Pinda kuutema Uwaziri Mkuu?

Pinda kuutema Uwaziri Mkuu?

hamtambui lolote , pinda ndy waziri mkuu bora kuliko wote waliyomtangulia kwa nn,,maamuzi mengi amekuwa akitoa baada ya kufanya uchunguzi kwa kina mdo maana ktk kauri zake zimekuwa zikitoka kwa umakini mkubwa bila kuingilia mamlaka zilizo juu yake ama chini yake.
 
Now basi watanzania tuache kushikiwa akiri zetu na watu wengine wakazichezea na kuzifanya wanavyo taka wenyewe na sisi tukafuata kama wanavyo taka basi........pufikie wakati tujue maana ya system basi kwa msaada zaid "system as a collection of interrelated components that work together toward a collective goal" so leo ukiniambia Pinda anataka kuutema PM unakuwa uongo na uzandiki mkubwa katika anga hii because Pinda is one among the component in a system, so hamna fact ya kumkosha moja na kumchafua mwine. Hatutofika hivyo... na tutoweza kujenga Tanzania mpya kwa taarabu kama hizi zisizo na mashiko kwa Taifa na wananchi
Defn na maelezo yako yana kaukweli lakini ni tofauti na hali halisi. Kwa maelezo yako, alipojiuzulu Lowasa ilitakiwa system nzima iodoke, mbona haikuwa hivyo?
 
Wadau!!!

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio yanayoonesha wazi kuwa serikali imekosa control juu ya utawala wa nchi. Matukio ya mapambano ya polisi na wamachinga mkoani Mbeya, machafuko ya Arusha na Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Aidha mchakato wa katiba mpya umeielemea serikali na haioni ni wapi pa kutokea. Kauli ya Mbunge wa Monduli na M/kiti wa kamati ya bunge ya ulinzi na Mambo ya nje na PM mstaafu Mhe. Edward Lowassa kutahadharisha kuwa wakati wowote bomu la machafuko laweza kulipuka ni mwiba mwingine kwa serikali. Hivi sasa serikali inasononeshwa na kauli mbiu ya CHADEMA ya peoples power kiasi cha kuifanya kutojua ni nini kitatokea kesho. Suala la Jairo lilimfanya Mhe. Pinda kunyong'onyea na hata kujinyanyapaa mwenyewe mbele ya bunge na hata raia wa kawaida.

Kwa siku za karibuni PM Pinda ameonesha wazi kuwa ni kama kiongozi asiyekuwa na mamlaka yoyote ktk utendaji kazi na kila jambo lazima lifanywe na Rais au maagizo toka kwa Rais pekee. Kwa ujumla amekuwa ni kama ceremonial Prime Minister!! Kwa hali inaonesha wazi amekata tamaa na anaona bora liende ili mradi anapata mshahara na marupu yake. Kwa jinsi mambo yanavyozidi kuharibika ni wazi Rais Kikwete anaweza kufanya mabadiliko makubwa ili kuepuka serikali nzima kuondoshwa madarakani kwa maandamano au kura ya kutokuwa na Imani na serikali bungeni!! Watch out and see!!

Kinacho ongelewa hapa kinaukweli ndani yake, maana hivi majuzi uongozi wa juu wa jeshi la police walikutana jijini Arusha na kuzungumzia haya yote, kwanza ilikuwa ni ishu ya chadema na kuomba kuongea na m/kit wa chama hicho kusaidia kupooza hali tete ya nchi maana maamuzi ya nchi kuendelea kuwa na Amani yapo chini ya CDM. Pili mzee wa magogoni hashauriki kutokana kufanya maamuzi kisiasa na kujisahau kuwe yeye ni kiongozi wa wote na hii ni pamoja na yale yanayoendelea Arusha.
 
Mimi nadhani ni waziri mkuu dhaifu kujiri kuliko wote tuliowahi kuwa nao. Ngoja tuone itakuwaje?
Unategemea waziri mkuu anayetokana na uteuzi wa rais dhaifu aweje? Kwa vyovyote lazima awe dhaifu kama boss wake.
 
Muheshiwa Pinda ni waziri mkuu mzuri kiutendaji, tatizo bosi wake( mkuu wa kaya kichwa boz JK) ndy boya, sasa ukifanya kazi na boya hata we utaoneka boya tu!! hata kama muheshimwa pinda angefanya kazi usiku na mchana ni bure.
 
From the economic point of view ni bora aendelee kuwa naye hadi 2015. Kwani kama atamtoa
na kuchagua mwingine utakuwa ni mzigo kwetu walalahoi kwani idadi ya viongozi wakuu wastaafu
tunao wahudumia kwa kodi zetu itaongezeka. Kumbuka katiba yetu inasema hata wale waliokwisha
fariki tutaendelea kuzihudumia familia zao hadi MASIYA atakaporudi duniani.

Pia hii itupatia a food for thought kwenye katiba mpya. Hivi kwa system yetu ambayo tuna RAIS
mtendaji kuna ulazima gani wa kuwa na PM? Kwanini tusiwe na VP tu kama USA?
Pendekezo langu hivi vyeo kama PM, RCs, DCs vinatakiwa viondoshwe kabisa kwenye KATIBA
MPYA ni unnecessary mzigo kwa nchi masikini kama Tanzania.
 
hakuna waziri mkuu mnafiki katika taifa hili kama Pinda, daima anataka kuonekana ni mwema kwa watu wa makundi yote yanayohasiamiana, kwenye ishu inayohitaji maamuzi huyu mzee hawezi kutoa maamuzi ni bora aende tuuu
 
Mtoto wa Mkulima kwa kweli amechoka kama Magamba walivyochoka,Sasa jamani mnadhani mnaweza kupata PM bora katika system Mfu? Waacheni Wafu wakazike wafu wenzao,Mwacheni Mtoto wa Mkulima alazike Magamba yake!!
 
Nchi hii itarudi barabara pale kapteni lowasa atakapo shika hatam
 
hamtambui lolote , pinda ndy waziri mkuu bora kuliko wote waliyomtangulia kwa nn,,maamuzi mengi amekuwa akitoa baada ya kufanya uchunguzi kwa kina mdo maana ktk kauri zake zimekuwa zikitoka kwa umakini mkubwa bila kuingilia mamlaka zilizo juu yake ama chini yake.
vipi kuhusu sakata lake na magufuli hadi kupelekea magufuli aandike barua ya kujiuzulu? Vipi kuhusu kauli yk juu ya mauaji ya Arusha?
 
mwanri ni mchapakazi na anafaa kuwa pm,.mtazamo tu.
 
nadhani sitakuwa namtukana au kumdhalilisha nikimtazama mh pinda na msukule. sidhani kama pinda ana kauli yoyote kuhusiana na governance ya nchi hii. maamuzi yote atafikishiwa tu. na kama akidiriki kutoa amuzi lolote, tai atamshukia na kumwacha ameumbuka kama ilivyotokea kwa jairo. kwa mtu anayegharimiwa hela nyingi na walipa kodi wa nchi hii kama pinda, hana faida kuwepo ktk uongozi wa nchi hii. kisiasa, kiutu na kiuungwana, ni bora tu yeye mwenyewe angejitoa kwenye uongozi wa utawala kabla hajapigwa chini na kuwa branded ni under performer.
 
Back
Top Bottom