Pinda na Uwaziri Mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda na Uwaziri Mkuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jallen, May 4, 2012.

 1. Jallen

  Jallen JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Kwa kuwa katiba inasema Rais atashauriana na Waziri mkuu kuteua mawaziri basi bila shaka waziri mkuu wa kushauriana nae ni Pinda.
  Kama Pinda alishindwa kuwakemea mawaziri waliopo je hao watakaoteliwa leo atawaweza.
  Hii ni kujaza mvinyo mpya kwenye chupa kuukuu. Baraza lilitakiwa livunjwe apatikane waziri mkuu mwingine, aidhinishwe na Bunge kisha akashauriane na Rais katika kuteua mawaziri wengine. Hata wakiteuliwa mawaziri wazuri kiasi gani upole wa PM ni tatizo pia.
   
 2. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kweli ndivyo katiba inavyosema, but in practice JK hahitaji ushauri wa Pinda. kama ingekuwa hivyo, Pinda angekuwa anachommeka watu wake humo.

  Kumbuka JK alishasema urais wake hauna mbia!!!
   
 3. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuna mantiki kubwa katika swali lako, assume mnatoka uchaguzini. Huyo PM uliyemchagua dakika kadhaa alikuwa ni mbunge tu.

  Wewe ulipofanya selection ulitumia machinery kama Usalama wa Taifa na kila kilicho ndani yua uwezo wako kuwajua na kuwa -vet uliowataka.

  Je, huyu PM ambaye dakika chache alikuwa mbunge, katumia machinery zipi kukushauri unaowataka.

  Afadhali wewe uchaguzini na kwenye kampeni ulikuwa na list yako ukijua kwamba ukisshinda watakaoukusaidia ni kina fulani. PM ameshtukizwa tu kimantiki hakuwa na maandalizi yoyote.

  Hivyo, ushauri wake unatiliwa shaka afadhali wa makamu wa Rais.

  Hivyo, mkuu, hii yako ni hoja hata kama umeijenga kwa ufupi, nina imani wataalamu wanaweza kuijenga vilivyo. Na sisi humu JF tulijadili kadiri tuwezavyo
   
 4. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ambacho anafanya rais ni marekebisho tu ya baraza sio kuvunja, maana kama anavunja ingebidi avunje, ateue waziri mkuu ndani ya siku 7 au 14, harafu waunde baraza la mawaziri. Hivyo kama hakuvunja baraza Pinda yuko ndani, ndo atashauriana naye kufanya mabadiliko. Vinginevyo atakuwa anavunja katiba, ambacho nadhani japo hamnazo hawezi fanya hivyo.
   
 5. Jallen

  Jallen JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Hoja yako ni ya msingi sana, kumbe ni vyema wakati wa Kampeni ya Urais chama husika kiwe na mkakati madhubuti wa kujua PM wake atakuwa nani kama ilivyokuwa kwa JK na EL hawa walijuana vyema na hata ushauri wa EL katika kuteua baraza la mawaziri ulizingatiwa sana lakin huyu PM wa kuchukuliwa katikati ya safari ni vigumu kuchukua ushauri wake
   
Loading...