cha habari kinavyo sema hapo juu leo tutaangazi mapiramidi ya giza yalioko kule misri..

Songa nayoo....

Piramidi za Giza ni kati ya majengo yanayojulikana zaidi duniani. Pamoja na mava mengine ni sehemu ya makaburi ya Giza yaliyokuwa mahali pa kuzika wafalme wa Misri na wakubwa wa milki yao kwa muda wa miaka 2500.

Ziko kando ya bonde la mto Nile, karibu na mji wa Giza takriban kilometa 15 kutoka Kairo, mji mkuu wa Misri.

Historia ya maeneo ya makaburi ya Giza kwa jumla

Makaburi ya kwanza yalijengwa huko tangu chanzo cha milki ya Misri ya Kale takriban miaka 3,000 KK.

Wakati wa nasaba ya 4 ya Misri eneo la makaburi hayo liliongezeka sifa kwa sababu wafalme Kheops, Khefren na Mykerinos waliamua kujenga huko piramidi kwa ajili ya makaburi yao wenyewe.

Kutokana na ujenzi wa makaburi ya kifalme ndugu wa familia zao na maafisa wa juu walizikwa huko pia hadi mwisho wa nasaba ya 7 ya Misri.

Baada ya hapo na kwa sababu ya kuhamishwa kwa mji mkuu wa milki kwenye kusini ya nchi umuhimu wa eneo la makaburi ya Giza ulipungua. Mazishi ya maana yalitokea tena wakati wa nasaba za mwisho za Misri, katika vipindi vya kuvamiwa na Uajemi.

Piramidi kubwa na Sfinksi

Eneo la makaburi ya Giza hujulikana hasa kutokana na piramidi kubwa pamoja na sfinksi kubwa zilizokuwa maarufu tayari katika nyakati za kale. Mwanahistoria wa Ugiriki wa Kale aliyeitwa Herodoti alizihesabu kati ya Maajabu Saba ya Dunia na tangu siku zile miaka 2,500 iliyopita zilitembelewa na watalii.

Piramidi tatu kubwa zinajulikana kufuatana na majina ya Kigiriki ya mafarao au wafalme wa Misri waliozikwa ndani yao: piramidi za Kheops, Khefren na Mykerinos. Piramidi za Kheops na Khefren ziko karibu kimo moja, ile ya Kheops ni kubwa kidogo lakini ile ya Khefren inaonekana kubwa kwa macho kwa sababu imejengwa juu ya ardhi ya juu kiasi kwa hiyo kwa macho ya mtazamaji inafika juu zaidi.

Jina la Kigiriki Jina la Kimisri Alitawala mnamo Kimo asilia Kimo cha leo Kipimo cha

upande wa msingi
Piramidi ya Kheops Khufru ~ 2620

- 2580 KK 146.1 m 138.75 m 230 m
Piramidi ya Khefren Khafre ~ 2558

-2532 KK 143.6 m 136.4 m 215.25
Piramidi ya Mykerinos Menkaure 2558

-2532 KK 65.55 m 62 m 102.2 m

x 104.4 m
Piramidi hizo zote hazikukaa peke yake bali zilijengwa pamoja na majengo ya kando.

Kila piramidi ilikuwa na mahekalu mawili ambako makuhani walitoa sadaka kwa ajili ya roho za mafarao marehemu peponi. Hekalu 1a kwanza lilijengwa mbali kidogo, kwenye chanzo cha barabara ya maandamano yaliyoendelea hadi hekalu la pili karibu na piramidi. Njia hizo za maandamano zilitumiwa hasa wakati wa sherehe za kumkumbuka farao.
Kwa kawaida malkia (wake wa farao) walizikwa katika piramidi ndogo au makaburi mengine kando ya piramidi kubwa. Piramidi za Kheops na Mykerinus huwa na piramidi 3 za malkia wa kila mfalme. Kwenye piramidi za Khefren hakuna makaburi ya malkia yaliyotambuliwa.
Historia ya baadaye

Tangu siku za kale watu walichukua mawe kutoka majengo ya Misri kwa kuyatumia katika majengo ya nyakati zao. Hii ndiyo sababu ya kwamba kimo cha piramidi kimepunga na hasa mawe mazuri yaliyofunika nyuso za piramidi yamepotea.

Katika karne ya 12 BK mtawala wa Misri al-Malek al-Aziz Othman ben Yusuf alijaribu kubomoa piramidi akizitazama kama ushahidi wa upagani wa kale. Wafanyakazi walianza kukata mawe kutoka piramidi ndogo ya Mykerinos lakini ikaonekana ya kwamba kazi ya kubomoa labda ingekuwa ghali sawa na kujenga. Baada ya miezi kadhaa shughuli hizo zilisimamishwa na hadi leo kuna pengo katika ukuta wa kaskazini.
Da'Vinci Mshana Jr
ledada warumi Bilionea msigwa
 
Inasemekana kwamba katika bara la Antactica kulikuwa na CIvilizaiton ya jamii iliyoendelea sana sana na walikuwa na kimo mara mbili ya binadamu wa kawaida. Inasemekana nao walijenga ma pyramid ambayo yameanza kuonekana baada ya barafu kuanza kuyeyuka. Inasemekana kwamba mataifa makubwa yamekuwa yakifanya project za siri huko na taifa la kwanza kufanya hivyo lilikuwa Germany wakati wa Hitler.
Ukifuatilia sana kuhsu watawala wa jamii nyingi za kale walikuwa na vichwa vyenye visogo vilivyo vutika sana nyuma. Kuna pharaoh mmoja naye alikuwa hivyo hadi ikadaiwa alikuwa na tatizo la kigenetic kwakuwa walikuwa wanaoana kaka na dada lakini hata Mexico ya kale watawala wengi walikuwa wana visogo vya hivyo.
inadaiwa kwamba hawakuwa na tatizo la kigenetic ila walikuwa ni watawala waliotokana na hiyo jamii iliyokuwa na maarifa mengi iliyokuwa ikiishi Antactica ambayo hata genes zake hazina uhusiano na binadamu.
 
Mkuu hiyo stori nilisikai mahali bado naifatilia

Nikiipata nitaileta hapa jf
 
Hizo ni figisu za mazeru zeru ambao pamoja na kufaham bayana kuwa pyramid na masalia mengine ya kale yalikuwa ni ustaarabu wa kiafrika, wamekuwa na kazi ya kuwaaminisha watu vinginevyo.. utakuta wanayumbisha habari hizi na kuzihusisha na viumbe wa sayari zingine. Hii siyo kweli bali propaganda za albino, kwani huwa hawaamini na wala hawapendi kuona dola kuu kama za Khemet ya kale zikihusishwa na watu weusi wa Africa.. tujihadhari na hadaa za mitandaoni
 
Pyramids za Giza hazikuwa makaburi ya mafarao,hakuna hata moja ambalo mlikutwa mwili uliohifadhiwa(mummy) wala maandishi hieroglifics zinazoashiria kuwa yalikuwa makaburi.

Pia hazikuwa mahala pakuabudu wala monuments,zina precision ya hali ya juu,zimefuata kanuni zote za hisabati na mpaka leo bado haijaeleweka vizuri yalijengwaje jengwaje na lini.

Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa zile pyramids zilikuwa sehemu ya Power plant ya kuzalisha na kusambaza umeme.
 
Kuna scrolls zilichibwa mesopotania zinaeleza story moja ya ajabu kuhusu hawa viumbe, kuhusu south africa, na mambo mengine ambayo yalitokea zaidi ya miaka bilion mbili zilizopita. Nikipata muda nitakuja kuandika. Kuna mambo mengi kwenye hii dunia ninahisi hayajafahamika historia ya mwanadamu haianzii kwa Adam inaelekea Mungu alitupatia kile ambacho alikuwa na hakika kinatuhusu sisi kama sisi na ndiyo maana hata katika Biblia kuna sehemu baada ya Kane kumuua abel tunaambiwa aliwekewa alama asije dhuliwa na watu wengine na akaenda mataifa ya mbali ambapo alioa huko.
Hii ina maana kulikuwa na jamii nyingine ya watu mbali na Adam na Eva pamoja na Kane na ndugu yake Abel.
 
Pyramids za Giza hazikuwa makaburi ya mafarao,hakuna hata moja ambalo mlikutwa mwili uliohifadhiwa(mummy) wala maandishi hieroglifics zinazoashiria kuwa yalikuwa makaburi.

Pia hazikuwa mahala pakuabudu wala monuments,zina precision ya hali ya juu,zimefuata kanuni zote za hisabati na mpaka leo bado haijaeleweka vizuri yalijengwaje jengwaje na lini.

Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa zile pyramids zilikuwa sehemu ya Power plant ya kuzalisha na kusambaza umeme.
ziko so accurate kiasi kwamba hata errors zilizopo kwenye ujenzi ni very minor ni zaidi ya zile zilizokubaliwa na field ya engineering. Yani mpaka leo ni kweli kwamba wanasayansi wanaumiza vichwa kujua iliwezekanaje hao watu wakaweza kujenga hizo pyramid.
 
Back
Top Bottom