PINDA: Ukiwa mkaidi usilalamike pale kichapo kitakapokufikia

Kama nilisikia vizuri muheshimiwa pinda alisema kipigo ni kwa yule atakayeleta vurugu au kuwa mkaidi me sidhani kama kuna tatizo hapa coz hata nyumabani mtoto akileta vurugu anashushiwa kipigo ili kumnyosha so nashangaa kuona mtu mwenye akili timamu akiona ni uaonevu kwa mtu mvunja amani kushughulikiwa tuache uchama jamani tusimame katika ukweli

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wapigwe tu maana tumechoka nami nasema wapigeni tu,je raia na wao wakiamua kuwapiga polisi maana wanaishi wote mtaani nani wa kulaumiwa.
 
Lkn siku zao zinahesabika watatoka tu hawa wakoloni weusi maccm,na polisiccm tutawachinja kama kuku mtaani we tulia uone
 
Inabidi tufike wakat kwa pamoja tukubaliane Pnda alikengeuka kwa kauli hii, laiti tungeonja madhala ya kipigo cha polic tungejua sio wanaopinga amri ya polic tu ndo wanaodhulika, hata wapita njia.mfano yule mkenya alokufa Arusha hakuwa na interest yoyote na chadema hivyo nidhahil hakusika.katiba ya nchi hairuhusu ilo. bado watz tunaitetea kauli ile?tusiwe watumwa wa fikra na mali, hii aman ndogo tuliyonayo ikitoweka ni cc tena tulioamliwa kupigwa ndo tutaangaika.wao wanatiket tayar za ndege
 
Kama akufikiria si afute hiyo kauli maana huu ni uchochezi ingelikua ni mbunge wa chadema ingekuaje ,sijawaiona waziri mkuu pumbavu kama pinda
 
Sasa nimejua ni kwanini watu wanakatwa kucha. Sijajua anatisha watu au ndo utawala bora /uongozi bora, enzi za mwalimu ulikuwa ni uongozi bora siku hizi unaitawala bora? Maanake kuna watawala wanaochuma na wanatawaliwa walioahidiwa maisha bora sasa wanaambulia kipigo cha mbwa mwizi? Eeh mola tuokoa na manayang'au hawa? Turejeshee mwalimu aliyejua shida za watu; akiona watu mabarabarani wanaomba anajua ni yeye akiona watu wanakufa kichwa kinamuuma; nyerere alikonda miaka yote ya kuoongoza kwasababu alibebamzigo wake sawasawa. Leo wanaoongoza kwa kuwakoga watu kwa suti na umaridadi kwa hela za ufisadi wa nchi yetu? T ni bahati mbaya kuwa na watawala wa namna hii. Maisha bora kwa kila mtz yako wapi???????????????????????????????????????????????????
 
Waziri Mkuu Mh Pinda amesema nchi inaendeshwa kwa misingi ya sheria,yeyote atakayeleta vurugu na fujo na akazuiwa na akakaidi atashughulikiwa, naunga mkono agizo hili,

Kwani vurugu ni nini? mbona tafsiri yake hauiweki wazi? Polisi anaweza akamtamani mkeo akaja kukukamata akikuita wewe ni orodha ya vurugu (kama Pinda anavyoadai) na kukuua .... na akawa huru kwa amri ya Waziri Mkuu .... au akawepo mtu anayetaka mali zako au vinginevyo .... akawalipA polisi wasio waadilifu wakakuua wakikuita mleta vurugu jamaa akachukua Mali zako na usiwe na haki.... au machimboni ambako polisi hunyang'anya mali za raia sasa wamepewa uwezo zaidi ni kuuua mtindo mmoja....hakuna atakayekua salama hata hawa wapiga debe watauawa tu hakuna wa kupona
 
Waziri Mkuu Mh Pinda amesema nchi inaendeshwa kwa misingi ya sheria,yeyote atakayeleta vurugu na fujo na akazuiwa na akakaidi atashughulikiwa, naunga mkono agizo hili,


Misingi ya sheria unayoijua wewe ni ipi? au una kariri tu? unadhani watu wakiuawa baada ya kauli ya Pinda yeye atakua huru kwa misingi hiyo hiyo ya sheria?

Labda anajua siku zake za kuishi zimekwisha sasa anajisemea alitakalo...!
 
Waziri mkuu akijibu swali la Mangungo kuhusu khali tete inayoendelea nchini hasa huko Arusha - amesema wale wanaovunja sheria polisi wawapige tu! Waziri mkuu akijibu swali bungeni amesema wao kama serikali wamechoka hvyo ni ruksa vyombo vya dola kupiga wananchi ambao ni wakaidi.

Ameongeza kuwa orodha ya wakaidi inajulikana na watachukuliwa hatua, zaidi ya hayo amesisitiza kuwa yeyote atakayeleta ukaidi asilalamike atakapoona kipigo kinamwangukia.
Mkuu unawaza karibu sana sidhani kama huu ni uchonganishi kwa hiyo unataka watu wafanye fujo waachwe tu,hiyo siyo kweli jiulize tena.
 
Hakufikiria wakati anatoa hiyo kauli

Hapana aliamua kuufichua unyama wake alionao moyoni mwake.... Pinda hajawahi kuwa mkweli kwa lolote pamoja na machozi ya karibu aliyonayo, ndani ya Tanzania ndio kauli kama hizi hutolewa na viongozi na zikaungwa mkono.....ila kauli km hizi kwa nchi za wanaojua kusoma na kuandika hua ni hadimu sana kuzosikia....!
 
"Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye ukaamua kukaidi, utapigwa tu... Eeh hamna namna nyingine, eeh maana lazima tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria. Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi watakupiga tu. Na mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine eeh. Maana tumechoka!." (By Hon Mizengo Peter Pinda).

Great thinkers - hebu tutafakari kwa kina maneno haya yaliyotamkwa na Waziri Mkuu na umuhimu wake katika kujenga jamii ya kidemokrasia inayoheshimu sheria bila shuruti.

Kwa mtazamo wangu muktadha wa alichokisema ni sahihi kabisa yaani hatutakiwi kukubali kuwa na jamii isiyoamini katika kufuata sheria na taratibu zilizopo "impunity". Kila kitendo cha uvunjifu wa sheria lazima kiwe na matokea mabaya kwa mvunja sheria. Ila kwa upande mwingine maneno haya yana hatari kubwa ya kutafsiriwa na hata kutumiwa vibaya na walinzi wa usalama wenye uelewa mdogo wa sheria. Wanaweza kabisa kuacha maneno mengine yote wakachukua sentenso ya mwisho yaani ile inayosema - "Na mimi nasema Muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine eeh. Maana tumechoka". - na kuifanyia kazi kama agizo la afande.
 
... Ila kwa upande mwingine maneno haya yana hatari kubwa ya kutafsiriwa na hata kutumiwa vibaya na walinzi wa usalama wenye uelewa mdogo wa sheria... - "Na mimi nasema Muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine eeh. Maana tumechoka". - na kuifanyia kazi kama agizo la afande.

Hivi wewe unaamini walinzi wetu wa usalama wana uelewa mkubwa? Wengi wanauelewa mdogo na hawatakiwi kuwa na elewa mkubwa. Wakiamrishwa huwa hawaulizi, wanatekeleza kama hawana akili nzuri, tena watalazimisha uwape mshiko hata kama wewe ndo mlalamikaji!

Ukiwauma sikio kuhusu mhalifu, watakwenda kumkamata na watakutaja wakishikishwa vijisenti! Askari wetu ni majanga!
 
Back
Top Bottom