PINDA: Ukiwa mkaidi usilalamike pale kichapo kitakapokufikia

Magesi

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
2,587
573
Waziri mkuu akijibu swali la Mangungo kuhusu khali tete inayoendelea nchini hasa huko Arusha - amesema wale wanaovunja sheria polisi wawapige tu! Waziri mkuu akijibu swali bungeni amesema wao kama serikali wamechoka hvyo ni ruksa vyombo vya dola kupiga wananchi ambao ni wakaidi.

Ameongeza kuwa orodha ya wakaidi inajulikana na watachukuliwa hatua, zaidi ya hayo amesisitiza kuwa yeyote atakayeleta ukaidi asilalamike atakapoona kipigo kinamwangukia.
 
Akijibu swali bungeni la maswali kwa waziri mkuu, pinda amesema wale wanaovunja sheria polisi wawapige tu..
Hivi hili linaruhusiwa kweli?..
 
Leo tar 20 waziri mkuu PINDA aruhusu vyombo vya dola kutumia nguvu kukabiliana na raia. Karuhusu kuwapiga wanapoleta shida. Hivi Polisi wanaruhusiwa kupiga raia wanapowakamata?Kisheria
 
Nimestuka kwa jinsi alivyojibu swali la Mwangungu alietaka kujua kwa nini polisi wanawapiga raia huko mtwara na sehemu nyingine..
Jibu..
''wawapige tu! Kama hawataki kufata sheria wawapige tuuuu'' jamani ni sawa kweli.. Naanza kuamini ccm wanawatuma polisi kwenda kuua na kupiga raia
 
Nimestuka kwa jinsi alivyojibu swali la Mwangungu alietaka kujua kwa nini polisi wanawapiga raia huko mtwara na sehemu nyingine..
Jibu..
''wawapige tu! Kama hawataki kufata sheria wawapige tuuuu'' jamani ni sawa kweli.. Naanza kuamini ccm wanawatuma polisi kwenda kuua na kupiga raia

huyo ndo msukule Pinda Mkatoliki na mpenda amani AMEJICHOKEA PINDA WAWATU!
 
Wanajf, salaama. katika hali ya ajabu,mh Mh. Mangungu akauliza swali kwa nin askari wanaumiza wananchi. Waziri mkuu amejibu,serikali imechoka ,wajeuri wamezidi. Na ameagiza askari wapige hata kuua mana hamna njia nyingine. Raia wote wakaidi wapigwe na wauawe. Sasa nchi inaingia vitani kwa kuua raia wate. Pinda ameondoa katika katiba kipengele cha haki za binadamu. Serikali inapaswa kuodhi madaraka kutoka kwa wananchi ila apa askari wanaruhusiwa kupiga kuua. Pinda asante kwa kuruhusu tufe.
 
Wana po kukamata unatakiwa kutiii kukukamatwa usipo tii watakulazimisha kutii kulingana na nguvu zako, ifikie mahara tuache kuweka vitu vinavyo chochea vurugu badala yake tuweke vitu vyenye maslahi kwa nchi yetu.
 
Waziri Mkuu Mh Pinda amesema nchi inaendeshwa kwa misingi ya sheria,yeyote atakayeleta vurugu na fujo na akazuiwa na akakaidi atashughulikiwa, naunga mkono agizo hili,
 
vurugu zimekuwa zikitokea hasa katika mikoa ya Mtwara na Arusha. Na ni dhairi inajulikana kuwa vurugu hizi zinatokana na uchochezi wa kisiasa. Mambo haya yamekuwa yanatishia amani ya Nchi kwa ujumla. Akijibu maswali ya papo kwa papo, Mh. Waziri mkuu ametoa rai kuwa orodha ya wakaidi inajulikana na watachukuliwa hatua, zaidi ya hayo amesisitiza kuwa yeyote atakayeleta ukaidi asilalamike atakapoona kipigo kinamwangukia.
 
Piga tu.... Yule anaekaidi kushikwa..
Nadhani huyu kiongozi ameshiba madaraka kweli kweli..
Hivi polisi wetu walivyo na sifa si watawauwa raia kwa kipigo! Sasa tujipange kwa vipigo vya kufa mtu, tutang'olewa meno na marungu..
LAKINI MUNGU YUPO...
MAPAMBANO YATAENDELEA.. HATA WAKIWATISHA
 
bora ametoa ruhusa, sasa tunataka polisi wafanye mambo yao. Kiga hawa wafanya fujo mpaka wasahau nyumbani ni wapi.
 
Akijibu swali bungeni la maswali kwa waziri mkuu, pinda amesema wale wanaovunja sheria polisi wawapige tu..
Hivi hili linaruhusiwa kweli?..

Kumbe watoto wakitoka Madrasa wanakuwa wamevunja sheria kiasi cha kupigwa risasi? Maana baadhi ya watoto waliopigwa risasi na wengine kufariki katika sakata la bomu Arusha walikuwa wakitokea Madrasa.
 
Back
Top Bottom