Pinda: Madhehebu madogo ni yapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda: Madhehebu madogo ni yapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nikupateje, Aug 14, 2011.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mbunge Suzan (CHADEMA) amewasha moto ambao serikali haikuutarajia.

  Alitumia kipindi cha maswali kwa Prime Minister kuiomba majina ya maaskofu wauza unga.

  Tunajua wote Pinda alisema kuwa ni madhehebu madogo.

  Kauli ile ya rais ilitolewa mbele ya Maaskofu wa Katoliki.

  Tatizo ni kwamba Pinda hakufafanua dhehebu dogo ni lipi na kwa vigezo vipi.

  Nchini Egypty, Papa hana wakatoliki wake maana kule kuna Eastern Church. Wanafanana na wakatoliki lakini hawako chini ya Papa na hata Christmas yao ni January 06 na si Decemba 25.

  Hawa wana tawi lao pale Musoma

  Roman Catholic (RC)ni dhehebu la huyu Suzzy (CHADEMA) aliyeuliza swali, vilevile dhehebu la Pinda mjibu swali lakini pia Anne Makinda, Andrew Chenge, Bernard Membe, Mary Nagu, Lyatonga Mrema (TLP), Selasini (CHADEMA).

  Kule Egypt hili RC lao ni kama halipo kabisa wakisafiri huko inawabidi wasali hili la Egypt ambaye Papa wao yuko Alexandria.

  Je, kule Egypt dhehebu la Pope Benedict XVI unaweza kuliita dogo?

  WanaJF,

  Nadhani tuweke orodha yetu humu ili tujue madhehebu madogo ni yapi na kwa vigezo gani walau tupime muelekeo wa mkatoli Mizengo Pinda.

  Mimi ni mkatoliki pia. Wakatoliki tunahesabu makanisa menzetu ni yale ya Eastern Church hata kama tulikosana miaka elfu iliyopita kama hili liloko Egypt.

  Zaidi ya hapo wengine wote tunawaita 'protestant' na kwa kuwaheshimu tunawaita 'Christian Community' yaani 'Vikundi vya wakristo'.Hatuwaiti kanisa au madhehebu. Niko kwenye phone mode nikiingia kwenye laptop yangu nitawapa link ya Vatican website inayoeleza hili kwa urefu, bila woga wala aibu inapofafanuliwa dhana ya 'Apostolic Succession'. Unaweza ku-mwenyewe maneno haya (Vatican+appostolic succession).

  Hivyo mimi mkatoliki nikisema Mlutheri ni dhehebu ukweli tunapozana hasira na kujenga amani tu, lakini ukweli umo kwenye hii website ya Vatican na si kejeli zangu mimi kama mleta post hapa JF eti hadi post yangu izuiwe, iwe-moved au nipigwe ban.

  Nimewataja wanasiasa ambao ninawajua ukatoliki wao vizuri. Anne Makinda anasali kila siku misa ya asubuhi kabla hajaingia bunge. Parokia yake akiwa Dodoma ni KIWANJA CHA NDEGE. Selasini (CHADEMA) sijui kama bado ni mwenyekiti wa walei Jimbo la Dar. Gaudence Lema yule meya-mzozo wa Arusha ni kiongozi mmojawapo wa jimbo la Arusha kama Selasini kule Dar.

  Hivyo ninawajua vilivyo hawa wakatoliki wenzangu, wakiniona kwa sura watanijua.

  Taabu yangu kwao ni jinsi hawa wakatoliki mle bungeni hasa wa CCM hawakujijua jibu la juujuu la mwenzao Pinda litaleta madhara gani.

  Tazama sasa maaskofu wetu wakatoliki walivyokuja juu baada ya jibu la muumini wao Pinda bungeni. Matokeo yake hata hayo anayosema ni madhehebu madogo ataishia kushindwa kuwataja.

  Ndiyo maana mimi nimeamua tujaribu humu JF kuya-list hayo madogo tuyajue.

  Tutakapoanza kuyataja ndipo tuone impact humuhumu JF na MOD waiache thread isifutwe.

  Tukianza kuyataja basi mimi nitasimamia hoja kwamba protestant wote ni madhehebu madogo kama mnavyoona wakubwa wangu huko Vatican wanavyosema ambao ni wakubwa wa Pinda, Makinda wenzao wote wakatoliki ndani ya CCM walioshangilia jibu lile.

  Idumu JE thd best informed media in TZ.
  .
   
Loading...