Pinda kwa hili Hapana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda kwa hili Hapana.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DENNING, Jun 25, 2011.

 1. D

  DENNING Senior Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 172
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Kwanza nianze kwa kusema ninamheshimu sana Waziri mkuu wangu Pinda, ajiitaye mtoto wa mkulima, lakini kwa hili la kutoa hoja dhaifu kuhalalisha posho za vikao naomba kutofautiana naye.Hebu tujikumbushe hoja hizi ambazo kimsingi sikutegemea kama zingetolewa na mtu anayetegemewa kuwa makini kama Waziri mkuu wa nchi, tena anayejiita mtoto wa mkulima. Hoja ya kwaza ni kwamba POSHO HIZI ZIKO KISHERIA na ya pili eti WABUNGE HATA HIVYO HAWAZITUMII WENYEWE BALI WANAWAPA WAPIGA KURA WAO.
  Hoja hizi kama zisingetolewa na Pinda mtu ninayemheshimu, basi ningeziita HOJA HEWA.Lakini kwa vile ni Pinda sitaziita hivyo ila ntazijadili tu. Ntaanza na hoja ya kwanza eti hizi posho ziko kisheria. Kwanza Pinda ameshindwa kujielekeza katika hoja iliyokuwa mezani badala yake amechepuka na kujisemea lililokuja kichwani mwake. Hoja ya msingi haikuwa juu ya kama posho hizi ziko kinyume na sheria au la bali kilichokuwa kinatakiwa kujibiwa ni juu ya tuendelee kuwalipa wabunge posho au la.
  Je kila kilichopo kisheria ni ni kizuri? au kila kilichopo kisheria kama kitaonekana kuwa kibaya hakiwezi kurekebishwa?.
  Kwa swali la kwanza Jenerali Ulimwengu ashajibu, kwamba si kila kilichowekwa kisheria ni kizuri. Nami naongezea mfano hapa kwamba serikali ya Makabulu wa South Africa ilikuwepo kisheria na iliwabagua waafrika kwa mujibu wa sheria. Lakini hili halikuacha kupigiwa kelele ati kwa sababu jambo hilo(serikali ile) lilikuwepo kisheria. Pinda ni mwanasheria wote tunajua.Ina maana Pinda ashasahau juu ya Sheria mbaya (Unjust law). Kama amesahau, manake yupo katika siasa siku nyingi labda hasomi tena vitabu vya JURISPRUDENCE vinavyoeleza juu ya sheria mbovu na dawa yake nini (kamsome Sengodo Mvungi, The Right to Disobey Unjust Law, East African Law Review, 2003).
  Kwa hiyo ni wazi Pinda amekataa makusudi kutwambia kama yeye mwenyewe na serikali yake yuko tayari kuandaa marekebisho ya sheria kuzifuta posho hizi. Kama ilivyo kwa watoto wa wakulima wengi, na mimi sikumwelewa kabisa Pinda.
  Hebu twende katika hoja nyingine dhaifu mno iliyotolewa kutetea posho hizi, ya wabunge siyo wanaozitumia fedha hizi badala yake ni wapiga kura wao wanaoenda kuwaomba pale bungeni.Mimi nafikiri katika hili pinda anapaswa kuomba radhi kabisa kwani ni wazi amewatukana wapiga kura waliopo majimboni waliowapigia kura wabunge wale.We hebu jiulize ni wapiga kura wangapi kutoka Katavi anakotokea Pinda wanaenda viwanja vya Bunge kumwomba Pinda pesa.Au wale wakuu wa wilaya na madiwani wanaotamburishwaga katika bunge ndo wapiga kura wanaoombaomba pesa kutoka kwao?. Hivi ni wangapi wanatoka jimbo la Wawi kwenda Bungeni kumwomba hela Mh. Rashidi? wangapi kwa wiki Pinda twambie. Au wangapi wantoka Karagwe kwenda kumwomba bwana Katagira, mbunge wa kyerwa?.
  Pili Pinda ni mkristo, tena amesoma seminali.Anaijua sana dini na ninaamini anamwogopa mungu. Sasa Pinda leo atwambie ametoa wapi andiko katika Biblia linalomwelekeza kuwasaidia maskini wanaotoka kwenye jimbo lake kumwomba fedhe kisha atangaze kwamba anawapa fedha hao ombaomba.Hii ni dhambi kubwa sana inayopaswa kuungamwa.Na kama hatofanya hivyo basi sidhani kama huruma ya mungu haina kikomo kwa mtu asiyejutia dhambi yake.
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa hili la posho, mimi pia linanipa shida kulikubali. Nchi ina matatizo mengi na posho hizi zinahitajika sana kupunguza matatizo na hata migogoro mingine inayohusu ukosefu wa fedha.
   
 3. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  umenena kweli tupu, Big UP. Tuseme hivi kutetea hoja ya posho za vikao inawezekana katika mazingira ya aina mbili tu. Moja kwa mtindo wa wabunge kupiga kura kichama... yaani wingi tu bila hoja. Pili ni kama huna sound mind...namaanisha una matatizo upstairs. Utetezi weak wa Pinda ni ushahidi tosha wa hizo argument mbili hapo juu. Tukumbuke kuwa waziri mkuu ni taasisi kubwa lakini pamoja na ukubwa imekuwa ni vigumu kutoa hoja ya kutetea posho... Matokeo yake ni Pinda kuwa na utetezi ambao umeidhalilisha serikali kwa kiwango cha juu sana.
   
 4. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Magamba hili hawalioni cjui kwanini.
   
 5. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ukiendelea hivi utakomaa kisiasa na kichambuzi! Karibu JF
   
Loading...