malimangapi
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 238
- 48
CDM hawajanunua mtanzania yeyoye. Lakini mtu yeyote mwenye akili timamu anaona wapi CCM wanakoipeleka nchi yetu. Wanaipeleka kwene kufilisika, huku viongozi wajuu wachache wakijaza matumbo yao kwa ulafi. Njia pekee ya kuiokoa nchi yetu ni kwa kuing'oa CCM madarakani. Usifikiri utakuwa salama wewe na dini yako, kwa sababu mfa maji hutumia kila njia kutaka kujiokoa. Utapata uhuru wa kuabudu katika utawala wa haki unaoheshimu sheria na haki ya binadamu. Hivi haviko CCM, ndio maana unaona kila siku damu zinamwagika kuanzia Visiwani hadi Bara, huku watu wasio na hatia wakibambikiziwa kesi nzitonzito ili kuwanyamazisha, lakini siku zote haki itatawala dunia. Amka uupinge huu udhalimu. Kwa pamoja tutashinda.